Dogo hajui kuimba na asilimia kubwa ya nyimbo zake ni mbovu, hata hii EP imebuma, nashangaa sana watu hawajamjulia huyu dogo, kabla hajatoa nyimbo mbovu hua anaanza kwanza kuandaa ama kutengeneza tukio la kusindikiza hizo nyimbo mpya mbovu, wakati huu akaamua aje na tukio la zuchu, inashangaza lakin ndio ukweli zuchu anajua kuimba kushinda hata dogo, akaamua atengeneze tukio na atembelee nyota ya zuchu, atafanyaje sasa kama hajui kuimba na competition ni kubwa wasanii wengine wana nyimbo kali zinapigwa kwenye sehem za burudani, sasa dj gani atapiga nyimbo ya watasubiri, baa au club ?
Kwa staili hio unategemea kwenda kuchukua tuzo za grammy, au kuitwa tu kufanya show kumbi kubwa ulaya na ku sold out ticket kama madison square, au O2 Arena, leo hii anasema eti sio wa kushindanishwa na wasanii wa tanzania, wasanii hao hao wa tanzania wanatoa nyimbo kali zinakua kama wimbo wa taifa , wewe hata hapa tu tanzania unapata competition, huko nje utaweza, utawaweza wanaijeria