Diamond Platinumz: Kwa nini nipo VEVO? Nasaha kwa wasanii

Diamond Platinumz: Kwa nini nipo VEVO? Nasaha kwa wasanii

Bravo chibu dangote,
Ameleta pia mapinduzi ya muziki Tz, kwamba music ni biashara.

Nadhani kupitia ww wenzako nao wataamka na kugundua sio ishu kua na ac ya vevo zaidi wananufaikaje na iyo brand.......
 
Na kuongezea tu VEVO hawalipi msanii binafsi ni lazima awe kwenye record lebo yenye shareholder kama universal , sonny au rock nation
Wasanii wa Tanzania ambao awako kwenye record lebo hawanuafaiki zaidi ya kuwa na status tu yupo VEVO.
Kuna siku mwaka Jana Flaviana Mtata aliuliza kwanin wasanii wa Tanzania wako VEVO wanajua haki zao? Wengi walimtukana ila nakumbuka wakazi alijitaidi kueleza kwaninn yeye hayupo VEVO,
 
Ishu siyo kuwa VEVO, ishu ni namna gani hao VEVO wanapromote kazi za msanii. Je ulishawahi kuona VEVO wamepost kazi za Vanessa, Alikiba au hata Rose Muhando? If hujui, hata Alikiba yupo VEVO, angalia kazi yake ya Aje remix. Alichoandika Diamond si kukuza mambo, bali kuwafumbua macho wasanii kwamba wasiingie mikataba kichwa kichwa bila kutathmini au kuhakisha hiyo mikataba inawafaidisha pande zote mbili.
Hao VEVO wamepost kazi ya diamond siku gani? ?una uhakika gani hao uliowataja nao hawatapostiwa na VEVO? ?
 
Hao VEVO wamepost kazi ya diamond siku gani? ?una uhakika gani hao uliowataja nao hawatapostiwa na VEVO? ?
Kwani a/c za VEVO so zipo wazi nenda basis kaangalie ujifunze mkuu
Nenda twitter, Facebook au instagram in vitu ambavyo viko wazi
 
Kwani a/c za VEVO so zipo wazi nenda basis kaangalie ujifunze mkuu
Nenda twitter, Facebook au instagram in vitu ambavyo viko wazi
Kwa hyo VEVO hawatapost video za akna alikiba na Vanessa siku zijazo? ?mi nataka kujua tu hata wewe unaweza njibu
 
We jamaa Inawezekana Sio Mzima
Ndio maana tunadai ndugu zetu walimu waongezewe maslahi imagine ndio una wanafunzi kama hawa 2 darasani
Yawezekana wengi tulikuwa tunajiuliza kwa nini Diamond Platinumz kauweka wimbo wake wa Marry You kwenye Youtube Channel mpya kabisa ya DiamondPlatnumzVEVO badala ile tuliyoizoea ambayo ipo verified ya Diamond Platnumz. Kupitia Instagram post, Diamond katolea maelezo na kutoa ushauri kwa wasanii wengine wanaotaka kujiunga na VEVO. Haya hapa chini ni maelezo yake.

“Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo... Nikawambia: "uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida.. Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo...na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo".....hivyo nikawambia: "siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida....

SABABU YA KUYASEMA HAYA:

Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa
Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu, vilevike umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae... nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao..." kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh... –SIMBA”

 
Kwa hyo VEVO hawatapost video za akna alikiba na Vanessa siku zijazo? ?mi nataka kujua tu hata wewe unaweza njibu
Diamond kajiunga juzi kwanin wanampost ? Ndo swali la msingi na Hawa waliojiunga kitambo kwanin hawakuwapost au hawajawapost hadi Leo ndo swali la msingi.
Tofauti hapo ndo point ya msingi
 
Diamond kajiunga juzi kwanin wanampost ? Ndo swali la msingi na Hawa waliojiunga kitambo kwanin hawakuwapost au hawajawapost hadi Leo ndo swali la msingi.
Tofauti hapo ndo point ya msingi
we jamaa kumuelewesha chizi utajipa kazi. Wanaelew ila hawataki tu kuelewa
 
mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya.
Umeelew kwa makini Alicho andika Diamond au ulivyo Ona neno Vevo mbio mbio ukamkumbuka Vanessa? Alikuwa anaweka Wimbo vevo Malipo ilikuaje? Soma post kwanza ndo ucomment au kisa ni Diamond kasema
 
Hiyo ni advert and am sure VEVO wamemlipa for that posting..or Barter Trade..I post you, you post me.But hiyo in typical scripted advert
 
mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya.
Kwasababu vanessa mdee alijunya na vevo lakini hakutoa taarifa stahili kama alivyofanya Diamonc binafsi nilikua sifahamu umuhimu wa kua Vevo na kua na akaunti ya youtube ya kawaida,,nilichofahamu ni kwamba ukiwa Vevo unalipwa pesa nyingi kwa mujibu alivyoandika Diamond sina uhakika...
 
Kwanini sasahivi? Jibu ni kwamba ukipitia a/c za VEVO za twitter na instagram utaona wanafanya Kazi ya kupromote wimbo wa marry you wa diamond ft neyo kote wamepost
Ndo maana diamond anakwambia kabla hajajiunga alitaka VEVO wenyewe watambue kina msanii wa Tanzania anaitwa diamond, hats kiwango cha pesa owe sawa na wasanii wa marekani per view,
Sasa sijui wewe hujaelewa wapi?
Tena kasema kila msanii ana mashabiki wake yeye hata akiwa nao wa 3 basi alipwe kwa view 3 sawa na wamarekani mwenye view millioni 3

Kwanza huu ushauri wa Diamond sio kwa sisi mashabiki ni kwa wasanii so wasanii ndo wakusema

Ila kwa vile kasema Diamond basi ni shida
 
Tatizo mnakimbilia kushangaa bila kuelewa kilichoandikwa.
Kaona watu hawana habari anaanza kujiongelesha mwenyew utadhani kaulizwa, nini Vevo ? Hata mbunguni akitaka aende,watu tupo busy na habari za mama wema na steve nyerere,hatutoi kiki
 
sina uhakika kama naropoka na nimerudia kusoma lakini bado nashangaa "mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya."
Mtu gani usiyeelewa? Sisi hatukatai vanessa kuwa Vevo tangu zamani?

Haya wewe unae jua kuwa vanesaa yupo vevo hadi sahizi kaingiza sh ngapi kupitia Vevo? Alikuwa analipwa sawa na Rihanna kwa view mmoja? Vevo wamewahi itangaza wimbo wake hata mmoja? Kuwa na akili acha kuropoka

Au kisa ushauri katoa Diamond
 
mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya.
Umesoma alichoandika au umetanguliza fitna tuu????
 
Back
Top Bottom