Diamond Platnumz adaiwa kodi Sh. Milioni 400 na TRA

Kinacho mponza Diamond ni sifa.

Ana piga hela ndogo tu za show na za Magumashi na za wafadhili wake wa...ung..afu anajisifu balaa. Mara choo tu 70m...
Nimenunua mjengo South 1Billion.

Mara Ooh na studio ya 300m.
Juzi tu kachambwa na Gwajima kaenda kukodi sijui Hummer. Oooh nimenunu hii ndinga kupigia misele nikiwa South.

Sasa pambana na wazee wa Number...JPM hataniii na utalipa tu...si ulikuwa unanyonga viono kwenye jukwaa la CCM ...ISOME NAMBA..
 
Bro ukiona mtu anadaiwa kodi kubwa ujue basi hata anachoinguza pia ni kikubwaa Iyo inakaribiia half bilion so unahisi atakuwa anaingiza sh Ngapi ?
 
Ali Kiba anadaiwa zaidi ya hizo lakini hapendi show off za kuandikwa magazetini
 
kulipa kodi ni kielelezo cha uzalendo!!
kila mzalendo kwa nchi yake hawezi kukwepa kodi!!

watanzania wenzagu tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi yetu!!!

awamu hii tunaona matunda ya kodi zetu!!!

tulipe kodi bila kinyongo!!
 
Kama wale masikini waandishi wa Uhuru publication waliokuwa WANADAI mishahara miezi 7 mpaka wananyimwa unyumba home, kweli ccm ilipaswa kujua dawa ya deni kulipa sio kusubiri mpaka Sizonje aje atoe amri ya kulipa.

Waliuza mashine ya kuprint kama chuma chakavu ili wapate hela ya mishahara
 
Halali yake kulipa hiyo kodi maana kama mtu ananunua cheni ya milioni 100 na saa ,heleni bangili kama vya milioni 200 inaonyesha kipato chake kikubwa na alipe tu.

Ila sometimes umaarufu na kujitangaza tangaza kuna ponza , angejikalia kimya hao TRA wasingemfata
 
Agizo la kila mtu alipe kodi ni la mkuu na linamuhusu kila mwananchi, kama TRA walikadiria hiyo na alipe tu kama ameona kaonewa awasiliane na TRA ili wafanye uhakiki na alipe ile inayo muhusu, mbona sie tunalipa na wala hatuna vipato vikubwa kama yeye?!
 
Maybe haujaelewa vizuri, nimesema mazingira ya kazi za wasanii hayajakaa poa. Pirates za kazi za wasanii zimezidi mtaani blogs ambazo zinavujisha kazi za wasanii tena kwa uwazi ni nyingi na hazichukuliwi hatua, hakuna msanii anayelipwa mirahaba kwa kupiga kazi zake kwenye vituo vya radio, sasa unamkadiliaje flani kaingiza kiasi gani wakati njia ambazo zipo legally za kuingizia pesa zake hauzisimamii?
 
Na mimi hujanielewa ndio maana nimesema awasiliane na TRA ili ajue hiyo kodi anayotakiwa kulipwa imepatiakana vipi? Kulalamika bila kuchukua hatua ya kujua sababu haita msaidia, lakini vilevile tujue Diamond ana mikataba na makampuni mengi tu na hayo makampuni yanawasilisha malipo yao TRA hivyo inawarahisishia wao TRA kujua kipato cha muhusiaka, maana kwenye kodi zao huweka wazi malipo yote waliyolipa na manunuzi waliyofanya ndio maana mfanyabiashara ukipewa risiti ya VAT lazima TRA watajua uliuza na ulinunua kwa nani return zinaonesha tu.
 

Acha kulialia Diamond analipwa na Vidacom, DSTV,Cocacola, GSM, , anauza nyimbo wasafi dotcom, anauza perfume moja tu 105,000 , anamiliki nyumba kadhaa bongo na south africa, magari kadhaa, show kadhaa anafanya ndani na nje ya nchi...

Hiyo kodi ni ndogo sana kwa kipato cha diamond.

Kuhusu kutengenezewa mazingira sijui sio tija maana huku mtaani kibanda cha duka unapigwa mikodi kibaooo mara fire, mara kuzoa taka, mara Osha, n.k

Hapo bado hujaja kwa wafanyakazi kodi wanayokatwa utaliaaaa bora huyo Diamond anachezea hata hela kununua cheni ya milioni 100
 
Dawa ya deni ni kulipa na kama hajaridhika anatakiwa kwenda TRA kupata maelezo zaidi kuhusu hilo deni na kukubaliana jinsi ya kulipa.
Swala la kodi halina mjadala maana mfano wafanyakazi wa serikali wanalipa kwa 100% sasa imagine wengine wote wangeweza kulipa 70% tu tungekuwa mbali sana.
Kwa hiyo bado naisisitiza serikali kutafuta njia mbadala ya kumbana kila mtu aweze kulipa kodi halali maana mashine za EFD tayari zimekwa.
 
Bosi! Weka jaribu kuongea kwa mantiki basi, haujui tija ya kuweka mazingira ya mziki kwenye masuala ya finance, its true inawezekana diamond anaingiza kipato kikubwa kuliko hiyo kodi na ni hasara ya kutokufanya kama nilivyoshauri juu, kuna pesa ambayo inapotea kutokana na hizo pirates za kazi za wasanii, mbona serikali isipoweka mazingira mazuri kwa uwekezaji mnalalamika? Kuna tatizo gani kwenye hiyo post?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…