Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Ni ngumu saana kumuelewesha mtu mweusi haswa linapokuja suala la uwekezaji,yeye huangalia matokeo tuu apate chake na si kuukuza mtaji ama ile biashara ili na yeye anufaike na wengine waje wanufaike.
Muziki ni moja kati ya biashara ngumu saana zama hizi za kidigital maana kila kona ukigusa wanataka pesa tuu hata kupostiwa weka pesa mezani
 
Nashauri Basata wangeweka kitengo maalum kwa ajili ya kupitia mikataba ya kati ya wasanii na lebo au wasanii na kampuni nyingine,kabla ya kuingia kandarasi.

Ni sawa na hii tume ya ushindani(FCC)ambayo inadhibiti na kupitisha mikataba inayotumiwa na Microfinaces kutoa mikopo kwa wateja au kama ambavyo benki kuu inadhibiti sheria na mikataba ya mikopo baina ya benki za kibiashara na wateja wao.

Hii itaondoa haya malalamiko baada ya mtu kuingia kwenye mikataba ndio anaanza kelele,kwa mazingira yetu wasanii wengi hawana elimu ila wana vipaji kwahio mambo mengi haya ya taratibu na sheria hawajui hasa ikizingatiwa wengi wanapoanza usanii wanakuwa hawana exposure,hawana uelewa na wana shida ya pesa hivyo ni rahisi kukubali chochote kilichopo mezani.

Haya malalamiko hayajaanza leo,tangu bongo movie walikuwa wakilaamikia wahindi,Ikaja hawa bongofleva wakamlaumu sana Ruge na wengineo,Na sasa Diamond nae ameingia kwenye lawama lakini yote haya ukiangalia ni kukosa udhibiti na uelewa mdogo wa wasanii.

Mwaka jana kama sikosei kuna msanii wa kike sijui ni Nandy au nani alilalamikia kampuni fulani sijui ilikiwa benki ile kumtumia na kumlipa malipo kiduchu.

Sasa tunawauliza nyie wasanii mnapoingia mikataba mwanzoni huwa hamuoni?kama mnaona kwanini hamkatai?Kwa hili naona Diamond yupo sahihi,kama ulikubali mikataba basi kubaliana na madhara yake pia.
Kwahio lazima kuwe na udhibiti wa hii mikataba,kama hii ni biashara basi Basata kama chombo cha serikali lazima ijue nini kimeandikwa humo na je hakikiuki sheria na taratibu za nchi?

Inawezekana pia katika hili Diamond akawa anatumia Lebo yake kujinufaisha zaidi dhidi ya wasanini wadogo kwa kisingizio kwamba amewekeza kwao,kwahio udhibiti unahitajika hapa.
Nina uhakika BASATA wakiweka hiko kitengo na kuweka vigezo label itakayo baki itakuwa WCB pekee,maanake label nyingine zimekuwa kama vijiwe vya kahawa mchana stori jioni kulala shows hawana,branding hamna wapo wapo tu.
 
Nashauri Basata wangeweka kitengo maalum kwa ajili ya kupitia mikataba ya kati ya wasanii na lebo au wasanii na kampuni nyingine,kabla ya kuingia kandarasi.

Ni sawa na hii tume ya ushindani(FCC)ambayo inadhibiti na kupitisha mikataba inayotumiwa na Microfinaces kutoa mikopo kwa wateja au kama ambavyo benki kuu inadhibiti sheria na mikataba ya mikopo baina ya benki za kibiashara na wateja wao.

Hii itaondoa haya malalamiko baada ya mtu kuingia kwenye mikataba ndio anaanza kelele,kwa mazingira yetu wasanii wengi hawana elimu ila wana vipaji kwahio mambo mengi haya ya taratibu na sheria hawajui hasa ikizingatiwa wengi wanapoanza usanii wanakuwa hawana exposure,hawana uelewa na wana shida ya pesa hivyo ni rahisi kukubali chochote kilichopo mezani.

Haya malalamiko hayajaanza leo,tangu bongo movie walikuwa wakilaamikia wahindi,Ikaja hawa bongofleva wakamlaumu sana Ruge na wengineo,Na sasa Diamond nae ameingia kwenye lawama lakini yote haya ukiangalia ni kukosa udhibiti na uelewa mdogo wa wasanii.

Mwaka jana kama sikosei kuna msanii wa kike sijui ni Nandy au nani alilalamikia kampuni fulani sijui ilikiwa benki ile kumtumia na kumlipa malipo kiduchu.

Sasa tunawauliza nyie wasanii mnapoingia mikataba mwanzoni huwa hamuoni?kama mnaona kwanini hamkatai?Kwa hili naona Diamond yupo sahihi,kama ulikubali mikataba basi kubaliana na madhara yake pia.
Kwahio lazima kuwe na udhibiti wa hii mikataba,kama hii ni biashara basi Basata kama chombo cha serikali lazima ijue nini kimeandikwa humo na je hakikiuki sheria na taratibu za nchi?

Inawezekana pia katika hili Diamond akawa anatumia Lebo yake kujinufaisha zaidi dhidi ya wasanini wadogo kwa kisingizio kwamba amewekeza kwao,kwahio udhibiti unahitajika hapa.
Ukiacha WCB, unaweza taja lebo nyingine iliyofanikiwa kutoa wasanii wake wakafanikiwa? Pia hii WCB ina wasanii wangapi wanaotumika kama reference ya unyonyaji kati ya wasanii maelfu TZ?
 
Huwa simpendi Diamond na vituko vyake, ila kwa hili yuko sahihi.

Wasafi ni music label, wako pale kutengeneza pesa kupitia muziki, sio kutoa msaada wa kukuza majina ya watu bure!

Kabla ya wasafi, Rayvanny alikua wapi? Harmonize alikua wapi? Vipi hapo walipofika leo, wangeweza kufika bila label ya Wasafi?

Hakuna kitu kinaitwa "Unyonyaji" kwenye dunia ya mabepari. Umepewa mkataba, ukausoma, na ukaona unafaa ukasaini. Hakuna la ziada hapo. Nitaamini Wasafi ni wanyonyaji siku akitokea mtu akatae mkataba wao mwanzoni kabisa kabla ya kupata umaarufu.

Sio mtu unatolewa manzese huko, watu wanakubrand, wanakupambania unahit mpaka nje ya nchi, alafu wakichukua return ya uwekezaji wao unasema wanyonyaji. Hakuna free lunch dadek!
Kabisaa
Fact
 
Ulimwengu wa kibepari HAUHITAJI HISIA HATA KIDOGO!!
Mtu awekeze kwao,akuze brand yako,akupe channel ya kukuingizia hela hata miaka 30 ijayo afu ukitaka kuondoka uondoke tu sababu sauti ni yako na ntimbo uliandika wewe??Ujamaa huu unatudumaza sana sisi watanzania.
Na hao mnaowaita wakongwe wanaongea tu sababu ya roho mbaya zao na wivu.walichezea senti mbili zao wakiwa kwenye peak,upeo umewapita na walau sasa soko linaweza toa hela ukiwa serious na zaidi sana hawakutarajia dogo angekaza mpaka hii leo na kuwa mkubwa kama alivyo so they just hating on him.Much as ana mapungufu yake mengine mengi kama binadamu yoyote,from the bussiness perspective kijana YUKO SAHIHI SANAA
 
Msanii wa kimataifa Diamond Platnumz akifanyiwa mahojiano na kituo Cha habari cha DW Swahili nchini Germany amejibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na mwanahabari Moja Kati ya swali ni kuhusu tuhuma ya baadhi ya watu kusema Wasafi ni wanyonyaji.

Diamond amejibu kama ifuatavyo

Nimekuwa nikiwachukua wasanii wachanga nakuwaleta Wasafi wakiwa hawana majina na kuwageuza kuwa biashara kwa kuwekeza hela nyingi unakuta natumia mpaka 500M Kwenye uwekezaji kwa msanii mmoja katika kubrand, kumtangaza na kufanya sanaa yake iwe kubwa ndio maana baada ya kumchukua msanii tunamfundisha vitu vingi Kwenye industry ya mziki ambayo alikuwa hajui tunamsaidia kwenye kuimba, kucheza na namna ya kumaintain status yake kwenye mziki ndio maana unakuta kabla ya kumtoa msanii inatuchukua miaka au miezi ili kumfanya awe full package kabla atujamtambulisha kwenye industry.

Industry yetu inazidi kukuwa na baadhi ya mambo watu wanaanza kuyaelewa hasa yanahusu biashara ya mziki tunachofanya sisi Wasafi ndio hata industry ya mziki wa Marekani wanafanya kwenye label nyingi shida ni Moja msanii ukishamfanya kuwa mkubwa na akishaona hela nyingi zinaingia kwenye label anaingia tamaa anatamani hela yote angekuwa anapata yeye ndio maana anaona kama ananyonywa anashindwa kujua hii ni biashara na tuwekeza hela nyingi kwake hakuchangia chochote kipindi tunamkuuza.

So lazima kuwe na return ya kile tulichowekeza mfano mimi sio kwamba hela zote napata pekee yangu lazima niwalipe wakina Sallam, Babu tale na Mkubwa fella ndio biashara ilivyo hauwezi kuondoka kirahisi tu njoo hapa tumalizane wakati pia hii label inalipa kodi na ipo kisheria na inatambulika na mamlaka ya mapato mfano last year tumelipa kodi 100M hivi tukikuachia kirahisi tu nani atalipa kodi? Hivi kuhusu kipaji kingine tutachokileta kwenye label nani atagharamia?

Nini Maoni yako kwenye majibu haya ya Mondi
Tatizo ni kwamba transparency haipo mpaka amulikwe na media.

Utetezi mzuri, sasa turudi kwenye sheria inasemaje
 
Huwa simpendi Diamond na vituko vyake, ila kwa hili yuko sahihi.

Wasafi ni music label, wako pale kutengeneza pesa kupitia muziki, sio kutoa msaada wa kukuza majina ya watu bure!

Kabla ya wasafi, Rayvanny alikua wapi? Harmonize alikua wapi? Vipi hapo walipofika leo, wangeweza kufika bila label ya Wasafi?

Hakuna kitu kinaitwa "Unyonyaji" kwenye dunia ya mabepari. Umepewa mkataba, ukausoma, na ukaona unafaa ukasaini. Hakuna la ziada hapo. Nitaamini Wasafi ni wanyonyaji siku akitokea mtu akatae mkataba wao mwanzoni kabisa kabla ya kupata umaarufu.

Sio mtu unatolewa manzese huko, watu wanakubrand, wanakupambania unahit mpaka nje ya nchi, alafu wakichukua return ya uwekezaji wao unasema wanyonyaji. Hakuna free lunch dadek!
Word!
 
Back
Top Bottom