Zai pokea likes milioni laki kumi na tano elfu sabini na mia tatu na nusu......
I always wanted to give them that kind of an example lakini nikaona kwa kuwa their hearts are full of hatred they won't even get my point.
Watu kama Dully Sykes walau you can dare to call them kings..
Coz toka wanaanza hawajawahi kukosea wala kushuka....na ukianza kupanga nyimbo zao na ukaanza sikiliza hata sasa bado zinakupa burudani kama uloipata wakati nyimbo zinatoka..
Msanii ambae anafata hizo nyayo ni chibu kwa sasa...
Ukianza kupanga nyimbo za chibu kuanzia kwa KAMWAMBIE mpaka NUMBER ONE,hakuna wimbo ambao Dogo kakosea....na uzuri zaidi unaona kuna maboresho ktk kila song from music to videos.
Binafsi wakati chibu anaanza nkaona hana muda mrefu baada ya mbagala.mara nkasikia ntarejea nkasema maybe ya mwisho mwisho,kustuka naskia MAWAZO(always my favourite) nkasema hatotoa tena kama mawazo,sijakaa sawa naskia lala salama mara kizai zai yaani mara kesho yaani mradi vurugu...mwenyewe nikakata tiketi ya ushabiki namba moja wa chibu.
So mm mtu akija na Sera zake za ufalme na reference akiwa alli binafsi namuona hayuko sawa.
We unasemaje wewe ? C unasema baada ya kuona Chibu anaanza ukajua hana muda mrefu?? Mi nikakumbuka ilikuwa hivi...!! Enzi hizo nilikuwa sijaacha kusoma magazeti ya Shigongo type! Sasa ilikuwa kila nikikutana na Shigongo type, nakutana na habari za mtu anayeitwa Diamond!!! Mimi nina tatizo moja... nina allergy na majina yanayovuta attention!!! Hata duka lako ukiliita SUPER kufanya nini cjui, kuna hatari nisiingie! Akili yangu inavyonituma ni kwamba u've some weaknesses ambazo unataka kuzi-cover up kwa jina tamu linalovutia huku likiwa limenyunyuziwa marashi! Kwahiyo Dogo ikawa nampotezea tu, kisa, jina la DIAMOND tu! Kama mara mbili tatu hivi nikakuta habari zake kwenye serious newspaper... nikampotezea vile vile... kisa kile kile, sikuwa na sababu za msingi... kwavile tu naona jina lake ni aina ya majina yanayovuta attention ambayo kwa tafsiri yangu ni udhaifu!
Wiki kadhaa baadae(siku chache kabla Mbagala haijakuwa released), hiyo cku nilirudi ghetto mapema! Nikiwa nimetulia nacheki EATV, mara akatokea dogo mmoja hivi ambae simfahamu! Binafsi nikiona mwanamuzi cmfahamu, nabadili channel instantly! Ile nagusa remote... naona jina DIAMOND... mi ehe, kumbe "mbwiga" mwenyewe ndo huyu! Kwa ubishi tu nikataka ku-change hivyo hivyo! Kabla cjafanya hivyo... nikavutiwa na beat ya nyimbo... nikakausha lakini kidole bado kikiwa kwenye remote tayari kwa kubadili channel sekunde yoyote akinizingua!!!
Sekunde chache baadae, dogo akaanza kuimba... mi, eh, kumbe dogo anajua! Nikataka ku-rewind chap chap, nikaona aiyaaa kumbe naangalia tv! Hili la kutaka ku-rewind watu wanaweza kudhani nanogesha lakini wenzangu waliokuwa addicted kwenye movie na series wanaweza kunielewa manake kv kwenye movie na series ni full mambo ya ku-rewind ili utamu uupate vizuri!!! Basi mazoea ya kucheza na remote kwenye series huwa tunayahamishia hadi kwenye tv programs!
Basi bwana, Nenda Kamwambie nikaisikiliza mwanzo hadi mwsiho... nikaona aaaanhaaa, kumbe ndo maana dogo kajiita Diamond ni kweli Diamond! Ikawa sasa nategeshea nimuone tena... ah wapi... sikupata tena hiyo bahati lakini siku chache baadae, nikamuona tena... mi aaaha, yule dogo si ndo huyu... kumbe ndo siku Mbagala inaoneshwa on TV stations kwa mara ya kwanza! Nikamkubali zaidi na zaidi... alipotowa Nitarejea, aaaaah... dogo ndo akamaliza kabisa! I short, simjui na hanijui... yeye anatoka Kigoma mimi natoka Lindi... mbali mbali, wala ukaribu hakuna lakini hata hivyo, kuna wakati nilikuwa nataka kumuunganisha kwenye mchongo fulani, unfortunately ukabuma... nikapiga kimya, lakini Inshallah, naamini ipo siku nitakuja kutoa mchango wangu wa aina yoyote kwake coz' chanda chema huvikwa pete! Na wala sipo Team Diamond... hayo ni mambo yenu nyie wa 1990's lakini penye ukweli lazima usemwe... dogo anajua, na more importantly, he's creative and hardworking than any musician in EA na ndo maana nashangazwa sana na mburullaz wanaosema kwamba Chibu ni mtu anayekwenda kwa kiki za kashfa lakini kila ninapowatwangwa maswali... hakuna anayejibu zaidi ya shouting! Yaani kwa makusudi wanashindwa kuona jitihada binafsi zinazofanywa na Chibu na ndio maana mie nawaita majirani wa Bwana Mcharo wanaokerwa na Bwana Mcharo kula nyama kila siku!!!
Duh! Nimeongea kweli kweli... utafikiri nipo jukwaa la siasa!!