[emoji1787][emoji1787][emoji1787]msamehe bure. kwa kuwa anaishi marekani basi anadhani kila atakacho zungumza kuhusu maceleb wa kimarekani kitakuwa genuine na tutakiamini.
mtu kama Nas avae cheni mdosho kwasababu za kijinga eti symbolic!!?....ku symbolize nini?.
hapana aise, babu Kiranga umetulisha tango pori. najua sio kosa lako,kosa lako ni umri. umri umesonga huo mzee, ndio maana umetaja watu wa generation yako ikina LL Cool J, Slick Rick, Big Daddy Kane, Heavy D.[emoji1787][emoji1787]
mijadala mingine ipotezee, waachie vijana.[emoji1787][emoji1787]
Inategemea na unaongelea nani.Si muumini wa fake jewelry au vito kwa ujumla lakini swali langu kwako kama wanaweza tundika vito fake inakuwaje kwenye magari waliyo nayo?
Baada ya kumsagia kunguni akose tuzo, sasa mnamsagia kunguni ili afe kwa kisutwa kizaramoAkiwa Marekani baada ya kukosa tuzo BET sadala katua studio kwa swizzbeats ambako sijui ana project gani, ila katika picha kaposti kwa insta ameonekana kachafua shingo na mikono kwa lundo la macheni, mapete na masaa ambayo wataalamu wa mambo ya vito vya thamani wa instagram yaani @fakewatchbusters wamethinisha kuwa ni feki na hazijawahi kutengenezwa na watengenezaji OG.
Ukiangalia kwa upande wa swizzbeats yeye kavaa simple tu bila lundo la mishanga kwani kavaa saa ya kijani aina ya Richard Mille RM 52-06 Green Emerald “Mask” Tourbillon Yenye thamani ya USD $2,500,000 ambazo kama TSHS Billioni 5,779,035,000 za kitanzania.
Kama kawaida kunya anye kuku akinya bata kaharisha. Mwacheni sadala aenjoy kama kimasomaso keshawatoa!nampongeza sana kwa hatua za kukutana na huyo mtaaalamu anayeheshimika duniani....hata mchizi DMX ameenda kaburini huku akimheshimu huyo jamaa. hits zake zote zilizohit vibaya dunia nzima huyo ndo mtengezaji.
alichoninikera diamond (najua hainihusu lkn nasema tu);
1. uvaaji wa micheni usiokuwa na maana kwa sasa naona kama umepitwa na wakati.....watu wanakuwa simple tu. ukifanya hivyo unaonekana kama mshamba flani hivi.
2. pozi zinazosema 'nioneni'. ukiwaangalia hao wawili unaona kabisa pozi yake diamond ni ya kuchamba, yaani ni pozi ya mswahili. huyo swizz beats anaonekana yuko relaxed, yuko real...
Inategemea na unaongelea nani.
Kuna watu wengi kwenye hip hop wanatumia magari ya kukodi.
Pia, mimi sisemi kwamba hip hop stars hawana hela za kununua magari au vito vya thamani.
Nasema kwamba, kwenye hip hop mtu kuvaa fake gold si kitu cha ajabu, hawa big stars wote ama at one point wamevaa, ama bado wanavaa.
Kuna mi chain fulani ukiiangalia unaona kabisa hii ni gold plated, kwa sababu ingekuwa real gold ingekuwa mizito sana.
Do Rappers Wear Fake Jewelry? (Interesting Discovery in 2024)
In trying to keep up, most rappers end up buying and wearing fake jewelry. Some even go to the extent of renting out the flashy jewelry just to look the part.www.afashionblog.com
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Waswahili wanasema "Kikulacho ki nguoni mwako".Shida yetu tunashadadia kila kitu kikifanywa na wanyamwezi! Mwenzetu akijaribu hatutaki, tunona kakosea au tunaona wivu.
View attachment 1843839
Kweli kabisaInategemea na unaongelea nani.
Kuna watu wengi kwenye hip hop wanatumia magari ya kukodi.
Pia, mimi sisemi kwamba hip hop stars hawana hela za kununua magari au vito vya thamani.
Nasema kwamba, kwenye hip hop mtu kuvaa fake gold si kitu cha ajabu, hawa big stars wote ama at one point wamevaa, ama bado wanavaa.
Kuna mi chain fulani ukiiangalia unaona kabisa hii ni gold plated, kwa sababu ingekuwa real gold ingekuwa mizito sana.
Do Rappers Wear Fake Jewelry? (Interesting Discovery in 2024)
In trying to keep up, most rappers end up buying and wearing fake jewelry. Some even go to the extent of renting out the flashy jewelry just to look the part.www.afashionblog.com
Ahahahahha
Tatizo fekiKama kawaida kunya anye kuku akinya bata kaharisha. Mwacheni sadala aenjoy kama kimasomaso keshawatoa!
Haya kuhusu hayo macheni kwenye ile clip ya studio ya busta rhymes iangalie vizuri kuna yule 'hitmaka' aliyechezesha mzigo wa macheni. Sasa niambie kati ya yule na sadala nani kavaa macheni mengi? Ila kwa yule sawa tu!
Shida meko na makondaWaswahili wanasema "Kikulacho ki nguoni mwako".
Waingereza wanasema "Familiarity breeds contempt".
Ukimjua sana mtu, unapoteza kumheshimu.Na watu wa karibu ndio wanaoleta matatizo.
Watu wa nje ya Tanzania wanamzimikia sana Diamond kuliko wabongo, pengine hawamsomi sana kwenye magazeti yao kila siku.
Sasa hao Wanyamwezi hatuwajui vizuri, huyu mtoto wa Tandale tumemuona tangu anakua tunamjua vizuri, kwa hivyo heshima inapungua kidogo.
Wala sio mtaji ml3.7 kwenda UsaMwenzio yupo US wewe upo insta hamuoni kwamba mnatakiwa kupimwa akili? Nauli ya kwenda na kurudi tu US kwenu ni mtaji. Wabongo tafuteni shughuli ya kufanya kuliko kufuatilia maisha y watu
Mondi namkubali ila hayo mapete... hapana.Hata zikiwa OG ukivaa mingi hvo mm ntakuona ww ni msambaa tu