Diamond Platinumz vs Ali Kiba, nani mkali?

Diamond Platinumz vs Ali Kiba, nani mkali?

Media zinapromote bifu,wanadai wanakuza mziki

Wadau na wasanii wabovu, malizieni wenyewe.

Alisema Msukuma mmoja hivi.

Kuna watu wanamchukia diamond kisa wanampenda Kiba.

wanadhani hawawezi kuwapenda wote,kama mimi ninavyoweza.
#team mziki mzuri
 
ukianza kuhesabu wasanii, ali k mweke kwenye sifuri then ndo uanze, huyo ni disaster aisee!.
 
Kwani hawa ni wanamuziki au wasanii? Ni vema kufananisha wanamuziki wa kiukweli ila si hawa wanaopikiwa kila kitu na kuchujwa sauti zao studio.
 
Mkuu we ni mswahili mimi ni mswahili na waswahili sisi tunajuana...Hapa kinachoendelea ni akili pure za kiswahili,yaaani sio kwamba watu wanampenda saaaaana Kiba,hell no...watu wanaona Diamond sasa kapata mtu wa kumuadhibu...Ni kama dua zao za kumfunza adabu Diamond sasa zimesikika maana silaha ya kumuangamiza imeshapatikana.......Sasa uliza kosa haswa la Diamond ni lipi mpaka wanamchukia ivyo utaambiwa "anajifanya yupo juu" "anabebwa" "hana talent"......Kwetu uswahilini awa wapo kibao,jamaa unakuta anamchukia mtu mpaka unashangaa,sasa muulize kwa nini unamchukia kiasi hicho utaskia "anajifanya anajua kuvaa",yani ndio tulivyo waswazi.

Na hichi ndio kinatokea kwa Diamond watu wanakwambia hana lolote anabebwa,so wanachotaka haswa ili roho zao zifurahi zisuuzike ni arudi chini afanane na wasanii wenzie hapo ndio atakuwa kwao wa ukweli,simpo,mtu wa watu,hana makuu nk nk.....

Kosa kubwa kwa waswahili sisi including Kiba na team yake ni Diamond "anajifanya yupo juu" so inabidi ashuke
 
Kuna wimbo mmoja unaitwa Daraja la sarenda,ndo kaimba nani kati ya hao?.Basi ndo kula yangu achukue

AISEEH WE HAUPO KABISA....KWENYE DARAJA LA sarenda MAGARI MAWILI YAMEGONGANA MAMAA NDIPO NILIPATWA NA MSHITUKO USIOSEMEKANA MAA DAH WAPI MR.PAUL ZUWENA
 
Diamond Vs Ali Kiba ni ushindani
usio rasmi unaochochewa zaidi na
mashabiki wa muziki Tanzania kwa
kuwa wawili hao licha ya kuwa wote
ni wasanii wenye uwezo mkubwa
sana kwenye uimbaji wanatajwa
kuwa na tofauti au vita baridi.
Wapo wengi ambao wanauzungumzia
hata kama sio kwenye vyombo vya
habari na kuna wachache ambao
maoni yao yamefika kwenye vyombo
vya habari.
Vijimambo imezungumza na mmiliki
wa G Records, Guru Ramadhani aka
DJ G-Lover ambaye studio yake ndiyo
ilimtoa Ally Kiba na kumfikisha
kwenye mkondo mkubwa wa muziki
ametoa maoni yake kuhusu utofauti
anaouona kati ya wasanii hao.
Guru anaamini kuwa Ali Kiba ana
hazina kubwa ya sauti na
anakumbuka kuwa Diamond aliwahi
kuisifia.
“Kwa kweli tofauti ukija kwenye
masuala uimbaji, wengi wanaongelea
hata katika mitandao tofauti tofauti
kwamba Ali ana sauti nzuri na
anaimba vizuri. Hata Diamond kuna
wakati alikuwa anakiri kwamba
angekuwa ana sauti kama ya Alikiba
basi angefanya mambo makubwa
zaidi.” Amesema G-Lover.
Kwa mujibu wa G-Lover, wakati Ally
Kiba yuko juu kupitia studio yake
alikuwa na team ya watu
wasiopungua thelathini, kitu
ambacho Diamond anakifanya sasa
hivi.
“Lakini unapokuja kibiashara
Diamond huwa anazungumza kuwa
yeye muziki wake anaufanya
kibiashara na ndo maana ana team
work kubwa ambayo inamsaidia yeye
kujua ni kitu gani anatakiwa kufanya,
kuna kitu gani anatakiwa kukifanya
kwa upande wa muziki. Sasa kwa
upande wa Ali kwa sasa hivi, kwa
kipindi niko naye nilikuwa na team
ambayo hata yeye alikuwa hajui
mimi nipo na akina nani nyuma
yangu. Alikuwa anajua kuwa yupo G,
lakini nyuma yangu nilikuwa na watu
takriban thelathini ambao ni team
work ambayo ilikuwa inafanya kazi
kwa Ali Kiba kujua ni kitu gani na
kitu gani tunatakiwa tufanye ili afike
na mpaka akafika hapo. Ameeleza.
“Diamond naye anafanya vitu kama
hivyo, unaweza kuona Diamond ana
team ya watu watatu tu au wanne
ambao wanamsaidia, kwahiyo utaona
Diamond kuna watu kibao ambao
amewapa ajira. Kwahiyo Diamond
hawezi kuwaangusha watu ambao
wapo nyuma yake ambao wamepata
ajira kutoka kwake. Kwa mfano kuna
utofauti mkubwa ambao Diamond
amekuja nao ambao ukiangalia ni
utaratibu uleule ambao nilikuwa
nikiufanya kwa Ali. Kwahiyo sijui
kuna utofauti gani kati ya
management ya Diamond na ya Ally
Kiba ya sasa hivi.”

Timesfm.com
 
Napenda nyimbo za zamani za Ally Kiba.
Napenda nyimbo za sasa za Diamond.

Mi nawapa haki sawa wote 9/10.

True say, Ali K ananivutia kwenye Usiniseme,Dushelele na ile aliyoimba na mdogo wake Abdul-Kidela....na Almasi namkubali kwenye,Mbagala, Kamwambie, Lala Salama, Kizaizai na My number one.....zilizobaki kwao wote naziona za kawaida tu....(kwa mtazamo wangu)
 
Hivi Unafikiri hawa watu wangekaa pamoja wakaacha hizo tofauti zilizopo kati yao n then wakatoa Single ya pamoja si ingekuwa poa sana?

na je unafikiri aina gani ya ngoma ambayo ingekaa poa sana? Ya Mapenzi, Ya Kisiasa, Au Kuelimisha Jamii?

Mi nahisi ni wakati wenu ali NA diamond kumaliza tofauti zenu sasa
 
Last edited by a moderator:
Hivi Unafikiri hawa watu wangekaa pamoja wakaacha hizo tofauti zilizopo kati yao n then wakatoa Single ya pamoja si ingekuwa poa sana?

na je unafikiri aina gani ya ngoma ambayo ingekaa poa sana? Ya Mapenzi, Ya Kisiasa, Au Kuelimisha Jamii?

Mi nahisi ni wakati wenu ali NA diamond kumaliza tofauti zenu sasa

Tofauti zao ndio tija kwa muziki wa Tanzania! Ili mradi wasipigane tu.
 
Tofauti zao ndio tija kwa muziki wa Tanzania! Ili mradi wasipigane tu.

Ni kweli, lakin wangejaribu kutoa single moja tu ili watanzania wajivunie kwamba ipo collabo iliyofanywa na Top Artist wa Tanzania, Mbona tunaona collabo za wenzetu P Square Ft Davido Na Wengine wengi.
 
Wasalaam

Messi na ronaldo ni majina makubwa kwenye ulimwengu wa soka katika mlongo huu kila mmoja akiiwa na rekodi za kutosha. ....sitaki kwenda ndani zaidi.

Katika sanaa ya muziki wa bongo fleva majina ya Diamond na Ally Kiba nayo yanachukua vichwa vya habari katika media mbalimbali . Hawa jamaa nao kila moja anarekodi zake na ladha yake.

Ronaldo na messi ni wachezaji bora wa dunia katika kipindi tajwa vivyo hivyo kwa diamond na kiba katika bongo fleva. Kwa kutumia taswira ya wachezaji hao Leo nataka tujadiliane kati ya diamond na kiba nani ni au nani anafuata principles au nyendo za mchezaji mmojawapo. Karibuni
 
Ally Kiba hayupo level za diamond, wacha kumpa jina la bure. Tafuta wa level za diamond ndo uanze kuwalinganisha.
 
Back
Top Bottom