kwanza if we talk about social media, over 90% ya mitandao ya kijamii inayotumika Tanzania, sio iliyoandikishwa Tanzania. Serikali na TCRA pamoja na mabavu yao, lakini kuna maeneo mengine makucha yao hayafiki labda kama kinachosemwa kina hatarisha maisha wa wananchi, uhai wa nchi au uhalali wa serikali iliyo madarakani.
tukija kwenye kazi za kisanii zinazo porwa mitandaoni, kama nilivyo sema awali, most of blogs, sites, and online portal are register out of Tanzania, and the servers in use are also located outside the country. Ukianzia kwenye mitandao inayotumika sana Tanzania, Blogger, Youtube, Istagram, sound-cloud, Audiomack etc etc yote hii inatumika kubadilishana kazi za wasanii bure na ni vigumu kwa TCRA kuifunga labda kama TCRA ina taarifa kama account fulani inamilikiwa na mtu fulani, tena huyo mtu awe anaishi Tanzania. MaDJ wengi Tanzania wao ndio wa kwanza kusambaza kazi za wasanii kwenye mitandao ya kijamii, bila hata kuwalipa fidia wasanii au kuomba idhini ya msanii. Sijaona mtu au kikundi chochote kilicho wahi kuoji kwanini maDj wanafanya hivyo huku wakijuwa kama ni kinyume na sheria. Hata hao wanamuziki wenyewe, hawajawa hoji au kuwashitaki maDj kwa kuweka kazi zao mitandaoni bila idhini yao?
Lazima tukubaliane kuwa muziki au sanaa ni pesa, na itahitajika "pesa kulinda pesa". Wenzetu hasa wa nchi zilizo enelea ni mara chache sana utakuta mwanamziki au msanini wa tasia yoyote ile anafanya kazi zote mwenyewe, nikimaanisha kufanya kazi ya usanii na kufanya kazi ya kulinda sanaa yake. Most of time they use art managements companies to control the flow of there work. Mwanamuziki anajiunga na music label au film agency ambayo ina uwezo kifedha kuwenza kumfikisha yoyote mahakamani kudai fidia kama itabainika kuwa amevujisha kazi ya msanii wao. Wewe kama msanii unabaki kufanya kazi yako ya kisanii tuu ladba mara moja-moja una chat na accountant kuona mambo ya kifedha yanakwendaje. Wasanii wanatakiwa kujuwa usanii sio kazi ya pesa ndogo, itahitajika pesa kubwa ili kutengeneza pesa kubwa zaidi. Cha msingi ni wao kutafuta wafadhili wa ukweli na kujijenga from there. Lakini tukikimbilia vya rahisi kusema oh....serikali, mara TCRA mtakuwa mnajidanganya with no clear end.