Unless kama anatangaza kwa ajili ya kutaka ku-prove kitu coz' hana sababu ya ku-prove kwa yeyote kwa chochote... it's his life awe ana uwezo wa kumpa mimba mwanamke au hana! Lakini ikiwa ametangaza si kwa ajili ya ku-prove chochote na kwa yeyote, binafsi sioni tatizo lolote... Diamond sio mtu wa kwanza na kamwe hatakuwa mtu wa mwisho kutangaza uja uzito wa mwandani wake! Tatizo hapa ni lile lile... kunya anye kuku, akinya bata kaharisha!!
Na hili la kutangaza mademu zake mie nampa big up... hataki unafiki wa wengine! Wasanii karibu wote ni malaya mbwa lakini wanataka kujifanya ni watakatifu mbele ya jamii lakini wanakuja kuumbuka baadae! Sioni sababu ni kwanini mtu ufiche mpenzi wako kama si kwamba unataka uwe unapiga show tofauti tofauti at the same time... wasikilize hata wengine wakati wanahojiwa... wakiulizwa wanatoka na nani, hawasemi kwa sababu wanajua wakisema ni kimbembe... huku kuna X, kule Y upande wa pili kuna Z... atamtaja nani!!! Matokeo yake anaishia kusema "nisingependa kumweka mpenzi wangu hadharani" X akisikia hivyo, anadhani ni yeye, hali kadhalika Y nae anadhani ni yeye na hivyo hivyo kwa Z... yaani tafrani mtindo mmoja!!!