Diamond Platnumz adaiwa kodi Sh. Milioni 400 na TRA

Inajulikana unaingiza kiasi gani na unalipa asilimia ngapi, kuna mdau kasema kwa kipato anachoingiza diamond hiyo mil400 ni ndogo, kwako hauoni tatizo? Sasa huyo harmorapa umemuwekea mazingira gani ya kuregulate kipato anachoingiza ili ukate kodi yako? Ndio wakina msaga sumu inatakiwa walipe kodi kwa kile wanacholipwa, je kwa calculation zipi? Yaani mpaka uzi umefika page ya pili mnashindwa kunielewesha kwa hili.
 
Atalipa tu hilo deni, huyu kaka namhisi ana hela sana japo simtunzii mimi, kama aliweza kuchonga yale maneno ya ugoro kwa milioni 11 hawezi kushindwa kulipa hio 400m
 
Kwani wamekwambia alikuwa halipi? Ina wezekana hizo ndizo alikuwa amekwepa kwa kuficha mikataba.

Diamond hadi sasa analipa Kodi ila alikuwa anakwepa zingine. Nakumbuka kuna post aliweka kuwa hulipa Tshs 30M. Sasa sijui per month or p.a? ACACIA waliambiwa walipe kama 8Billion , ile siyo kodi yao bali waliyo kuwa wamedanyanya au kukwepa.

Kwa TRA hii ni issue ya kawaida tu. Yy alipe.
 

Naweza kuwa kweli sijakuelewa, na bahati mbaya bado haunielewi.

Suala la kutakatisha pesa ni jinai, na kwa bahati nzuri ume assume, still unatumia hisia zako ku judge issues, yaani TRA waongeze kodi kwa mtu kufanya jinai? Seriously! Huyo tale angekuwa uraiani anafanya nini? Nimekwambia serikali iweke mfumo ambao unawezesha hata kina man fongo walipe hizo kodi, sio kuchungulia instagram na ku assumes kodi kiasi gani! Nyinyi wenyewe mmesama kiasi hicho mil400 ni ndogo ukilinganisha na mapato yake, sasa wewe haini tatizo? Kwa hiyo unaona sawa kukadilia?

Nimeandika maoni yangu mwisho wa post kuwa serikali inatakiwa kuweka mazingira mazuri kwenye sanaa kama inahitaji kodi ya msanii. Watu wanakuja mala ooh! Ana nyumba south, ana label sijui kanunua cheni mil100 and the likes. Wasanii wana overrate kila kitu walichonacho ili kuongeza thamani yake, dunia nzima ipo hivyo. Wasanii hawajui hata idadi ya watu wanaotumia caller tunes zao, yaani wanaambiwa tu na makampuni kuwa una wateja wangapi!

Ukweli ni kwamba yakisimamiwa vizuri maslahi ya wasanii basi kodi italipwa hadi na kina young dee na kina young killer, ila kwa kumvizia tu msanii na kumkadilia basi tutakuwa tunapata hizo mil500 kwa mwaka mzima
 

Nimesema tunahitaji mfumo ambao utamfanya hadi young killer kulipa kodi, usiweke masiko pamba. Refer post hapo juu kabla ya ku comment. Ni Tanzania tu ndio unakutana balabalani ni gari la PA la airtel linapiga nyimbo ya msanii kwenye promotion yao bila kumlipa msanii, sheria hizi ndio zingefanya kujua mapato halisi ya msanii na kuweka % ya kodi,

Digital platform hakuna sheria na kama ipo aitiliwi mkazo watu wana account youtubes na blogs wanasambaza kazi za wasanii na wanagenerate traffic na wanaingiza pesa.

Sasa serikali inaangaika na diamond tu
Kwa sababu kaamua kuweka biashara ya mziki wazi! Narudia tena je, Man fongo na msaga sumu wanashiliki vipi kulipa kodi kutokana na faida ya mziki wao?
 

Mdau unaonekana kumuonea Huruma Sana CHIBU kutokana na mazingira magumu ya kufanya kazi.. SAWA,
Vp na siye wa kkoo tunaolipa kodi kabla ya Hata kufungua Biashara na baada ya kufungua Biashara wamachinga kufungua biashara Kama yako mbele ya duka lako na kodi hawa kipi..?
 

kwanza if we talk about social media, over 90% ya mitandao ya kijamii inayotumika Tanzania, sio iliyoandikishwa Tanzania. Serikali na TCRA pamoja na mabavu yao, lakini kuna maeneo mengine makucha yao hayafiki labda kama kinachosemwa kina hatarisha maisha wa wananchi, uhai wa nchi au uhalali wa serikali iliyo madarakani.

tukija kwenye kazi za kisanii zinazo porwa mitandaoni, kama nilivyo sema awali, most of blogs, sites, and online portal are register out of Tanzania, and the servers in use are also located outside the country. Ukianzia kwenye mitandao inayotumika sana Tanzania, Blogger, Youtube, Istagram, sound-cloud, Audiomack etc etc yote hii inatumika kubadilishana kazi za wasanii bure na ni vigumu kwa TCRA kuifunga labda kama TCRA ina taarifa kama account fulani inamilikiwa na mtu fulani, tena huyo mtu awe anaishi Tanzania. MaDJ wengi Tanzania wao ndio wa kwanza kusambaza kazi za wasanii kwenye mitandao ya kijamii, bila hata kuwalipa fidia wasanii au kuomba idhini ya msanii. Sijaona mtu au kikundi chochote kilicho wahi kuoji kwanini maDj wanafanya hivyo huku wakijuwa kama ni kinyume na sheria. Hata hao wanamuziki wenyewe, hawajawa hoji au kuwashitaki maDj kwa kuweka kazi zao mitandaoni bila idhini yao?

Lazima tukubaliane kuwa muziki au sanaa ni pesa, na itahitajika "pesa kulinda pesa". Wenzetu hasa wa nchi zilizo enelea ni mara chache sana utakuta mwanamziki au msanini wa tasia yoyote ile anafanya kazi zote mwenyewe, nikimaanisha kufanya kazi ya usanii na kufanya kazi ya kulinda sanaa yake. Most of time they use art managements companies to control the flow of there work. Mwanamuziki anajiunga na music label au film agency ambayo ina uwezo kifedha kuwenza kumfikisha yoyote mahakamani kudai fidia kama itabainika kuwa amevujisha kazi ya msanii wao. Wewe kama msanii unabaki kufanya kazi yako ya kisanii tuu ladba mara moja-moja una chat na accountant kuona mambo ya kifedha yanakwendaje. Wasanii wanatakiwa kujuwa usanii sio kazi ya pesa ndogo, itahitajika pesa kubwa ili kutengeneza pesa kubwa zaidi. Cha msingi ni wao kutafuta wafadhili wa ukweli na kujijenga from there. Lakini tukikimbilia vya rahisi kusema oh....serikali, mara TCRA mtakuwa mnajidanganya with no clear end.
 

Serekali haijaweka mazingira Rafiki kwa watu wote na sio Diamond pekee.. hv unajua mtu mwenye Kigoli cha kawaida kabisa kkoo analipa kodi ya shilling ngapi kwa mwaka... MILLIONI 3 hiyo ni TRA.. manispaa laki moja na nusu achilia upuuzi mwengine wa city..

Hv unajua wale machinga wanalipa shilling ngapi kwa Mwaka 0 na wanauza vitu vile vile tulivyoweka katika vigoli vyeti
 
Umevamia thread haujui mantiki yake, sasa wewe mwenye duka umelipa kodi na huyo mmachinga halipi hiyo kodi na wala hatumii efd machine kwako wewe unaona hakuna tatizo? Sasa nimeuliza, tunapata kodi kwa diamond sawa, japo kwa kukadilia, je kwa man fongo utatumia njia gani kupata kodi kutokana na kazi yake ya mziki? Kama kuna kitu hakipo sawa huko kariakoo sio kigezo.
 

Sasa hapa tunaongelea music industries, kama seheme nyingine hayajawekwa mazingira mazuri ndio iwe sababu ya kuacha kuwekea mkazo kwenye music? Mfanya biashara atalalamika kwenye biashara zake na mwanamziki pia atafanya hivyo kwenye tasnia yake. (According to you) kutokuwa na fair base ya tax kwenye biashara kama unavyolalamika ni sawa? Na kutokusimamia vyanzo vya mapato kwa wasanii ni sawa?
 
Huyu kijana alitumia gharama kubwa kumtengeneza bwana chibu akitarajia faida kubwa lakini alichotarajia kimekuwa ndivyo sivyo. Kwa sasa dogo anadaiwa kila kona. Namuomba Magufuli asimpendelee katk hili akanyage twende
unanuka chuki
 

Ulichokiongea kinaeleweka na ni ukweli lakini jua kuwa kila serikali ina shelia zinazohusu kazi za wasanii na kuna raw inforcement, ndio maana nimetoa mfano ukiwa tanzania ni kawaida kuona magari ya PA ya makampuni yanafanya promotion balabalani kwa kupiga nyimbo za wasanii bila mkataba wowote yaani dj anaweka kwenye playlist anapiga tu, same company utaikuta Uganda imenunua several tracks za kufanyia promotion, hata hao wenye mablogs na ma you tube chanel wengi wanajulikana but hakuna shelia ya kuwadhibiti utaishia kureport youtube ili tu zifutwe. Bado auoni tatizo, unaweza kumkamata mtu na ukashindwa kumshitaki au kulipwa fidia. Serikali kazi yake ni kusimamia hizo haki miliki za wasanii. Sasa hata kama utachukua kampuni ya kusimamia kazi zako kwenye digital platform bila sheria inafanya kazi vipi? Kwa wenzetu kuna shelia na watu wanapigwa faini ya mamilioni ya dola? Na hizo kampuni zinaendeshwa kwa faida, serikali inaweza kuamua destiny ya hawa watu, ndio maana hadhi ya msanii wa uganda, kenya, south adrica , nigeria na tanzania ni tofauti kwa sababu kila nchi ina policy zake kwenye sanaa na nyingine hazipo sawa
 
Ivi wale waliomuita na kumtolea mfano kwamba ndo mlipa kodi mzuri kati ya wanamuziki ni PSPF au TASAF
 

Mazingira ya mfanyakazi anayekatwa kodi kwa lazima kila mwezi aliyaweka nan awali? Kumbuka shule ulisoma mwenywe kwa bidii zako tena kwa kukopa kopa ada na mkopo wa chuo ulikosa lakini ulipoajiriwa tu serikali hao mbio kukufyeka. Kwa hyo haki sawa kwa wote
 
Upande wa wananchi ni upi ?

- Wanasiasa wote porojo na lao ni moja ukitumika CCM basi UKAWA wanaona wivu wanataka wakutumie wao, Ujinga mtupu

Basi akili lazima ikucheze kama msanii, we unaona bongo movie kuwa upande wa ccm hasa Makonda kumewasaidia au ndo wamejiongezea matusi kwa mashabiki na kuwapoteza zaidi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…