Diamond Platnumz: Aslay angekuwa chini yangu angefika mbali zaidi

Diamond Platnumz: Aslay angekuwa chini yangu angefika mbali zaidi

Sii wakati wote kufanya kazi za kujitegemea kunampa mtu kipato zaidi ya kuajiriwa au kufanya kazi kwa mkataba chini ya mtu. Sii wakati wote. Ndio maana watu wengi wanaoenda ajira. Ili watumwe.
Ingawa mimi sio mtaalamu wa mziki lakini mtu anaweza kuwa mwimbaji, mpiga gitaa, mnenguaji mzuri sana lakini asipochanganya vionjo na wenzake hafiki mbali. Ali Choki alipotoka Twanga Pepeta alifika wapi?
Kuwa chini ya Diamond ni ajira. Ama ya mkataba au ya mshahara. Lazima msanii afuate masharti ya mwajiri wake kulingana na walivyokubaliana. Umaarufu wa msanii unatokana na lebel aliyopo ambayo inamwongezea vionjo vinavyokubalika kwenye soko. Ufundi wa juweka vionjo kwenye mziki ndio umaarufu wa lebel yenyewe. Nje ya hapo msanii anayetoka anakosa vionjo vya nyongeza mziki wake unaanza kuteremka.
Diamona anatumia fedha kuwapandisha kimziki. Wanalipwa. Wanapata umaarufu. Siko linaongezeka. Wanapata kipato zaidi. Wakioata hela na umaaru waliotengenezewa wanasema wanayinywa. Hapana.
 
Back
Top Bottom