Diamond Platnumz amewakosea nini wanaomshambulia?

Naomba kujua nini kibaya Diamond Platnumz anakosea tofauti na wasanii wengine?

Nini afanye ili iwe sawa naonaga watu wanamshambulia ila sijawahi sikia mtu yeyote akisema makosa anayofanya tofauti na watu wengine?
Dogo ni mshamba mno yaani ushamba kwao ni chakula mpaka wanakera.
 
ya harmo nae kuachia siku moja na simba mbona mnashangilia? au yeye hapaswi kuchukiwa
 
Umeandika upuuzi mtupu, yaani msaani X hatakiwi kutoa wimbo wake kwa sababu msanii Y ametoa wimbo, hii akili ya wapi hii ?
 
Tangu mzee Maria na Miss Kigogo wameanza kumshambulia kule twita wakisaidiwa na wafuasi wao umewahi kuona Diamond akiwajibu chochote ?
 
Shortly ni tabia za kibinadamu,kuchukia na kupenda pia. wamepingwa na kupongezwa pia watu wengi mno toka huko nyuma. kwaio dont mind ni akili zetu tu na hakuna atakaye toa jibu litakalokuwa na mashiko kwenye kuchukia hilo na hata wenye kupendelea pia.

kwenye industry ya muziki amefanya mengi makubwa na hata ni wasanii wachache tu ambao tunaweza kulinganisha nae kwa alichokifanya lakini haituzuii kumchukia au kumpenda kwa vile tumeumbwa na roho hizo..
 
Haki haupewi kama zawadi, ni lazima uipiganie, sasa nyinyi wanaharakati uchwara mnapiga makelele mitandaoni huku mkikutana face to face na mnaowapigia kelele mnaishia kujikesha chekesha tu
 
Kweli ila natamani kujua anachokosea tumuhukumu kwa haki
Kosa kubwa alilofanya Mondi kuwa karibu na Bashite...na Roma alivyotekwa akatoa kawimbo kake nikae kimya huku akidharau vijana wanaozunguka barabarani na bahasha wakitafuta kazi ..mbaya zaidi aliposema yeye ni kada wa CCM wakati 90% ya vijana hawapendi CCM..alitakiwa akafanye kampeni Kama mwanamuziki mfanya biashara sio kusema nafanya kampeni hata bure...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…