hyo ndo Chibu roho mbaya kwake mwiko
Unajua kuna vitu watu hawaelewi wanapiga tu makelele, hakuna kampeni watu watafanya itamshusha Diamond kama ni kushuka atashuka muda wake ukifika na sio leo hiyo.
Ngojea niwaambie kitu hao mbululaz, Diamond ana supporters wa kutosha hakuna mtaji mkubwa kwa mwanamziki kama supporters. Hao wanaowapiga makelele sio supporters wa yeyote ni wapiga kelele tu na haters ambao kwa sasa wamegeuka voters.
Bongo hii kuna mastaa wachache sana wenye supporters wa ukweli, watu wenye supporters ni Jide, Juma Nature, Sugu, alikuwa Kanumba na sasa ni Diamond. Awa watu wasikie tu kwa wasiwasi awa wana majeshi ya ukweli yenye true love kila angle ya nchi.
Leo mtu anakuja anataka kuwaaminisha watu eti yeye anauwezo wa kushusha watu na kampeni zake, ni uongo unaoonekana ni ukweli kwa wasio na uwezo wa kufikiria. Mtu kama Wema yeye ana followers sio supporters ambao kazi yao ni kupiga kelele kwenye mitandao na Kutukana watu baada ya hapo hakuna kinachoendelea. Kitu ambacho hatuwezi kukipinga ni kuwa Wema ana jeshi kubwa la wapiga kura za online kwa sasa sababu nature ya watu wa Wema ni watu ambao 24/7 wapo mitandaoni wanatukana watu so ni rahisi sana kwao kupiga kura.
Hapa ishu inakuja je Wema, joketi na kiba wana supporters? Je kwa nini project za Wema zina fail kama yeye ana nguvu kiasi hicho? Wema amezunguka Mwanza, Zanzibar na Dsm akifanya instagram party lakini tunajua alichokumbana nacho show zote ilikuwa ni aibu tupu watu hawakujitokeza na dsm ndio muandaaji alikula hasara akurudisha ata nusu ya gharama za kuandaa, alidanganyika na wapiga kelele wa Wema insta akachukua uwanja wa wazi akiamini patatapika. Wema ana show ya TV ambayo muda sio mrefu wadhamini wataikacha imekosa watu. Wema ametokea kwenye video ya Ommy Dimpoz iliyofanyika South Africa lakini haijamsaidia Dimpoz kufika popote video imeshasaaulika. Wema ni meneja wa msanii Mirror leo hii mirror pamoja na nyimbo zake nzuri ila nyota tunayoambiwa ya Wema haijamsaidia chochote. Mifano ni mingi ila najaribu kuwaonyesha tofauti ya supporters na mashabiki ambao siku hizi wanaitwa maandazi.
Tukija kwa Jokate au maarufu kama Kidoti ndio anaangaika tu na biashara zisizo fanikiwa mara nywele mara sendoz mara mikataba ya mabilion. Ila pamoja na hiyo nguvu wanayojifanya wanayo mbona haiwasaidii wao project zao. Tunarudi pale pale hawana supporters ila wana mashabiki haters wa daraja la juu ambao wao wanahama muda wowote kama bendera inavyofata upepo hawana love ya kweli ni haters haters haters leo watamtukana Zari kesho Penny keshokutwa Kajala mara Lulu mara Mange mara upepo ukikosa mwelekeo watarudi kwa Madame wao mara watamtukana Kidoti.
Sasa turudi kwenye ishu ya kupigia kura wasanii wa nje huku wakifikiri wanamkomesha msanii wa ndani, hii kampeni inayoratibiwa na Wema, Joketi, Ali kiba na Diva ni kielelezo cha watu walio confused na frustrated na maisha ambao wamepata mashabiki wanao fanana nao. Ila mwisho wa siku wao ndio watakuja kuluz anayebisha ahifadhi maneno yangu hapa kuna watu wataumbuka mchana kweupe muda sio mrefu.
Uwezi kupiga hatua kwa kupigiwa kelele, utasogea mbele kwa kazi nzuri tu. Fanya kazi nzuri kuwa tofauti waguse wabongo mbona utawapenda wabongo. Yani kiukweli hakuna watu wenye akili timamu kama wabongo, mbongo piga kelele zako fanya ujinga wako anakutazama tu ikifika kwenye support ndio utamuona rangi yake ya kweli. Chuki haiwezi kubalance mchezo ata siku moja watu wafanye kazi watz waamue, hamuwezi kubalance talents kwenye keyboard never.
Nimeona nitoe gazeti kabisa kuwaelewesha wanaoangaika na wanaosikitika na utoto unaoendelea.