Diamond: TRA wananifanya kama mkimbizi

Diamond: TRA wananifanya kama mkimbizi

Akili ya kimasikini huwa inafikiria tajiri kapata hela kwa njia isiyo halali na siku akisikia mwenye hela amepata matatizo basi masikini hufurahi kiasi kwamba itampunguzia ugumu wa maisha.
Sina hela wala mali ila akili za kimasikini sina ndicho najivunia.
Yes , stay positive always
 
Aendelee kukatia mauno CCM. He is having a taste of his own medicine. Kwani wakereketwa na wanachama wa chama tawala na wao wanalalamika 'barabarani' kama wapinzani? Si akalalamike ndani ya vikao vya chama huko?

Kwa afrika hii sio rahisi uwe tajiri au umiliki ukwasi mwingi bila kuwa chawa wa Serikali.

Vinginevyo hufiki popote
 
Kwa vile mimi nina kampuni, wengi wa wafanyabiashara wadogo walioshika pesa ndefu kwa bahati, vipaji na mambo fulani, are not tax compliance, hao mameneja wao ni mameneja sio mameneja lolote, chochote, ni ma promota tuu!, Wasafi lazima aajiri Tax Consultant, amsaidie kwenye tax compliance, haya mambo ya e- filling yanahitaji umakini mkubwa!.

Diamond Platinumz na Wasafi media lazima alipe kodi stahiki kwa kila mapato halali anayoingiza, asitafute visingizio na kutafuta huruma kwenye mitandao ya jamii!.

TRA wako very right kumfungia accounts, ukiona hivyo ujue alitumiwa reminder kibao za kodi atapuuzia, leo ndio tarehe ya mwisho ya TRA kufunga mwaka wa kikodi, hivyo akalipe tuu kodi zetu zote na accounts zinafunguliwa leo leo.
P
Umesema kweli. Kama anataka aajiri Accountants wabobezi na Tax consultants wakueleweka. Sio kuzungukwa na machawa kina Mwijaku na baba levo au mama yake! Atakwama

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kabisa Mkuu ,US hawana mchezo ukikwepa kodi,Hao kina sinza ni Misukule ya Dainamo ,inalipwa inavyomtetea Boss wao humu ,Dainamo anapata pesa lakini halipi kodi kabisa ,TRA wamemminya Makende anaanza kulia lia wakati huku sie Apeche alolo tunalipa kodi..
Halafu wanaomtetea wanashindwa kujua kuwa hizo ni hela wanazompa na kila mapato lazima yalipe kodi.


Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
"shetani Hana rafiki"
Mwisho wa kunukuu
 
Awaache TRA wamkague, nyie si ndio mnaliaga eti mama anakopa, Sasa mama ameamua kukusanya.

TRA wanatembea mpaka manzese, kwenye maduka, yeye nani asitembelewe?

Na anajua kwamba serikali imeshajua kitu katika makampuni yake. Don't mess na Serikali inapokuwa kazini
Si mlikuwa mnasifu Samia kuwa anadai kodi kwa staa,akagui na ku funga account za watu kama Magufuli, Sasahivi Diamond analalamika mnaanza kusema alikuwa anakwepa kodi.Samia alisema Magufuli alikuwa anawanyanganya watu ela yao kupitia tra,sasa mbona naye anafanya hayo hayo.
 
View attachment 2463774

“Kuna wakati sipendi kuongea ila TRA wamekaa kama wanataka kuiua WASAFI, sio sawa nadhani viongozi waliangalie hii kwa namna nyingine.”

“Kama juzi account zangu zote zilishikiliwa bila hata sababu maalumu inaumiza,” Diamond.

Pia soma;

TRA: Taarifa kuhusu madai ya Diamond Platnumz kwa TRA
Kwa hiyo kujiliza mitandaoni ndo utasamehewa?
Kila siku tunaambiwa shule ni muhimu, ninyi munaamini pesa hupatikana hata bila shule! Ndiyo sasa utaweza kuilinda bila watu wenye shule? Ajiri watu wenye shule wakuelekeze uhusiano wako na serikali. Hakuna ushabiki na mihemuko hapa! Waulize akina Messy wanaishije?
 
Kama ni Kodi halali lipa tu,kama unaonewa si sawa......kuimba kwenye kampeni haimaanishi hutolipa Kodi kijana
 

Samia mama lao..

Mama anaupiga mwingi

Mwaka ujao tena tuwasubiri.
 
Back
Top Bottom