Aah ghafla visenti sina, nimerudi tandale...
Nimeshindwa kulipa bima, nimeuza madale...
Redio nyimbo wamezima, TV ndio hatare....
Nimenyunda limebaki jina, mitaa ya tandale...
Wale shabiki zangu, walionisifu kwa maneno
matamu... Leo maadui zangu, wakitusi tu kwa
instragram... Nikimuona sallam, anasema
hanifahamu... Hata harmonize nikimpigia
ananifokea kama sanamu.... Na magazeti ya
nyumbani kwa kukuza habari si mnajuaga...
Utasikia tafalani eti mond kwa zari
kashamwagwa... Na mi nilivyo mnyonge, tabia ya
kuwajibu sinaga... Kama naiona michambo ya
madem wa zamani niliowakazaga.... Ninayosema
yana maana, kwani hakuna hajuaye kesho...
Anayepanga ni rabana hila ameificha ni
confidential.... Ukisali omba sana, mumeo nisije
kuwa kichekesho... Mara rafiki wa jana, ndio adui
mkubwa kesho... La lala lala la je utanipendaga,
la lala lala la au nawe utanimwaga???