Diamond platnumz na Kasimu mganga nani mkali wa nyimbo za mapenzi?

Diamond platnumz na Kasimu mganga nani mkali wa nyimbo za mapenzi?

Kwa wale wapenzi wa nyimbo za mapenzi watakubaliana na mimi kwa 100% kwamba kwa hapa Tanzania ukitaka kusikiliza nyimbo kali za mapenzi zenye kubembeleza,kuliwaza,kufariji na kusuuza moyo basi sikiliza nyimbo za hawa magwiji wawili ambao ni Kassimu Hemed au Kasimu Mganga na Naseeb Abdul au Diamond Platnumz .

Kila mmoja kwa wakati wake amekuwa akitamba kwamba yeye ndio fundi au tajiri wa nyimbo za mahaba

Kassimu kwa upande wake amesumbua na ngoma kali kama vile Awena ,Usiende kwa Mganga ,Subira aliyomshirikisha king of the best melody hapa namzungumzia Christian Bella nk

Kassimu kwa sasa anatamba na ngoma ya Somo aliyowashirikisha Kilimanjaro band (wana njenje ) waliotamba na ngoma yao ya kinyau nyau

Naseeb kwa upande wake ametamba na ngoma kama vile nimpende nani, tatizo kwetu mbagala , lala salama,moyo wangu nk

Kwa sasa Naseeb anatamba na ngoma yake ya marry you aliomshirikisha mwanamuziki Ne-Yo

View attachment 476752

Huyu ni Kassimu Hemed Mganga

View attachment 476753

Huyu ni Diamond Platnumz Simbaaaa

Haya sasa wakuu kazi kwenu nani fundi hapo kwenye upande wa nyimbo za mapenzii tuuu basiiii ?
Jaman jaman... acha kumpambanisha mganga na vitu vya ajabu, huyu level zake at least kina Kiba
 
Kwanza tafuteni asili ya hao watu wawili. Kassimu ni mdigo wa tanga, tanga ukisikia mapenzi huwazungumzii watu wengine ni hao wadigo, sio wake wala waume wote mafundi sana.

Mondi asili yao kigoma, huko hakuna ufundi wowote, mondi ni mjanja wa town tu na ameshika soko la music ila kwa nyimbo za mahaba kassim break.

Tofautisheni mahaba na matusi. Kuna mmoja anaimba mahaba mwengine matusi
 
Umeanza vizuri ila umeharibu mwishoni
 
Nyimbo ya Awena bado haijatokea ya kuifunika upande wa muziki wa mapenzi
 
Napenda nyimbo za Kassim Mganga ila anavyoimba, uvaaji , uchezaji , mapozi na muonekano kwa ujumla kama team Kaoge vile
 
Kassim mganga aisee!
Awena, i love u,hizi ngona hazijawahi kunikifu.
 
ki ukweli wote ni my fevs artists, lakini usifanye mchezo na kassim ktk mashair ya mapenz, we sikiliza nyimbo yake ya manuari tu utaelewa. . . . . just take your time na uisikize hyo nyimbo utaelewa namaanisha nini
Kiukweli hakuna wakumfanisha kassim mganga na mwanamuziki yoyote katika nyimbo za mapenzi, manuari ni nzuri mno but kwangu mimi nafsi nyonge ni balaa.
 
binafsi sijawahi ruhusu device yangu yoyote ile ya music iwe cm,laptop nk ikae bila kuwepo na nyimbo ya manuari...sasa sijui ameimba nani kati ya hao wawili.
 
Kassim Yuko vizuri..ukweli lazima usemwe kinachombeba Mondi ni promo tu...huyu kijana wa Manza Bay ni habari nyingine..
 
Back
Top Bottom