Diamond Platnumz arekodi ngoma na Wiz Khalifa

Diamond Platnumz arekodi ngoma na Wiz Khalifa

Naomba link ya kazi waliyofanya, kupiha picha sio tatizo, hata rafiki yangu ana picha pamoja na kikwete ila hana hata awasiliano nae
Basi na wewe leta kazi ya diamond na wizkhalifa kama picha inamaanisha mfanye kazi
 
Basi na wewe leta kazi ya diamond na wizkhalifa kama picha inamaanisha mfanye kazi

Taabu lazima muipate tu 😎😎, kijana anapiga hatua ila kuna watz kama nyie mafanikio yake yanawafanya muwashwe

 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Hizo ni pichatu za kawaida, wasanii wengi wa marekani kupiga nao picha mkikutana hawana maringo

Hawa wapo studio kikazi, sio picha tu ilimradi

View attachment 1842281
Kwani picha ya kazi na picha ya kawaida tofauti ni nini au Kuna nyingine wamesima miguu juu? Mpaka watoe huo wimbo ,hata wakazi angesema hizo picha za kazi hamna anayekataa,hakuna utofauti wa picha tatizo mnasifia ujinga tu ,picha akipiga wakazi na wiz khalifa ni tofauti akipiga diamond na wiz khalifa kivipi?
 
Hata kama Diamond simpendi lakini kusema eti anakutana na wastaafu ambao hawahiti unakua umejitoa akili na unaonyesha kabisa unafikiria kwa kutumia makalio na sio akili.

Hao wasanii wanaohiti wana view ngapi YouTube?

Ni msani gani anamfikia Wiz kwenye view za YouTube? Ana ngoma imeangaliwa mara bilioni 5 na milioni mia kadhaa, hao wanaohiti wana hata ngoma ya view milioni mia tano?

Wiz bado ana influence kubwa sana kwa sababu ngoma yake ya 5B bado inampa mileage kubwa sana na inaangaliwa na mamilioni ya watu kila siku. Hilo tu linamfanya wiz aendelee kua ni mtu anaetafutwa sana YouTube kuliko hao wasanii wenu mnaosema wanahit, bora hata wangekua wanaheat kuliko kuhit.

Hata kama Diamond hatumpendi lakini kwenye ukweli tuwe wakweli.

Ni sawa na mtu aseme leo ukifanya ngoma na J-Zey umefanya na msaafu, hiyo itakua akili ama mavi?

Mwakani wiz atakua na view bilioni 7 na hakuna hata msaanii mmoja wa hao wanaohiti sasa atakua na hata view milioni 200.
diamond hana ubunifu, he is done

remake za nyimbo zimemuonyesha kama yuko relevance, zero anapotea
 
Alikiba katoa song salute ft p square aliyechuja mnaimba pambio kila siku,
Now diamond yupo na wizkhalifa mnadai kachuja?
Witch hunt.
Unawachoma sindano kali sana, haters usipowaunga mkono ndiyo wanazidisha chuki na wanafura kwa hasira. Just take them slow usije kujikuta umekuwa kama wao ukaonyesha hate kwa mtu asiyehusika, huyo Kiba naye anapambana kwa kiwango chake si vibaya kwani naye amefunguka kwamba international collaborations zina umuhimu katika kukua kwake kisanaa japo awali alikuwa anaziponda sana. Better late than never hivyo aendelee kupambana.
Wabongo wana husda na huumizwa sana na mafanikio ya mtu, huyu dogo Sadala atazidi kuwatesa kwani ana malengo ya mbali sana na ni fighter asiyesikiliza vijibwa vinavyobweka pembeni visije kumpoteza direction. Level za Afrika ashaanza kuziachia vumbi sasa anapambania level za mbele.
To him, sky is just the beginning.
 
Anyway, mimi siyo muumini sana wa collabo hasa za kuwashirikisha wamarekani. Unless hizo collabo ziwe unafanya tu kutimiza ndoto yako kufanya kazi na msanii fulani, maana hata hao wasanii wa Marekani mara nyingi huwa wanafanya hizi collabo kama charity tu.

Mifano halisi kwamba hizi collabo hazina impacts,

  • Davido feat Meek Mill
  • Wizkid feat Drake
  • Davido feat Chris Brown
  • Dbanj feat Gucci mane
  • 2face feat TPain
  • Fuse ODG feat Ed Sheeran
  • Fuse ODG feat Sean Paul
  • Mr Easy feat Tyga

Hizi collabo zimefanyika lakini mpaka leo hazijasaidia chochote kwenye muziki wao.
True say, hua sioni impact yoyote
 
Back
Top Bottom