Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Kwa nini Diamond ndio amuache zuchu na sio Zuchu amuache Diamond.
Power imbalance. Hii concept inawasumbua sana wabongo kuelewa sababu ya lack of exposure na elimu.
Ni vigumu sana mtu aliye chini yako kikazi kukataa mahusiano na wewe wakati unaweza mbananisha kwenye maslahi yake. Inawezekana zuchu anagoma na nasikia alitoa waraka na kusema yeye na Mondi wameachana ila akafuta the very next day. Nani anajua alitishiwa nini? Mondi ni boss wa Zuchu, Mondi anaweza kusema sikulipi stahiki zako unataka zuchu akale wapi?
Boss anaweza kuwa mwananmke na akambana mwanaume hivyo hivyo, umewahi kusikia houseboy kakataa mahusiano na mama house hata siku moja? Unadhani wote wanapenda?
Ni dhahiri mondi anatumia position yake kuwabana hawa warembo; hii pisi leo ilikua video vixxen kwenye video ya mondi, in other words, mfanyakazi wake temporarily ila akaishia kupita nae. Hiyo tu ni ushahidi tosha kwamba anatumia nafasi yake kama fimbo. Sitashangaa vixxens wengine wakijitokeza na kudai mondi alipita nao wakiwa mazingira ya kazi.
Jisomee: "if there is a power imbalance leading to potential for coercion or creating a hostile work environment, which could be considered sexual harassment or discrimination under employment laws; most companies have policies discouraging relationships between supervisors and their direct reports"