Diamond Platnumz adaiwa kodi Sh. Milioni 400 na TRA

Kama hakujipanga kwa hili toka mwanzoni, atapigwa vibaya sana.

Awe na Financial Advicer wa kumuambia jinsi gani ya kumanage pesa zake.
Tatizo letu waswahili ni.kutojua yapi ni mapato na yapi ni matumizi. Kwa mfano mtu wa kodi akikuuliza kama ulipata faida yoyote kwa mwaka. Utajibu hukupata wakati huo huo utamweleza jinsi maisha yalivyo taiti maana mwaka huo imepeleka waroro 4 int school, mdogo wako akaoa ukatoa 5, kwa sababu ulichamganyikiwa ukaenda kupumzika na familia dubai, ukazidi kulalamika kuwa mwaka ulikuwa mgumu maidi maana hata ulipomwagizia mke gari tra walikutoza kodi kubwa. Kwa hiyo kwa kweli mwaka ulikuwa mgumu kwa hiyo hukupata faida yoyote. Kumbe unajikaanga mwenyewe kwa ofisa wa kodi. Utakapokupigia kodi unalia.
 
Huwa wanaona raha kuongeza sifuri sifuri mbele ya wanachokipata.. Majuzi hapa alisema hapigi show ya chini ya Million 100 hapa Tz, pia ana deals za Billions sijui Vodacom mara Tomato Sauce.. Sasa kwa mchanganuo huo kwanini analia lia kutoa hiyo Million 400?? Si kwa mwaka anapiga zaidi ya show 20 hapa ndani ya nchi? Hiyo tayari ni Billion 2 kama kweli alidai analipwa Million 100 kwa show..

Na kuna yule mwingine juzi alisema analipwa Dola 3500 kila mwezi kutoka YouTube, nae ajiandae asije kuanza kulia lia kama boss wake.

BTW hapa ni kazi tu na kampeni mlipiga wenyewe.. Kaziiii tu
 
Hata hayo anayosema yakifanyika hatoendelea kulipa hiyo million 400 bali kodi itaongezeka zaidi. Yeye anadhani kodi ni fixed? Kimsingi kama alikuwa analipwa Million 100 lakini hapo kuna mikono ya watu wengi na yeye anabaki na kiduchu basi ajiandae tu kulia..

Voda alisign deal ya pesa ndefu sana lakini kuna staffs wa voda waliongeza pesa zao humo ndani. Kwahiyo unaweza kuta deal alisign million 500 lakini yeye aliambulia 200 tu na hiyo 300 wakala wajanja. Hapo TRA hawajui hilo calculations zinapigwa za Million 500.. Kama show unasema unalipwa Million 100 lakini ndani ya hiyo 100 kuna pesa ya Tale, Fella na Ruge wao hilo hawajui watapiga 100 yote ni yako..

Ushauri wangu kwa Diamond ni wakati sasa wa yeye kuajiri kijana mwenye degree ya Account/Finance amlipe mshahara mzuri awe ndiye mshauri wake mkuu wa masuala ya kifedha na negotiations zote za madili ya kifedha afanye yeye na hao akina Tale wabaki tu kama mameneja au marafiki wa kawaida. Huwezi ukawa unalipa kodi mpaka kufikia hiyo million 400 wakati mshauri wako wa kifedha ni darasa la saba na anaishi mjini kiujanja ujanja tu..
 
Wananchi wepi labda!
 
Kwa hesabu hiyo hata ingekua chama gani kingemtoza kodi tu, vp mwalimu anayelipwa pesa kiduchu na analipa kodi kubwa! Wakisikia 400m akili zinaruka.
 
400m kwa mwaka mmoja??? Kwa muziki wake2 huu huu au na biashara zingine??
 
Kwani sisi tunaolipa kodi kila siku tuna mazingira mazuri yapi mkuu!?
 
Tatizo unakuja kishabiki sana, tuliza akili unaweza kuelewa, nimesema serikali kama inahitaji kodi ya wasanii basi iweke mazingira mazuri ili wapate hiyo kodi, sasa kama diamond anaingiza kiasi kikubwa zaidi ya kodi anayolipa kwako wewe hauoni tatizo? Hivi mpaka sasa tupo katika zama za kukadiliana kodi? Sasa je kwa msaga sumu na man fongo ambaye hauwezi kumkadilia kipato chake kwa kupitia instagram, unapata wapi kodi yake? Tahadhari; usichangie huku kichwani unamfikilia sana diamond, jaribu kuchangia kwa kufikilia mapato wanayopoteza wasanii na kodi ya serikali kwa kuto ku regulate kazi zao.
 
Kwani sisi tunaolipa kodi kila siku tuna mazingira mazuri yapi mkuu!?
Haujaeleza ni kodi gani unayolipa! Anzia hapo kwanza, kama ni mfanya kazi inajulikana unalipwa sh ngapi na unakatwa % ngapi, kama ni mfanya biashara ndio maan kuna EFD Machines nad the likes. Sasa niambie man fongo au sholo mwamba inatakiwa alipe tsh ngapi? Kumbuka anaingiza kipato!
 
Upande wa wananchi ni upi ?

- Wanasiasa wote porojo na lao ni moja ukitumika CCM basi UKAWA wanaona wivu wanataka wakutumie wao, Ujinga mtupu
 
Any Income earned in lieu of Employment, business or investment MUST be taxed!!
Wafanyakazi kwa muda mrefu wamekuwa wao tu ndio wafadhili wa Budget ya Nchi kupitia PAYE na VAT ktk matumizi yao.
Huyu huyu mfanyakazi alikipwa Lump sum amount kama Gratuity (Malipo kila baada ya mkataba) hukatwa karibu 30% ya kipato kile. Weka pembeni PAYE ya 30% kila mwezi.
Hivyo huu ni muda muafaka wa ku spread the Burden of TAX to other tax payers kama wasanii (Diamond), na ma MC (Kibonde/Pilipili/Kipanya).
Hivyo Diamond asilalamike alipe kodi kwa kila kipato chake cha Show, Matangazo yake, kodi itokanayo na malipo yatonayo na kipato kitokanacho na studio yake (yy pamoja na wasanii wengine kurecord muziki WCB studio) na CHIBU Perfume yake.
 
Kwa hesabu hiyo hata ingekua chama gani kingemtoza kodi tu, vp mwalimu anayelipwa pesa kiduchu na analipa kodi kubwa! Wakisikia 400m akili zinaruka.
Sasa mpaka hapo wewe hauoni hadara inayopatikana kwa kutosimamia vizuri mapato ya wasanii? Mwalimu anajulikana kipato chake na anajua ni asilimia ngapi analipa kodi, same time serikali haitojua kipato cha darasa unless a show off kwenye mtandao,
 
Yaani huyo diamond alipe hatamarakumi yahizo 1 laanayababayake 2 rafikiya bashite 3 kada waccm aisome namba kiritimba mkubwahuyo shyzzzz
 

Watu wengi mnakomenti
Kwa hisia bado, hata comment ya diamond imejieleza hapo, serikali haijaweka mazingira rafiki kwenye sanaa na wanahitaji kodi kwa kuwakadilia, na inawezekana diamond akalipa kodi ndogo kwa sababu ninaamini serikali haina tasrifa ya mapato katika sana kama ilizonazo kwenye hizo paye zenu, kama ingeweka mfumo mzuri isingeishia kwenye taarabu tu ingefika mpaka kwa kina hadija kopa na kina msaga sumu, lazima serikali iweke mfumo huru na rafiki kwa walipa kodi ikiwemo wasanii, leo msanii anayelipa kodi tanzania anaonekana diamond kwa sababu ameamua kufanya biashara in legally way, lakini ni wasanii wangapi wana lebal na brands?
 
Upande wa wananchi ni upi ?

- Wanasiasa wote porojo na lao ni moja ukitumika CCM basi UKAWA wanaona wivu wanataka wakutumie wao, Ujinga mtupu

Ndio siasa hizo kuna upande unamuona ney wa miteho shuujaa kuna mwingine unanona kapotea,

Upande mwingine unaona diamond kachagua upande sahii mwingine unaona anajipendekeza na kasaliti wananchi.

Wengine yetu macho tu.
 
Ndio siasa hizo kuna upande unamuona ney wa miteho shuujaa kuna mwingine unanona kapotea,

Upande mwingine unaona diamond kachagua upande sahii mwingine unaona anajipendekeza na kasaliti wananchi.

Wengine yetu macho tu.
Na huo ndio ukweli, ni bora tukaheshimu kila mtu atumike anakoona kuna afadhali kwake
 
Huyo Man Fungo simjui ila Diamond nilimwona akiwa ameweka picha akiwa ofisi za TRA na Kayombo Director wa elimu kwa mlipa kodi wa TRA pale HQ.. Na siku hiyo hiyo alipewa EFD Machine yake.. Sasa EFD inasema anadaiwa kodi ya Million 400.. Inatakiwa alipe hakuna namna..

Tatizo la wasanii wetu ni ujinga wao wenyewe.. Na hili si ajabu sababu hata miaka ya nyuma kidogo wasanii wengi wa Marekani walikuwa wana hizi scandal za kukwepa kodi and money laundering. Unaweza kuta anasema mimi show nalipwa million 100 lakini kati ya hizo 80 ni chafu na zinasafishwa kupitia hizo show na vitu kama hivyo na zikishasafishwa zinapelekwa kwa wenyewe.. Let's assume this, Tale anafanya biashara ya dawa kwahiyo ili aweze kusafisha fedha zake basi wanatengeneza hizo show za ukweli na uongo na matour ya ukweli na uongo na kujilipa mapesa mengi kupitia huyo Diamond alafu lastly unakuta figure za TRA zinasema labda Diamond ameingiza Bilion ndani ya miezi miwili au mitatu lakini kwa uhalisia kaingiza fedha chache sana kuliko hizo.

Mimi msingi wa hoja yangu wala si hicho ambacho umekisema, msingi ni kwanini aone Million 400 nyingi sana wakati huwa anatamba kuingiza billions? Alafu huu upumbavu wenu wa mtu aliye against na mawazo fulani basi ana chuki na huyo mtu sijui mnaotolea wapi. Mtu akisema sijapenda hiki cha Diamond basi eti una chuki nae.. Mimi siwezi kuwa na chuki na mtu ambaye wala hanijui na wala mimi si shabiki wa huyo Diamond wala mahasimu wake.. Mimi ni die hard sports fan, sina mahaba sana na muziki zaidi ya nikiwa bored naingia Youtube kuangalia kazi zao, huwa mara nyingi huwezi kukuta miziki kwenye device zangu, kwasasa nina videos tatu tu moja ya Davido na nyingine ya Wizkid na French Montana ile ameimba Uganda. Kwa kifupi ni sawa sawa na wewe si shabiki kabisa wa mpira alafu eti uambiwe unamchukia Kichuya au Ngassa.. Lazima hata wewe mwenyewe ushangae..
 
Wote wanapaswa walipe kodi siyo Diamond tu!! Hata Shilole au Harmorapa!! Hata mm hapa nalipa PAYE na kodi ya Gratuity! Achilia mbali VAT kila siku nalipa.
Kwani serikali imeniwekea mazingira yapi ya kulipa kodi mm au ya kazi yangu?

Kwani yy akilipa kama mm kuna shida?
 
Mb Mbona hawakomai kwenye madini kudai kodi
 
Si huwa anajisifia kuwa yeye ni msanii pekee Anaelipa Kodi? Sasa analialia nin?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…