Diamond: TRA wananifanya kama mkimbizi

Mkuu kwani umemuelewa kijana yeye hajapinga suala zima la kulipa na amesema ni mlipaji mzuri wa kodi anacholalamikia ni namna njia wanayotumia TRA kuvamia ofisi as if yeye ni kibaka
Kwan manzese uswahilini TRA hawafiki?
 
CCM wanataka kuchukua mamilioni waliyokulipa wewe Diamond wakati walipokutumia kwenye kampeni za 2020 maana wanajua hukuwasidia kitu chochote kushinda maana walipora na kunyakua ushindi kwa nguvu wakitumia polisi-CCM, usalama wa taifa, jeshi-JWTZ, magereza, tume ya uchaguzi, jeshi la uhamiaji nk
 
Walimuita Magu shetani hoa kima. Wacha wajambe sasa tena huu ndio wakati mzuri wa kusema mama anaupiga mwingi.
 
Aiseee. Wengine tukajuwa kuhodhi macheni ya 500m/= na kujigamba nayo basi hata TRA wakileta zao siyo issue?!
Analalamika kama sisi?! Kumbe kabwela tu Diamond. Kujimwambafayi kumbe hamna kitu.
Maisha ya social media fake sana sana aise
Jamaa ameminywa kidogo kende kelele kibao pesa yenyewe mil 700 kama dola 300 hv. Kwa ukubwa wa jina lake na kiasi cha pesa haviendani dogo kabwela huyu. Wangekuwa wamemkamatia B7 hapo ningeelewa.
 
Nenda kazungumze nao na usipige kelele mitandaoni hauwezi kusaidika. Kile kipini cha pua umelipia Kodi kweli , jitahidi uende nacho watakuhurumia kwa kweli
 
Jamaa ameminywa kidogo kende kelele kibao pesa yenyewe mil 700 kama dola 300 hv. Kwa ukubwa wa jina lake na kiasi cha pesa haviendani dogo kabwela huyu. Wangekuwa wamemkamatia B7 hapo ningeelewa.
Wewe hiyo hela umewahi hata kushika
 
Wewe kula kulala ndio maana unaponda jitihada za mtu mwingine ungekuwa ni mtafutaji usingeongea maneno kama hayo
Kila mtu ni mtafutaji humu,
Asake wa Tandale anatakiwa aachane na machawa afanye Kuajiri Tax Consaltants wafanye kazi kitaalam. Biashara sio kupiga manyanga.
 
Pasipokujua hiki kikombe wafanyabiashara wote tunanywea....tatizo ujuaji mwingi...hapo unakuta kawazingua sana maofisa, tena huyu atakuwa yule wa "hapa hawalambi hata kumi"
Ngoja yakukute ndio utatia akili
 
Ngoja yakukute ndio utatia akili
Kwamba unadhani hayajanikuta au ni mapya kwangu?nikikuwekea mikeka yangu ya huko TRA inayosubiria hizi sikukuu ziishe ungekufa kwa presha, kodi zinaumiza siku zote hamna mtu ambaye anazipenda, ila ndio sheria lazima ifuatwe...wembe ninaonyolewa nao ndio huo huo unawanyoa wafanyakazi serikalini, sekta binafsi na unatakiwa ukunyoe wewe na diamond platnumz pia
 
Sio wewe tu acha kujiona upo peke yako, ni kuwa wengi hawapendi kukimbilia kuonewa huruma kwa kulalamika kwenye vyombo vya habari, lipa kodi zinavyostahili na uwe muwazi, onyesha risiti za VAT za matumizi yako kutokana na kandarasi ulizotolea malipo ya VAT. Kuna wengine wamelalamika humu hawa wanaomiliki vituo vya mafuta na changamoto wanazopata za kupigwa faini na kufungiwa akaunti zao wakati tatizo ni za mashine ya risiti kuwa zinaharibika. Domo umezidi kulialia, kila siku unalalamika kuonewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…