Diamond sasa ni kubadili mafanikio kuwa hela

Diamond sasa ni kubadili mafanikio kuwa hela

Burnaboy

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2019
Posts
1,070
Reaction score
1,439
Diamond amefanya vizuri 2019 hakuna ubishi. Amefanya shows za mafanikio na ameangaliwa zaidi kwenye You Tube kuliko msaanii mwingine yeyote Afrika!!!

Wasanii wa West na South Afrika ambao Mondi kawazidi wanamiliki ukwasi mkubwa, majumba, ndege binafsi....!!!

Sasa kilichobaki ni kubadili mafanikio ya Mondi kuwa hela. Hii likifeli wa kulaumiwa ni menejment ya diamond!!!

Hii menejment sasa inabidi iende hatua mbele zaidi ya kuendeleza uswahili, mabifu yasio na maana na kukazana kuonyesha wanajaza maviwanja wakati msanii wao hajavuna hela na kufaidika inavyotakiwa!!! Mambo ya kujaza maviwanja vya bongo wamwachie konde boy!!!

Mondi angekuwa mganda au mkenya si ajabu muda huu angekuwa na ndege binafsi mbili tatu!!!
 
mkuu unajua thamani ya ndege kweli? au unaongeelea tule twa TANAPA tena za zamani kichizi. lakini kama ni Gulf Stream huenda hata assets na pesa aliyo nayo hawezi nunua
Mkuu nazungumzia ndege za ma star kama kina davido, wizkid au hata jaguar. Vile vya TANAPA vinatikisa sana kuliko vile bora aache tu!!!
 
Uganda,Kenya na Nigeria wana mfumo unao eleweka unao wabeba wasanii wote ktk Industry haubagui na kila mshika dau anajua wajibu wake ni kupromote nakuufikisha mbali mziki.

Kibongo bongo makundi makundi kibao,majungu,vinyongo,visasi,wivu chuki kibao.

Ngumu sana msanii wa bongo hasa asiye kwenye haya makundi kutoboa,Mondi na mngt yake wamejitahidi sana,sababu yy crew yake ina power.

Pili hiyo ndege binafsi sio msanii wa Kenya wala Uganda hamna msanii mwenye ndege,hata Nigeria hayupo mwenye ndege,Ila wanaijeria wanapiga hela kwanza wapo wengi,pili mziki wao hauna mateam na mashabiki wao hawaja gawanyika na wana upenda mziki wao na ndio maana Itunes,Sportfy,Shazam,Tidal wanakimbiza wao na huko ndio kwenye hela kuliko Youtube.Jaguar ana ndege sababu ni mfanya biashara mkubwa wa magari.

Sisi mashabiki wa bongo kwanza kuna mateam,msanii kama sio wa timu yako humsapoti,pili Mashabiki wa bongo wengi wanafiki kwani sio wanunuaji wa nyimbo online wengi tuna msubiria kideboy,bekaboy aweke nyimbo kwenye website yake tupakue.Hatuna utamaduni wa kununua nyimbo online.Leo hii kama tungekuwa kweli tunawasapoti wasanii wetu Online basi Mkito na Mdundo zisingekufa.

Vyombo vya habari kila mtu na msanii wake,kila mtangazaji na msanii wake,kuanzie watangazaji,redio nazo zipo kwenye hizi timu.So mpaka unamwona Diamond hapo ,yy na mngt wamepambana sana,kuna uwezekano mwakani Mondi akalimaliza bara lote la Africa (ukitoa inchi za kiarabu) ,kwani kishapiga show 90% ya nchi zote za Africa ,mwakani ana show Gambia,Gunea konakry na Liberia zote comfermed.

Industry yetu wasanii wengi wana fail kutoboa,sababu hamna UPENDO.
Angalia Nijeria Wizkid kagombana na Davido yameisha,Yemi Alade kagombana na Tiwa hata kabla mwaka hujaisha yameisha na mwaka jana msimu wa christmas Tiwa alikuwa na show,Yemi akasapoti,Don Jazzy na Olamide walikuwa na Beef 2016 hata mwaka haujaisha yakaisha na wasanii walio kuwa chini ya Olamide na Donny Jazz wakaanza kushirikiana.Hio haitoshi wakati MTV inaanza playlist kwa asilimia kubwa walikuwa wasouth,wanaijeria baada ya kuingia MTV wameleta fitina leo hii playlist ya MTV wana dominate wao turn,Trace napo hivyo hivyo hata channel O mwishoni walikuwa wana tawala wao.

Cha msingi Mondi aje na Content zitakazo zivutia nchi nyingi za nje hasa za ulaya kwani wenzetu wanasupport sana wasanii,pili afikirie kutoa album nyingine kwani kuna tuzo nyingine mfano BET,wanazitazama sana hizi albums na mngt ijitahidi kutafuta deals nyingi zaidi kwenye makampuni makubwa huko ndipo kuna hela.
 
Mkuu nazungumzia ndege za ma star kama kina davido, wizkid au hata jaguar. Vile vya TANAPA vinatikisa sana kuliko vile bora aache tu!!!
hahaha ya jaguar huwezi kuitaa ndege ya kistar haija tofautiana na ya tanapa, davito hivi ana private jet? Mkuu wenye ndege hata wasanii wa Marekani wanaomiliki ndege wanahesabika. Kuna ndege na vijidege yani hata ukikapanda inakuwa kama umekaa kwenye beseni
 
hahaha ya jaguar huwezi kuitaa ndege ya kistar haija tofautiana na ya tanapa, davito hivi ana private jet? Mkuu wenye ndege hata wasanii wa Marekani wanaomiliki ndege wanahesabika. Kuna ndege na vijidege yani hata ukikapanda inakuwa kama umekaa kwenye beseni
Davido anayo nzuri tu ndio kaenda nayo ghana juzi hapa. Hivi ile ya jaguar aliotua nayo dar siku za nyuma mbona si haba? Au niliona picha vibaya?.hata hivyo nachosema wamwezeshe diamond kupata hela zaidi asiingie kwenye historia ya kuwa na umaarufu usioendana na kipato
 
Cha msingi Mondi aje na Content zitakazo zivutia nchi nyingi za nje hasa za ulaya kwani wenzetu wanasupport sana wasanii,pili afikirie kutoa album nyingine kwani kuna tuzo nyingine mfano BET,wanazitazama sana hizi albums na mngt ijitahidi kutafuta deals nyingi zaidi kwenye makampuni makubwa huko ndipo kuna hela.

Mkuu umelenga mia kwa mia kwenye uhalisia wa mambo. Kutokana na zengwe zilizoko bongo mondi angejitahidi kujipanua nje kibiashara hasa kwenye udhamini.
Amekaa na Bellaire muda sasa wakati angeweza kupata brands nyingine zinazoweza kuuza kwa jina lake. Hizi brand za kibongo sidhani kama zinalipa vizuri!! Sasa menejment yake ijikite kwenye shoo na udhamini wa nje.
Waachane na uswahili wa kutupiana maneno na kina kiba na konde boy.
 
Back
Top Bottom