Simba wa Muziki barani Afrika
diamondplatnumz amevunja rekodi ya Kufikisha YouTube Views million 1 ndani ya Muda mfupi zaidi iliyokua inashikiriwa na Mwanamuziki
davido Kutoka nchini Nigeria, na Kuandika Rekodi yake mpya kupitia Video ya Hit song yake ya #Waah aliyomshirikisha @koffiolomide_officiel .
Diamond ameweka Rekodi hiyo mpya baada ya Kufikisha Views Milion 1 ndani ya Masaa 8 TU, rekodi ambayo awali ilikua inashikirikwa na
davido ambae alifikisha Views Milion 1 ndani ya Masaa 9 kupitia Video yake ya #FEM .
Rekodi hii inaendelea kudhihirisha ubabe na nguvu kubwa aliyonayo
diamondplatnumz katika Muziki, kwasababu si rahisi wala mzaha kufikia namba za kutisha namna hii !
Mpaka hivi sasa Video ya #Waah ina watazamaji zaidi ya Milioni 1 ikiwa ni Masaa 8 TU tangu iachiwe ..
Source# wasafi tv