Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

PITIA K VANT 3 KWA MANGI, NAKUJA KULIPA
 
Sooner they will start sending the attacks to Rayvanny, Matter of fact the kid has no hard skin like his brother Harmonize then will forget him soon.
Kwani mzee baba aliyeanzisha Ligi na Wasafi baada ya kutoka ni nani? Baada ya harmonize kutoka Wasafi alianza kuandika nyimbo za kuwaattack Wasafi ndio maana akawa anashambuliwa na mawacha wa Wasafi ni hivo hivo kwa kiba machawa hawakuattack kama hujawagusa mabosi ila ukiwagusa tu mabosi wao ndio watakushambulia
 
Dayamondi is right. WCB isn't a not-for-profit organization. Lazima hela yao irudi na faida juu kama biashara zingine zote.

Wasanii wanasaini mikataba so they know what they get into na taratibu za kuvunja hiyo mikataba, kama hawakubaliani na masharti wasikubali kujiunga. It's that simple.
 
Diamond ni mwimbaji na choreographer mzuri sana , lakini kukosa elimu kunamuangusha sana.

Hana song writers na anaishia kuimba mashairi ya matusi yasiyotamkika.

Kuna siku nimepanda Emirates, nikapenda kusikiliza nyimbo za nyumbani.
Nilipochagua nyimbo za Diamond kukawa na angalizo kuwa nyimbo hizi hazina hadhi na zina matusi, na ukisikiliza its at your own risk.

Abadilike na aende shule , bado kijana na inabidi hadhi yake iendane na ustaarabu.
 
Yaani ku mbrand msanii mmoja na kumtangaza ifikie MILLION 500
500000000
Nadhani wewe ufuatilii mziki wa sasa wewe ulikuwa ni mshabiki wa mziki wa zamani ndio maana vitu vingi ujui huyo msanii anapewa apartment na label analipiwa kodi, kapewa photographer ambaye analipiwa na label kuna madancer, mabodyguard, videos za nyimbo zake zote pamoja na audio, promotion local and international, gharama za designers za mavazi yake kila anapoenda kwenye shows au activities za music, gharama za kuandaa shows n.k piga calculation cost zake kwa muda ambao yupo hapo kwenye label how much label will spend
 
Mkuu nyimbo za diamond hazina matusi wewe na hao waluozitafsiri ndio kuna shida
 
Nashauri Basata wangeweka kitengo maalum kwa ajili ya kupitia mikataba ya kati ya wasanii na lebo au wasanii na kampuni nyingine,kabla ya kuingia kandarasi.

Ni sawa na hii tume ya ushindani(FCC)ambayo inadhibiti na kupitisha mikataba inayotumiwa na Microfinaces kutoa mikopo kwa wateja au kama ambavyo benki kuu inadhibiti sheria na mikataba ya mikopo baina ya benki za kibiashara na wateja wao.

Hii itaondoa haya malalamiko baada ya mtu kuingia kwenye mikataba ndio anaanza kelele,kwa mazingira yetu wasanii wengi hawana elimu ila wana vipaji kwahio mambo mengi haya ya taratibu na sheria hawajui hasa ikizingatiwa wengi wanapoanza usanii wanakuwa hawana exposure,hawana uelewa na wana shida ya pesa hivyo ni rahisi kukubali chochote kilichopo mezani.

Haya malalamiko hayajaanza leo,tangu bongo movie walikuwa wakilaamikia wahindi,Ikaja hawa bongofleva wakamlaumu sana Ruge na wengineo,Na sasa Diamond nae ameingia kwenye lawama lakini yote haya ukiangalia ni kukosa udhibiti na uelewa mdogo wa wasanii.

Mwaka jana kama sikosei kuna msanii wa kike sijui ni Nandy au nani alilalamikia kampuni fulani sijui ilikiwa benki ile kumtumia na kumlipa malipo kiduchu.

Sasa tunawauliza nyie wasanii mnapoingia mikataba mwanzoni huwa hamuoni?kama mnaona kwanini hamkatai?Kwa hili naona Diamond yupo sahihi,kama ulikubali mikataba basi kubaliana na madhara yake pia.
Kwahio lazima kuwe na udhibiti wa hii mikataba,kama hii ni biashara basi Basata kama chombo cha serikali lazima ijue nini kimeandikwa humo na je hakikiuki sheria na taratibu za nchi?

Inawezekana pia katika hili Diamond akawa anatumia Lebo yake kujinufaisha zaidi dhidi ya wasanini wadogo kwa kisingizio kwamba amewekeza kwao,kwahio udhibiti unahitajika hapa.
 
Kama huna chuki binafsi basi nachelea kusema hujamuelewa jamaa alichosema.
 
Na hiyo point ya mwisho sidhani kama inakwepeka kwa tajiri kama yeye anaetaka kuendelea kua tajiri.

Ni vile tu vijana wanakua hawana mtu wa karibu wa kuwasimamia kwenye hiyo mikataba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…