Diamond Platnumz usibabaishwe na tuzo za BET kwasababu soko la mziki Marekani limeanguka na Wasanii wake hawana mashiko kwa sasa

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
1719862682165.png

Diamond Platnumz

Diamond Platnumz usibabaishwe na tuzo za BET kwasababu soko la mziki Marekani limeanguka na Wasanii wake hawana mashiko kwa sasa. Mziki mzuri upo Africa kwa sasa ukishikiliwa na nchi ya Nigeria

Wasanii wa Marekani wameanguka sana na soko lao limedorora sana, hawana nyimbo za kueleweka zaidi ya makelele kwenye masikio

Miaka ya 2015 kurudi nyumba kulikuwa na wasanii wazuri na waliburudisha sana hii dunia akiwemo Rihanna, Mariah Carey, Lil Wayne, Rick Ross, Snop Doggy na wengineo

Miaka ilipozidi kusonga hadi sasa soko lao la mziki limekuwa likizidi kuanguka kwasababu ya kukosa wasanii wenye vipaji na kuishia kutupigia kelele

Miaka ya nyuma hata tuzo za BET zilikuwa na hadhi kubwa sana lakini sasa hazina thamani tena

Nimekuwa nikifuatilia BET Awards tangu 2010 mpaka sasa naweza kusema kuwa hakuna event mbaya kuwahi kutokea kama BET Awards ya 2024
Yaani imepoa kama kono

Wasanii hawana nyimbo nzuri tena zaidi ya makelele ndiyo maana nina kila sababu ya kusema Diamond Platnumz usibabaishwe tena na hizi tuzo

Piga kazi tupo nyuma yako, achana na haya Makapuku ya BET
 
Hebu wataje hao wasanii wa kizazi cha sasa ambao wewe unasema wana makelele tu,

Kwahiyo sasa hivi soko la mziki lipo nchi gani?
Mi nadhani umri wa mtoa mada umesogea ile era aliyekuepo imesogea...sawa na sasa wanasema bongo fleva sio nzuri kuliko 2010 kurudi nyuma ukichunguza wanaosema hivyo ni nani unakuta wale waliozaliwa 1980s
 
Soko la mziki Marekani kwasasa halina mashiko, limejaa Wasanii wenye makelele hawana vipaji, Wasanii walikua kizazi cha Rihanna hiki cha sasa hakina jipya
Usilazimishe kila mtu akubaliane na ww, huo ni mtazamo wako na yy katoa maoni yake. Be humble.
 
Marekani sasa hivi inainamishwa na Nigeria
Mkuu, ingekuwa hivyo basi wamarekani wangekuwa bsy kutaka kufanya collabo na wanaija ila ukweli ni kwamaba wanaija ndio wanafanya collabo la Wamarekani na ndio maana bado akina Tylor Swift ndio wanamuziki matajiri zaidi. Yani huenda ukianza kutaja list ya wasanii wanaoingiza pesa ndefu unaweza hata fikisha 50 hata mnaija hajaingia mmoja.
List za wanamuziki wanaoingiza pesa tukianza kuzitaja tunataja za kwetu za Afrika sio za world wide.
Kuhusu diamond kwenda international, ukiachilia mbali nyimbo ya juzi ambayo baada ya chris kuicheza basi ikawa kama ndio grammy, ila naona siku hizi kama vile alikuwa ameacha kufukuzia kwenda international na alikuwa keshajiweka pembeni na ligi alizokuwa nazo za kwenda sambamba na wanaija.
 
Kipaji na pesa ni vitu viwili tofauti. Wasanii wa USA wana hela hatujakataa namaanisha miaka ya nyuma ndio walikuwa wa moto kizazi cha sasa cha Marekani hakina vipaji ni makelele tu yamewajaa
Kizazi cha sasa ni cha Ice Spice
Ukirudi kwa Rihanna, Justin Bieber na Rick Ross ndo unapata picha ya maana ya kipaji
Naija inawakunja kwa sasa na wala Diamond Platnumz asibabaishwe
 
Mkuu kila zama na watu wake. Hata kuna wanaoona bongo fleva ya sasa hakuna vipaji watu wanaimba melody zinafanana na matusi. Kuna wanaoamini kizazi cha akina professor j na akina jay d ndicho bora.
Mimi kizazi cha muziki wa Marekani ninachokielewa pia ni cha akina Rihanna, Eve E one of my best kwa upande wa akina dada, akina foxy brown, akina Aaliyah, left eye kwa wanaumeakina Jay Z, eminem, T.I, Fabulous, chingy, Ja Rule, Ashanti, ni mara chache mimi kusikiliza nyimbo za US za zama hizi.
So mimi nadhani ni generation fulani kuona hii mpya mbovu lakini muziki mara zotr unabadilika
 
Nikweli mkuu
Wa sasa makelele, wasanii wa kike hawana la kutuonesha zaidi ya kalio zao sijui nani kawambia anataka vyoo vyao
 
Juzi nlikuwa natazama wimbo wa what niggas all want wa Eve E, halafu nasoma comments. Bidada alikuwa kavaa kwa kujistiri halafu anatema bars. Comments watu wanasema hicho kizazi wanawake walikuwa watrend kwa vipaji si mishape. We tazama Miss Eliot na sura ngumu but alikuwa anakinukisha.
 
Back
Top Bottom