Diamond Platnumz ahoji kwanini Ali Kiba (mkongwe) hana media yake? Atoa onyo kushindanishwa na wasanii wa Tanzania 'ni wadogo sana kwake'

Diamond Platnumz ahoji kwanini Ali Kiba (mkongwe) hana media yake? Atoa onyo kushindanishwa na wasanii wa Tanzania 'ni wadogo sana kwake'

Wabongo tumepewa kipaji cha majungu. Wadau, naomba tujipigie makofi kwa hilo.
 
Dogo hajui kuimba na asilimia kubwa ya nyimbo zake ni mbovu, hata hii EP imebuma, nashangaa sana watu hawajamjulia huyu dogo, kabla hajatoa nyimbo mbovu hua anaanza kwanza kuandaa ama kutengeneza tukio la kusindikiza hizo nyimbo mpya mbovu, wakati huu akaamua aje na tukio la zuchu, inashangaza lakin ndio ukweli zuchu anajua kuimba kushinda hata dogo, akaamua atengeneze tukio na atembelee nyota ya zuchu, atafanyaje sasa kama hajui kuimba na competition ni kubwa wasanii wengine wana nyimbo kali zinapigwa kwenye sehem za burudani, sasa dj gani atapiga nyimbo ya watasubiri, baa au club ?

Kwa staili hio unategemea kwenda kuchukua tuzo za grammy, au kuitwa tu kufanya show kumbi kubwa ulaya na ku sold out ticket kama madison square, au O2 Arena, leo hii anasema eti sio wa kushindanishwa na wasanii wa tanzania, wasanii hao hao wa tanzania wanatoa nyimbo kali zinakua kama wimbo wa taifa , wewe hata hapa tu tanzania unapata competition, huko nje utaweza, utawaweza wanaijeria
Diamond ndio ananyimbo nyingi zinazopigwa club kwa wasanii wa ndani, nyimbo zake zinapigwa sana kwenye sherehe mbalimbali, zinapigwa mashuleni jaribu kuangalia hata vipindi vya watoto kwenye TV nyimbo gani zinazopigwa? EP mpaka sasa inazaidi ya streams 30,000,000. Imebuma kivipi? Tujifunze strategies za biashara ya muziki la sivyo tutamuona dogo mchawi, freemason n.k.

Diamond ndio msanii pekee anayekuwa nominated kwenye tuzo za nje hata hiyo grammy, mpaka hapo ni ushahidi tosha kuwa mziki wake unatembea kuliko wasanii wengine, ndio msanii anayepiga show nje ya nchi kwenye viwanja na kujaza, suala la 02 arena n.k ni hatua halitokei kama mwanga wa radi itafika mahali anaweza kufanikiwa.

Suala la kushindana nyumbani ni suala lililokaa kinafki, hata wasanii wengine walishakataa kushindanishwa na tuzo kuzikataa akiwemo Mwana FA, Jay MO, Dully. Hivyo yeye siyo wakwanza na ni kwa sababu watu wanapenda kushushana angalia mfano kwa Jay Dee, Rubby. Ukifuata wanacho kitaka watanzania bila kufanya utafiti unapotea then wanakucheka.

Suala la kutembelea nyota ya zuchu si kweli ile ni promotion angalia hatua za kanye kwenda kuzindua Donda alifanya nini na mauzo yake yakoje mpaka sasa?

Mziki umebadilika.
 
Diamond washabiki wake wanamshindanisha na Wizkid sasa kwan yeye yupo level za wizkid ayo?

Sent from my SM-G960U1 using JamiiForums mobile app
Diamond anasema tusishindanishwe ndani ila tushinane na wasanii wa nje, lengo ni ku-win soko la nje. Kumshindanisha Diamond na WIZKID ni sawa, ALI KIBA na WIZKID ni sawa, KUSA na wizkid, Nandi na YEMI ALADE. Hata katika mpira hatuwezi tukawa tunaishia tu yanga na simba, lazima tupambane wakashindane na timu za nje tena kubwa, ndio watapata hela nyingi, wachezaji wataonekana zaidi.
 
Dogo hajui kuimba na asilimia kubwa ya nyimbo zake ni mbovu, hata hii EP imebuma, nashangaa sana watu hawajamjulia huyu dogo, kabla hajatoa nyimbo mbovu hua anaanza kwanza kuandaa ama kutengeneza tukio la kusindikiza hizo nyimbo mpya mbovu, wakati huu akaamua aje na tukio la zuchu, inashangaza lakin ndio ukweli zuchu anajua kuimba kushinda hata dogo, akaamua atengeneze tukio na atembelee nyota ya zuchu, atafanyaje sasa kama hajui kuimba na competition ni kubwa wasanii wengine wana nyimbo kali zinapigwa kwenye sehem za burudani, sasa dj gani atapiga nyimbo ya watasubiri, baa au club ?

Kwa staili hio unategemea kwenda kuchukua tuzo za grammy, au kuitwa tu kufanya show kumbi kubwa ulaya na ku sold out ticket kama madison square, au O2 Arena, leo hii anasema eti sio wa kushindanishwa na wasanii wa tanzania, wasanii hao hao wa tanzania wanatoa nyimbo kali zinakua kama wimbo wa taifa , wewe hata hapa tu tanzania unapata competition, huko nje utaweza, utawaweza wanaijeria
mbona unaongea pumba, inamaana kwenye soko la music target ni nyimbo za club tu. Inamaana kwenye ep hujaona wimbo kama fresh, sona nk za club au unaongea chuki tu, hivi unaposema ep imebuma unatumia vigezo gani mkuu?
 
Screenshot_20220314-214537.png
 
Hio namba tatu embu ngoja kwanza tui list tuone

1. Wizkid
2. Burna boy
3. Davido

Alaf tuwaache madogo ambao wamepiga shows o2 arena hadi Marekani na wamepiga kolabo kubwa na watu kama wakina ed sheeran na justine bieber madogo hao ni Joe Boy, Fire Boy na wapopo wengine wengine kibao wakina simi nani na nani?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] looh hio top 3 nadhani ndo ile kitu wabongo wanasema "ametupiga na kitu kizito".
Top 3 ya mchongo,
 
Hii ni interview au kichambo duh!

Jamaa anajibrag mpaka anadanganya, mbaya zaidi anakandia wengine hapo u proffesional wake uko wapi?

Hivi wasanii top 3 Africa naye yumo anatuonaje lakini?
Dabliyusibii wanaamini, ni Kama misukule
 
Wakina Zuchu, Rayvanny, mbosso na harmonize Nani kawabeba?
Hajabeba mtu hapo, huo ni mtaji wake wa biashara, kubebana wanabebana Nigeria huko, WizKid na Burna ni mfano mzuri, wanaalikana Hadi kwenye maconcert kutoa support, wanafanya collabo, na labels zao ni tofauti.
 
Diamond anasema tusishindanishwe ndani ila tushinane na wasanii wa nje, lengo ni ku-win soko la nje. Kumshindanisha Diamond na WIZKID ni sawa, ALI KIBA na WIZKID ni sawa, KUSA na wizkid, Nandi na YEMI ALADE. Hata katika mpira hatuwezi tukawa tunaishia tu yanga na simba, lazima tupambane wakashindane na timu za nje tena kubwa, ndio watapata hela nyingi, wachezaji wataonekana zaidi.
Nmeelewa sasa

Sent from my SM-G960U1 using JamiiForums mobile app
 
Hajabeba mtu hapo, huo ni mtaji wake wa biashara, kubebana wanabebana Nigeria huko, WizKid na Burna ni mfano mzuri, wanaalikana Hadi kwenye maconcert kutoa support, wanafanya collabo, na labels zao ni tofauti.
Upo level gani ya kielimu?
 
Back
Top Bottom