Diamond Platnumz: Niliibiwa Tsh. Bilioni 4 niliyotaka kununulia ndege

Mimi nakuelewa, ndio maana siwezi kufanya deal ya kizembe.
 
Labda ndio kutengana na Salam SK inawezekana aliwapiga wenzake japo kiasi inawezekana ikiwa kick ya festival yake kuongeza zero. Tunajuwa mambo ya ndege yalikuwa chini SK kwa maana kina Babu Tale lugha ilikuwa shida sasa kuna uwezekano mkubwa SK alihusika kama yeye au aliingizwa mjini.
 
mwambieni apunguze sembe, sisi sio watoto wadogo atudanganye mchana ivo.
 
Ukisoma comment humu watu wanabisha na sijaelewa kabisa. Diamond hana hicho kiasi cha pesa au Diamond hawezi kutapeliwa?

Mkuu namimi nimejiuliza kama wewe

Unajua shida yatu ni hii

Mosi tumezoea kudanganya kwa kuongeza sifuri mbele haswa maselebriti wetu

Pili tulio wengi ni masikini na hatuamini kama Mtz kama Domo anaweza kuwa na mahela mengi kiasi hicho
 
Mkuu namimi nimejiuliza kama wewe

Unajua shida yatu ni hii

Mosi tumezoea kudanganya kwa kuongeza sifuri mbele haswa maselebriti wetu

Pili tulio wengi ni masikini na hatuamini kama Mtz kama Domo anaweza kuwa na mahela mengi kiasi hicho
Kuna jamaa juu kasema wabongo habari kama hii hawaamini ila wakiambiwa jamaa anatumia unga wanaamini
 
[emoji23][emoji23][emoji23]..labda billioni4 za Haiti
Dah Billion 4 ni hela ambayo anao uwezo wa kumiliki mbona? japo siyo hela ndogo ila wafanya biashara kibao account zao zinasoma B+, zamani nilikua naona Billion ni kitu cha ajabu sana mtu kumiliki lakin kwenye mihangaiko nimekutana na wafanya biashara wenye utajiri huo wengi tu tena wanaishi mikoani huko.

Kwahiyo hata yeye kumiliki anaweza ila kuibiwa ndo sina uhakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…