Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao ongeza kiukweli anatakiwa atafute mhariri wa mashairi na mistari yake. Kwenye ngoma ya ongeza anasema "we ndo wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe" anamuongelea mwanamke/ msichana/demu wake.

Kwa hili Diamond hapana umeenda mbali mno na umetukosea Wakristo. Hivi mkristo aimbe wimbo amljnganishe demu wake na Mtume Mohammad au Allah atakuwa sawa?

Kwetu Wakristo Yesu ni Mungu kweli, mtu kweli Yohana Mtakatifu 1:1-10. Yesu ni Mungu mwana katika nafsi tatu za Mungu zinazofanya Utatu Mtakatifu.

Yesu aliacha kiti chake cha nzi kule mbinguni akauvaa mwili akashuka duniani ili atufie na kutukomboa sisi na dhambi zetu. Alisulubiwa akafa, akazikwa siku ya tatu akafufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na hapa tulipo tunasubiri arudi aje awahukumu walio hai na wafu. Maana ameahidi anakwenda kwa Baba kutuandalia makao na atakuja kutuchukua ili alipo nasi tuwepo. Je ni Yesu huyu wa kumlinganisha na demu wake kweli Diamond Platnumz?

Yesu huyu ambaye alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa ambaye maandiko yanasema vitu vyote viliumbwa kwa jina lake na pasipo yeye hakuna kilichoumbwa? Huyu ndiyo wa kumlinganisha na demu.

Ni kweli sanaa inahitaji ubunifu lakini siyo kwa kiwango hiki Diamond aombe radhi kwa kweli au wimbo wake ufungiwe na BASATA.
Dai ni Freemason na ana pepo la Uasherati, kila anayetembea naye anaharibikiwa, na haolewi.
Mwanamke unayekubali ku-michwa na Dai huolewi.
Hesabu kuanzia " kialama", "Wama Sapatwa" , Ze Buss Zali", Amisi Mabito",
na wenzake wengi, hawaolewi
 
Kwahiyo kutoolewa Ni ufreemason? basi Freemason wapo wengi Sana.
 
Qummk [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kama unataka nitakupa full story. Jamaa si alikuwa fundi selemara, sasa ilikuwaje kapelekwa mahakamani (kwa Pilato) huku kabeba mbao zake. Kuna neno hapo, fikiria mara mbili kabla ujajiumiza kichwa.
 
Dai ni Freemason na ana pepo la Uasherati, kila anayetembea naye anaharibikiwa, na haolewi.
Mwanamke unayekubali ku-michwa na Dai huolewi.
Hesabu kuanzia " kialama", "Wama Sapatwa" , Ze Buss Zali", Amisi Mabito",
na wenzake wengi, hawaolewi

Okay, tuwekee picha ya mumeo ambae. amekuwowa.
 
nimeandika nikafuta, anyway kupanga ni kuchagua,haya ni maisha yako lakini nakushauri usiwahi kuropoka hayo maneno mbele za watu,ishia huku tu

Wewe ni stupid mmoja hivi ambae umeenda shule kuhesa vidato ukaacha elimu ikutawale badala ya upata majibu kutokana na elimu unsyosumbua kichwa yako kila siku. If you believe on Jesus or Mohammed, it's clear, you're stupid. Do we need excuse for this? No, you're a plain stupid.
 
Jamaa anawapeleka puta left, right and center mpaka mseme bas!
Utakuta hiyo verse kaiweka makusudi akijua mtakomalia kujadili.
Acoustic simple tu atapata kiki kubwa, views nyingi, mkwanja, maisha yanaendelea....hata kama ikifungiwa kiki tayari....
 
Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao ongeza kiukweli anatakiwa atafute mhariri wa mashairi na mistari yake. Kwenye ngoma ya ongeza anasema "we ndo wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe" anamuongelea mwanamke/ msichana/demu wake.

Kwa hili Diamond hapana umeenda mbali mno na umetukosea Wakristo. Hivi mkristo aimbe wimbo amljnganishe demu wake na Mtume Mohammad au Allah atakuwa sawa?

Kwetu Wakristo Yesu ni Mungu kweli, mtu kweli Yohana Mtakatifu 1:1-10. Yesu ni Mungu mwana katika nafsi tatu za Mungu zinazofanya Utatu Mtakatifu.

Yesu aliacha kiti chake cha nzi kule mbinguni akauvaa mwili akashuka duniani ili atufie na kutukomboa sisi na dhambi zetu. Alisulubiwa akafa, akazikwa siku ya tatu akafufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na hapa tulipo tunasubiri arudi aje awahukumu walio hai na wafu. Maana ameahidi anakwenda kwa Baba kutuandalia makao na atakuja kutuchukua ili alipo nasi tuwepo. Je ni Yesu huyu wa kumlinganisha na demu wake kweli Diamond Platnumz?

Yesu huyu ambaye alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa ambaye maandiko yanasema vitu vyote viliumbwa kwa jina lake na pasipo yeye hakuna kilichoumbwa? Huyu ndiyo wa kumlinganisha na demu.

Ni kweli sanaa inahitaji ubunifu lakini siyo kwa kiwango hiki Diamond aombe radhi kwa kweli au wimbo wake ufungiwe na BASATA.
Ile ya Jiwe alivyoitwa kwamba yeye ni Yesu vipi na ile? Au ile ni sawa?!
 
Ni makufuru kumlinganisha Yesu na girl friend wake, lakini pia ni makufuru kumwita Yesu Mungu Muumba wa mbingu na dunia.

Soma Mathayo 16:16,17 Simoni Petro akajibu: “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”17 Yesu akamwambia: “Mwenye furaha ni wewe, Simoni mwana wa Yona, kwa sababu mwili na damu havikukufunulia hilo, bali Baba yangu aliye mbinguni ndiye aliyekufunulia.

Yohana 14; 28 Mlisikia nikiwaambia, ‘Ninaenda, nami nitakuja tena kwenu.’ Kama mngenipenda, mngeshangilia kwamba ninaenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.
Ile ya Jiwe alivyoitwa kwamba yeye ni Yesu vipi na ile? Au ile ni sawa?!
 
Wakristo sie wapole sana ingekua waislamu muda huu kijana angekua keshaharibiwa sura na vitisho kibao vya kusomewa albadir.

Domo mpuuzi halafu mdini balaa hapo ndipo kaonyesha rangi yake halisi.
Ile ya Jiwe alivyoitwa kwamba yeye ni Yesu vipi na ile? Au ile ni sawa?!
 
Wakristo wenyewe wameshajidharau na kumfanya Yesu wao adharaulike. Ndio maana Diamond anaweza kutunga mashairi ya kumkejeli Yesu. Tena Diamond ameiga tu, aliyeanza kutoa hizo dharau ni Kangi Lugola alipomfananisha Magufuli na Yesu, na viongozi wakubwa wa dini ya kikristo wakakaa kimya huku wakimshangilia Magufuli na kumsifia ovyo ovyo. Sasa tuwaache wakristo wavune walichopanda. Yote haya ni mafanikio ya uongozi wa awamu ya tano!

Heshima ya Yesu italetwa na wale wanaomwamini, na itapotezwa na hao hao wanaomwamini.

CCM oyeee!
Magufuli oyeee!
Diamond oyeee!
Unaongea kishabiki, kangi alikemewa kwa maneno yake embu uwe mtu wa kuchunguza ndio unaongea sio unaropoka tu
 
Back
Top Bottom