Tatizo lako Matola unamuona
Muuza Sura kama Mungu mtu anayejua kila kitu hapa mjini... kwangu mimi yeye hana tofauti yoyote na wewe au yeyote yule anayependa kuji-mix na ma-celebs... !! Hawa watu wangekuwa wanafahamu undani wa watu kama wanvyotaka tuamini basi wangetuletea Breaking News za Zari na Diamond kabla kila kitu hakijakuwa hadharani... kama unakumbuka, hata wewe mwanzoni kabisa ulikuwa unabisha kwamba Diamond alikuwa anatoka na Zari na hata uliponihoji nami nikasema wazi kwamba hata mimi I doubt coz' for what I know Zari ni mpenda mafoto na celebs... hata hivyo nilihitimisha kwa kukueleza kwamba, kwenye mapenzi, kila kitu kinawezekana!
Kwamba Muuza Sura yupo flexible sio kweli hata kidogo... humu jamvini tayari ameshajitanabahisha kwamba yeye ni Team Kiba! Kwamba eti hiyo game Diamond hawezi kushinda ni sawa na dua la kuku... by the way, tukiuliza ni game lipi
Muuza Sura anaweza kutujibu? Au ndo yale yale ya akina Ivan kwamba Diamond kamwe hawezi kuzaa na Zari?? Anyway, hata kama Muuza Sura hapo kabla angeweza kuaminika, alikuja kuharibu pale alipoanza kuchukua upande... angeendelea kubaki neutral basi hoja yako ingekuwa na nguvu sana!!! Lakini yote hayo tuyaache... hivi kabisa ndugu yangu unamaani kwamba huyo Muuza Sura anaweza akawa anafahamu undani wa mimba ya Zari zaidi ya Zari mwenyewe? Let's be serious dude! Huyo MS atakuwa anayafahamu yale tu ambae yeyote anaye-interact na celebs atakuwa anayafahamu lakini usitarajie eti atakuwa anafahamu undani wa mtu kama Zari au Diamond!