Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Dai ni Freemason na ana pepo la Uasherati, kila anayetembea naye anaharibikiwa, na haolewi.Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao ongeza kiukweli anatakiwa atafute mhariri wa mashairi na mistari yake. Kwenye ngoma ya ongeza anasema "we ndo wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe" anamuongelea mwanamke/ msichana/demu wake.
Kwa hili Diamond hapana umeenda mbali mno na umetukosea Wakristo. Hivi mkristo aimbe wimbo amljnganishe demu wake na Mtume Mohammad au Allah atakuwa sawa?
Kwetu Wakristo Yesu ni Mungu kweli, mtu kweli Yohana Mtakatifu 1:1-10. Yesu ni Mungu mwana katika nafsi tatu za Mungu zinazofanya Utatu Mtakatifu.
Yesu aliacha kiti chake cha nzi kule mbinguni akauvaa mwili akashuka duniani ili atufie na kutukomboa sisi na dhambi zetu. Alisulubiwa akafa, akazikwa siku ya tatu akafufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na hapa tulipo tunasubiri arudi aje awahukumu walio hai na wafu. Maana ameahidi anakwenda kwa Baba kutuandalia makao na atakuja kutuchukua ili alipo nasi tuwepo. Je ni Yesu huyu wa kumlinganisha na demu wake kweli Diamond Platnumz?
Yesu huyu ambaye alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa ambaye maandiko yanasema vitu vyote viliumbwa kwa jina lake na pasipo yeye hakuna kilichoumbwa? Huyu ndiyo wa kumlinganisha na demu.
Ni kweli sanaa inahitaji ubunifu lakini siyo kwa kiwango hiki Diamond aombe radhi kwa kweli au wimbo wake ufungiwe na BASATA.
Mwanamke unayekubali ku-michwa na Dai huolewi.
Hesabu kuanzia " kialama", "Wama Sapatwa" , Ze Buss Zali", Amisi Mabito", na wenzake wengi, hawaolewi