Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amejivunia kumiliki gari la kifahari aina ya Bentley Continental GT W12 ya mwaka 2019. Gari hilo lilionekana kwenye msafara wa Diamond alipokuwa akienda Ivory Coast kwa ajili ya show yake, likifuatana na Cadillac na Rolls Royce.
Bentley hiyo ina uwezo wa kufikia kasi ya 318 km/h (198 mph) na inaweza kutoka 0 hadi 100 km/h kwa sekunde 4.3. Gari hili linajulikana kuwa ni chaguo la mastaa wengi duniani na sasa linauzwa kwa $230,000, sawa na TSh 575,000,000. Pamoja na kodi na usafirishaji hadi Tanzania, gharama ya kuiingiza inakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 900.
Diamond Platnumz sasa anamiliki magari manne ya kifahari, ambayo ni Rolls Royce, Bentley, na Cadillac Escalade 2, zote za mwaka 2019.
Pia, Soma: Billnass amzawadia mtoto wake Naya, gari aina ya Alphard, aahidi kumpa gari la kifahari 'Escalade'
Pia, Soma: Billnass amzawadia mtoto wake Naya, gari aina ya Alphard, aahidi kumpa gari la kifahari 'Escalade'