Diamond Platnumz anunua gari mpya la kifahari Bentley GT W12 ya Milioni 500

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amejivunia kumiliki gari la kifahari aina ya Bentley Continental GT W12 ya mwaka 2019. Gari hilo lilionekana kwenye msafara wa Diamond alipokuwa akienda Ivory Coast kwa ajili ya show yake, likifuatana na Cadillac na Rolls Royce.

Bentley hiyo ina uwezo wa kufikia kasi ya 318 km/h (198 mph) na inaweza kutoka 0 hadi 100 km/h kwa sekunde 4.3. Gari hili linajulikana kuwa ni chaguo la mastaa wengi duniani na sasa linauzwa kwa $230,000, sawa na TSh 575,000,000. Pamoja na kodi na usafirishaji hadi Tanzania, gharama ya kuiingiza inakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 900.

Diamond Platnumz sasa anamiliki magari manne ya kifahari, ambayo ni Rolls Royce, Bentley, na Cadillac Escalade 2, zote za mwaka 2019.

Your browser is not able to display this video.

Pia, Soma: Billnass amzawadia mtoto wake Naya, gari aina ya Alphard, aahidi kumpa gari la kifahari 'Escalade'
 
Hii mipesa ya laana ya unga na usengee huwa haikawii wishi na wakafirisika. Badala ya kuwekeza kwenye vitu vya maana, wanawekeza kwenye matoi ya kitasha.
 
Daaah ahsante khadija kopa kwa update
 
Hongera zake

kwanini gari inawaka moto? Mad Max
Naam mkuu.

Sema mtoa mada katudanganya iyo sio ya 2020.

Iyo ni second generation ya 2013 iyo.

Third gen inaanzia 2018 yenyewe moto zaidi.


Pia naona kama bei zimeongezwa sifuri. Maana gari ya 2013 huwezi pata mpya ni used.



TRA nao hawataki mchezo wanataka mil 120.


Kwahiyo on average mil 250 unapata iyo chuma.

No hate na Mond wala simpingi mtoa mada, mawazo yangu tu haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…