Diamond sasa ni kubadili mafanikio kuwa hela

Diamond sasa ni kubadili mafanikio kuwa hela

Screenshot_20200105-112036.png

Screenshot_20200105-112420.png
 
Hiv kwann na sisi watz tuamue kuwapemda wasanii wetu bila kiwabagua kama tunavofanya miaka mingi iliyopita!!?? [emoji848] Au tuna subir mpaka wafe ndo tujue kuwa walikuww na thamani kubwa kwa nchi!!?? [emoji848] Michezo mingi hata haijawahi kutupaisha kimataifa ila mziki wa bongo flava kwa kweli hasa diamond kajitaaidi sana kwann tusimpe support ya kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
Wabongo wanamtaka Mond au Kiba lakini hawataki tuwe na Kiba au Mond wawili~ Fid Q.

Wabongo tunapenda kitu kimoja tu kizuri, siku kikitokea kingine kizuri tunaanza kukishindanisha na kizuri cha zamani na hatimae kukipoteza kimoja wapo.

Angalia mfano hata sasa hivi, Harmonize amavyoshindanishwa na Mond huku wengi wengi wakitaka mmoja apotee kabisa.

Ni kama ugonjwa fulani hivi ambao uko so chronic

Mi sina ugomvi kwenye wasanii wazuri kuongezeka. Ugomvi wangu upo kwenye kuiga sababu hii itafanya mmoja wapo au wote wawili wanaoigana wakwame kisanaa!!!

Na hapa mwenye tatizo ni kondeboy anaiga kila kitu kwa mondi!!! Kuanzia mziki hadi swagga!!!

Ukiangalia ali kiba, rayvanny wanajitofautisha na mondi. Vile ukiangalia watu kama davido, wizkid na 2face wana utofauti kila mmoja analeta chake kwenye gem fani inakua.
 
Mkuu ile ndege ya Davido nimesoma pahali bei yake kwa used ambayo ishatumika mtu anakuuzia haipungui Billion 30 za Tz...Davido anaweza afford kweli hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Neymar Jr. anamiliki ndege ambayo ni USD 13.5M. Davido kumiliki ndege sidhani ingawa wiki hii alimpa lift ex wake kwenda Ghana. Labda awe na akili za kibongo ambapo gari linakuwa na thamani ya 57% ya assets zote alizonazo kijana.
 
Mond is business mogul not just a musician.

Sio tu kwamba ana kipaji cha muziki bali pia jamaa ana kipaji/uwezo mkubwa wa kibiashara.

Nahisi hata wafanyabiashara wakubwa baadhi wanamfuataga kuomba ushauri.

Ni watu wachache sana dunia hii wenye uwezo wa ku commercialize talanta zao kutoka kwenye mazingira magumu na kupata mafanikio kiasi cha kwenda sawa na wale waliotoka kwenye mazingira rahisi na wezeshi.

Kwa industry yetu ilivyokuwa milongo miwili iliyopita ilikuwa ni ngumu sana kudhani kuna siku na sisi tutakuja kuwa na msanii ambaye ni brand kubwa afrika, kutokana na aina ya mziki wetu,lugha,popularity ndogo ya nchi yetu,kutokuwepo kwa watangulizi,support mbovu ya serikali,amateurish media industry,roho za wabongo.

Lakini leo hii hayo yote yameonekana si vikwazo kwa mtoto wa tandale, he has beaten all the odds and now he is on top of the game, he has shown the rest of us nothing is impossible if you put genuine efforts to pursue it, he owns this industry,he has transformed the mainstream genre to his own stylish rhythm, sasa hivi kila ngoma kali unayoiskia unakuta ina vionjo vya Wcb kwa mbali.

Kiukweli huyu mtu tunaweza tukawa hatufurahishwi na personal life aliyonayo lakini kwenye suala kazi tunamuangalia kwa jicho la kufarishwa naye na la kujifunza pia.

MOND BABA LAO.[emoji441][emoji441]

Sent using Jamii Forums mobile app
Bakhera , Mo, Kishimba, wakamuombe ushauri Diamond ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vile hata siyo vijet ni turbo propellar makelele kibao not comfortable we jet mchezo, hata hao psquare hawana na nina mashaka hata huyo davido kama anamiliki jet. Hivi jet unaijua unaiskia mzee baba
Davido ana back up ya dingi yake ni bilionea mkubwa sana Huko Nigeria .

Ukimfananisha mondi na davido utakuwa unamwonea mondi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Davido ana back up ya dingi yake ni bilionea mkubwa sana Huko Nigeria .

Ukimfananisha mondi na davido utakuwa unamwonea mondi

Sent using Jamii Forums mobile app
That is what I mean,kwapesayake yeye kama yeye hana uwezo wa kununua ile jet maana inacost pesa nyingi kuliko hata utajiri alionao yeye binafsi. Ile jet ni ya baba yake so akipewa au kusaidiwa na baba yake that is another case haitakuwa imetokana na mziki wake
 
Neymar Jr. anamiliki ndege ambayo ni USD 13.5M. Davido kumiliki ndege sidhani ingawa wiki hii alimpa lift ex wake kwenda Ghana. Labda awe na akili za kibongo ambapo gari linakuwa na thamani ya 57% ya assets zote alizonazo kijana.
😂😂😂
Ila mondi anazimikia Rolls Royce.
Avute basi Rolls Royce Phantom!!!
 
Mi sina ugomvi kwenye wasanii wazuri kuongezeka. Ugomvi wangu upo kwenye kuiga sababu hii itafanya mmoja wapo au wote wawili wanaoigana wakwame kisanaa!!!

Na hapa mwenye tatizo ni kondeboy anaiga kila kitu kwa mondi!!! Kuanzia mziki hadi swagga!!!

Ukiangalia ali kiba, rayvanny wanajitofautisha na mondi. Vile ukiangalia watu kama davido, wizkid na 2face wana utofauti kila mmoja analeta chake kwenye gem fani inakua.
Hapo kwa konde boy kuiga kweli anastahili kubadilika.... maana yeye mwenyewe anonekana hana stylistical rhythm ya kwake mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hili unaliamini ww
Mfano mimi ni shabiki wa Diamond ila my favourite station radio ni Clouds
Na bado kiba namkubali ila tunapopishana na kuona kwamba shabiki wa Dia ni adui wa Alli ni pale tunapoanza ubishani wa n nan bora kiliko ko hapo wengi wanachukulia n kama uadui same to football shabiki wa messi na Ronaldo shabiki wa Ronaldo anajua ubora wa messi na shabiki wa messi anajua ubora wa cr7 ila anawake bora kuliko
Katika football ni tofauti kidogo herman joshua kwa sababu wao kwenye football ni rahisi kukuta ronaldo na messi wakikumbatiana na kuchela hata kwa sekunde kadhaa, na huwezi kukuta ronaldo anatoa maneno makali yanayo mlenga messi moja kwa moja ila hawa wasanii wetu ni kawaida sana mara waambiane mashoga mara huyu kamuibia penseli mwenzie yaani mambo ni taflani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hajui hata naloandika huyu jamaa ndege thamani yake 27 million dollars davido net worth 2020 according to fores ni 16 million dollars sasa anaweza mortgage vipi hiyo ndege?

Mkuu ushawahi kujiuliza Forbes huwa wananufaika vipi na hicho wanachokifanya?

Mkono mtupu haulambwi..hizo takwimu huwa wanapika. Wanachofanya ni kumfuata mhusika (inategemea na image ya muhusika kwa jamii) wananegotiate. Au muhusika kuwafuata forbes then wanapika mambo. Forbes ni wafanyabiashara wajanjajanja tu🤣🤣🤣🤣.

Takwimu huwa zinakuwa ni za makadirio ya juu juu tu. Kuna wajuba wana hela zile za urithi walizikuta toka vizazi na vizazi, lakini hata forbes hawajawahi kutokea. Wao ni kuamka na kucheza tu karata asubuhi huku wakitoa donation kwa watu wa UN.

Maisha haya bwana hayana usawa kabisa😁😁😁
 
Sasa kati yako na forbes nimuamini nani? Atleast forbes ni source ya kuaminika. Unaweza leta ushaidi wa hizi allegation zako?
 
Sasa kati yako na forbes nimuamini nani? Atleast forbes ni source ya kuaminika. Unaweza leta ushaidi wa hizi allegation zako?
Forbes ni wafanyabiashara pia...huwa wanatetea ugali wao kwa style hio. Jaribu tu kufikiria kwa akili ya kawaida utapata jibu haina haja ya kleta ushahidi hapa mkuu
 
Forbes ni wafanyabiashara pia...huwa wanatetea ugali wao kwa style hio. Jaribu tu kufikiria kwa akili ya kawaida utapata jibu haina haja ya kleta ushahidi hapa mkuu
Forbes ni reliable source wamekuwa wakifanya hiyo kazi kwa miaka nenda rudi na ni source inayotumika kama reference ya utajiri wa mtu dunia nzima kuanzia masheik wa middleeast, wafanyabiashara mpaka wafalme.
Sema kwa forbes ya africa naweza kukuelewa si kwamba wanachukua hongo ila kwa africa ni vigumu sana kujua utajiri halisi wa mtu maana afrika mambo yanafichika fichika watu sometimes hawaweki wazi biashara na mali walizo nazo kwakuwa hawakuzipata kihalali na hawataki kulipa kodi.
na forbes afrika nasikia inajitegemea
 
Hawafanyi kazi bure...maslahi/hongo ni lazima ndio point yangu hio mkuu. Hongo ndio hupindisha ukweli...
 
Back
Top Bottom