Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,235
- 4,252
Diamond Platnumz
Diamond Platnumz usibabaishwe na tuzo za BET kwasababu soko la mziki Marekani limeanguka na Wasanii wake hawana mashiko kwa sasa. Mziki mzuri upo Africa kwa sasa ukishikiliwa na nchi ya Nigeria
Wasanii wa Marekani wameanguka sana na soko lao limedorora sana, hawana nyimbo za kueleweka zaidi ya makelele kwenye masikio
Miaka ya 2015 kurudi nyumba kulikuwa na wasanii wazuri na waliburudisha sana hii dunia akiwemo Rihanna, Mariah Carey, Lil Wayne, Rick Ross, Snop Doggy na wengineo
Miaka ilipozidi kusonga hadi sasa soko lao la mziki limekuwa likizidi kuanguka kwasababu ya kukosa wasanii wenye vipaji na kuishia kutupigia kelele
Miaka ya nyuma hata tuzo za BET zilikuwa na hadhi kubwa sana lakini sasa hazina thamani tena
Nimekuwa nikifuatilia BET Awards tangu 2010 mpaka sasa naweza kusema kuwa hakuna event mbaya kuwahi kutokea kama BET Awards ya 2024
Yaani imepoa kama kono
Wasanii hawana nyimbo nzuri tena zaidi ya makelele ndiyo maana nina kila sababu ya kusema Diamond Platnumz usibabaishwe tena na hizi tuzo
Piga kazi tupo nyuma yako, achana na haya Makapuku ya BET