Deo Corleone
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 17,006
- 13,281
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu we ni mswahili mimi ni mswahili na waswahili sisi tunajuana...Hapa kinachoendelea ni akili pure za kiswahili,yaaani sio kwamba watu wanampenda saaaaana Kiba,hell no...watu wanaona Diamond sasa kapata mtu wa kumuadhibu...Ni kama dua zao za kumfunza adabu Diamond sasa zimesikika maana silaha ya kumuangamiza imeshapatikana.......Sasa uliza kosa haswa la Diamond ni lipi mpaka wanamchukia ivyo utaambiwa "anajifanya yupo juu" "anabebwa" "hana talent"......Kwetu uswahilini awa wapo kibao,jamaa unakuta anamchukia mtu mpaka unashangaa,sasa muulize kwa nini unamchukia kiasi hicho utaskia "anajifanya anajua kuvaa",yani ndio tulivyo waswazi.
Na hichi ndio kinatokea kwa Diamond watu wanakwambia hana lolote anabebwa,so wanachotaka haswa ili roho zao zifurahi zisuuzike ni arudi chini afanane na wasanii wenzie hapo ndio atakuwa kwao wa ukweli,simpo,mtu wa watu,hana makuu nk nk.....
Kosa kubwa kwa waswahili sisi including Kiba na team yake ni Diamond "anajifanya yupo juu" so inabidi ashuke
Kuna wimbo mmoja unaitwa Daraja la sarenda,ndo kaimba nani kati ya hao?.Basi ndo kula yangu achukue
Napenda nyimbo za zamani za Ally Kiba.
Napenda nyimbo za sasa za Diamond.
Mi nawapa haki sawa wote 9/10.
Hivi Unafikiri hawa watu wangekaa pamoja wakaacha hizo tofauti zilizopo kati yao n then wakatoa Single ya pamoja si ingekuwa poa sana?
na je unafikiri aina gani ya ngoma ambayo ingekaa poa sana? Ya Mapenzi, Ya Kisiasa, Au Kuelimisha Jamii?
Mi nahisi ni wakati wenu ali NA diamond kumaliza tofauti zenu sasa
Tofauti zao ndio tija kwa muziki wa Tanzania! Ili mradi wasipigane tu.