Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

Ni msanii wa kimataifa anayevuma Afrika na hasa nchini mwake Tanzania !
... halafu, hivi wanaojaribu kumlinganisha na Ali Kiba huwa wana maana gani ?
 
KWA mara ya kwanza ndani ya Global TV Online ya Global Publishers, supastaa ndani na nje ya Bongo kutoka muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz' amewafungukia waliowahi kuwa wapenzi wake, Jokate Mwegelo ' Kidoti ' , Wema Sepetu ' Madam' na Penniel Mungilwa ' Penny ' kuwa waligoma kumzalia mtoto.

LIVE CHUMBA CHA HABARI

Akizungumza na Kipindi cha Live Chumba cha Habari kinachorushwa na runinga hiyo kilichofanyika kwenye ofisi za gazeti hili, Bamaga - Mwenge jijini Dar, Jumanne wiki hii, Diamond alisema hayo alipoulizwa na waandishi wetu kwamba amekuwa akitangaza kupenda watoto lakini kwa nini hana hata wa dawa licha ya kuwa na uhusiano na wanawake tofoutitofauti.

Diamond : " Ni kweli napenda watoto lakini siwezi kupata mtoto peke yangu bila mwenzangu. Lazima kuwe na mwenzangu ambaye tutakubaliana. " Nilichojifunza ni kwamba wenzangu hawakuwa real (hawakumaanisha ) hivyo wakawa wanachengachenga. " Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz' akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Penniel Mungilwa ' Penny '.

PENNY NI ZAIDI YA WOTE

Diamond alieleza kwamba, kati ya wanawake aliokuwa nao, Penny ambaye ni mtangazaji wa Radio E - FM ndiye msichana ambaye alikuwa wa kipekee kwani hakuwahi kumkera hata siku moja. "Nimeishi na Penny kwa muda mrefu. Kweli hakunikosea. Sema basi tu . "

MIMBA MBILI KWA PENNY

"Ukweli Penny ningezaa naye, aliwahi kuniambia ana mimba yangu, sikuamini, nikampeleka hospitali kupima ikawa kweli. Kesho yake niikamnunulia gari, nikamwambia mama tulia.

Siku mbili tatu akasema mimba imetoka. "Nikaja nikamjaza kingine cha pili ( mimba), nayo baada ya muda akaja kuniambia imetoka. Nikaona huyu mzinguaji, nikammwaga. Lakini iliniuma sana. "Kwa wengine (Jokate na Wema) walikuwa wakinichenga tu bila sababu, unamuona huyu hataki kubeba mimba yangu.

Mtu kwa mdomo anasema kwamba yuko na wewe kikamilifu lakini kwa matendo unaona siye. "Lakini kusema ukweli kabisa natamani sana kuwa na mtoto. "Hapo juzikati nilitaka kuoa, kila kitu kilikuwa sawa, nikaja kubadili mawazo. "

Swali : " Ulitaka kumuoa nani ?"Diamond : "Ah ! Siwezi kumsema hapa. "

WEMA ALITOA MIMBA YAKE? Alipoulizwa juu ya Wema kama aliwahi kutoa ujauzito wake, Diamond alijibu huku akiachia tabasamu la kiaina: " Siwezi kumsemea yeye labda mumuulize mwenyewe, najua mna mawasiliano mazuri. "
 

Attachments

  • 1419012538876.jpg
    1419012538876.jpg
    83.1 KB · Views: 1,706
Ni msanii wa kimataifa anayevuma Afrika na hasa nchini mwake Tanzania !
... halafu, hivi wanaojaribu kumlinganisha na Ali Kiba huwa wana maana gani ?

huwezi kuwalingalisha labda kama unamatatizo ya akili
 
Sometimes ustaa unakufanya unakuwa kama umepagawa..........................

Asa ndo alikuwa anabwabwaja nini!!!!
 
Saa zingine unaweza kuta kajijua mwenyewe hana uwezo wakuzaa so anatafuta pakujishika mapema na kama kweli ana mguu wa mtoto anadhani wanawake wake itakuwa rahisi kushika mimba! Ndo maana zinatoka ikiingia kabla ijashika vizur ye anachokonoa anadhani mimba itakaa lazima itoke. All in all nadhani dogo hajitambui kwa sasa kalewa sifa Ila ukisema unaitwa hater
 
Ni msanii wa kimataifa anayevuma Afrika na hasa nchini mwake Tanzania !
... halafu, hivi wanaojaribu kumlinganisha na Ali Kiba huwa wana maana gani ?

Mi mwenyewe huwa nashindwa kuelewa wana maana gani yani,maana ni suala ambalo lipo wazi kabisa kua dangote anajua
 
Back
Top Bottom