Diamond usiwapuuze wanaokuandama sasa, hao sio shilawadu au Konde Gang. Chukua hoja zao

Diamond usiwapuuze wanaokuandama sasa, hao sio shilawadu au Konde Gang. Chukua hoja zao

Sasa kwanini usimkamate umpeleke rumande kuliko hii kuzunguka zunguka kama kuku anataka kutaga?
Mimi polisi mpaka nimkamate, mbona wao wenyewe polisi na watu wa usalama wanajuwa na ndiyo maana wanamtumia tu kwenye kampeni zao.
 
Tatizo mondi mwenyewe Sasa hivi skendo ndo zina beba kuliko mziki wake. Yaani nyimbo wiki watu washaisahau.
So hata akiomba msamaha... Yule ni mtu wakujali tumbo lake kama most of wanasiasa. So usitegemee akiona ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu au hata za mziki bado atauchuna akisubiria wengine waongee....ni opportunist akusbiri wengine waumie Yeye aneemeke.
Halafu wakati wa anawachamba wapinzani alisahau alizani kuwa mashabiki zake ni wa CCm tu??
Tatizo ni Sasa anapotaka hili jambo liwe la KITAIFA wakati hao mashabiki zake waliomo upinzani wakati wanatekwa wanapigwa mapanga wanafungwa kwa kesi uchwara hakuona sababu ya kuwaongelea. Why now anataka wawe upande wake.
Yeye angekuja a sema jamani "wale mashabiki zangu" naomba mnisapoti but sio kulifanya jambo la KITAIFA.na Uzalendo
Halafu jamani hata tukisema tusapoti hivi kweli hizi nyimbo zake Za weka nipake mate mara nipitie kwenye tope mara nipake mafuta niteleze ndo Nyimbo za kusimama kama TAIFA na kusema zinatuwakilisha???
Mjomba ebu tuwe wawazi kidogo!
Kulingana na hali ilivyo hapa nchini kwetu Tanzania (kiutawala), ungekuwa wewe ni Diamond, serikali ya CCM ingekufuata uiunge mkono ungekataa?
Ungekemea maovu ya serikali? Ungeweza kuwa mwanamziki na wakati huohuo kuwa mwanaharakati?
Chukulia ungekuwa Diamond!
 
Mjomba ebu tuwe wawazi kidogo!
Kulingana na hali ilivyo hapa nchini kwetu Tanzania (kiutawala), ungekuwa wewe ni Diamond, serikali ya CCM ingekufuata uiunge mkono ungekataa?
Ungekemea maovu ya serikali? Ungeweza kuwa mwanamziki na wakati huohuo kuwa mwanaharakati?
Chukulia ungekuwa Diamond!
Ndo maana nasema hata ss hivi angekuja na kusema jamani wale mashabiki zangu wa CCm mnipigie kura. Asingelifanya la kitaifa. Sababu sehemu nyingine za uzalendo na Utaifa anajificha
 
Mwache tu hajui kwamba hao hao waliompandisha ndio watakaomshusha.
Hii statement nimeanza kuisikia kabla huyo dogo hajatoa wimbo wake wa 'number one', nadhani hutoka kwa wale wasiojua mashabiki zake kindakindaki ni watu wa aina gani.
Majority ya die hard fans/fanatics hawana Twitter accounts na hata JF hawamo, zaidi ya habari za udaku za Tiffa, Zari, Mobeto, Wema and the likes hakuna kingine wanachofuatilia.
Ukimkosoa Diamond wanakuchukulia ya kuwa wewe either ni Konde gang au Ali Kiba fan au just a hater mwenye wivu wa maendeleo ya mpambanaji aliyetoka kwenye maisha ya chini kabisa mpaka kuwa high flyer.
Hao activists hawana kabisa uwezo wa kumshusha na kukaa kwake kimya kunawakera kwani walitaka aongee kitu ili waweze ku-twist maneno yake, sasa huyo dogo ana washauri ambao kutetereka kwake kutaathiri maisha yao na familia zao ndiyo maana asemayo/afanyayo yako calculated.
 
Kakaa kimya mnataka aseme ... wabongo tunashida kubwa sana mtu mnamshambulia alafu mnamfundisha jinsi ya kulia?
Ndio maana ya ustaa iyo

Beyonce na ustaa wake wote kuna kundi lake linamfundisha namna ya kuishi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]kupata ustaa ni sekunde tu ila kuumaintain ndio mziki ulipo hapo
 
Hii kitu ni ngumu sana. Nakumbuka bwana diamond mwanzoni hakujihusisha na mambo ya siasa kabisa. Kuna moja ya interview yake alieleza kwamba alifuatwa akitakiwa ku support chama flani... aka delay delay akapigwa mzigo wa tax (kama mna kumbuka) mara paap huyo kwa kampeni.

Kulinda ugali wa familia zetu I bet 99% tungefanya the same thing.
Killmonger Yah nakumbuka mpaka ikawa gumzo bungeni alitakiwa alipe 400m kwa TRA
 
Tatizo hawa "influensazi" na "aktivisti" wa Twitter wanadhani wanaomkubali Diamond ni MATAGA tu, hii vita hampigani na MATAGA tu aisee. Wapo watu ambao hawajawahi kuipenda CCM kabisa lakini wanamkubali Diamond, kuna mwehu anaweza asinielewe, wapo watu wasiokuwa wanachama au wapenzi wa chama chochote cha siasa lakini wanamkubali Diamond, wanamkubali na kumpenda "eidha" kwa upambanaji wake au mafanikio yake au nyimbo zake.
Kabisa mkuu kwamfn kuna mwanayanga aliwah kuvaa jezi imeandikwa simba babalao na kuna wengine wakasema Waz kuwa ni diamond pekee ndo anaweza kuwafanya wanayanga waimbe simba babalao
 
DIAMOND USIWAPUUZE KINA KIGOGO NA WANAMTANDAO, HAO SIO KINA KONDE NA SHILAWADU

Na, Robert Heriel

Diamond hapaswi kupuuza hii movement ya Wanaharakati wa kimtandao na wanasiasa, asije akafikiri kundi hili nila Wale Wasanii wenzake ambao hata shule hawajaenda.

Diamond anapaswa Ajue kuwa Wanaharakati wa mtandaoni ni wasomi tena sio wakubahatisha, wana-exposure ya hali ya juu kumshinda hata yeye mwenyewe,

Kama ningeambuwa nimshauri Diamond kuhusiana na kile kinachoendelea mtandaoni ningemwambia aombe radhi hata ya kinafiki kwani yote anayotuhumiwa ni kweli.

Diamond anapaswa Ajue kuwa kundi hili ndilo lile lile lililokuwa linamshambulia Mwendazake bila kukoma mpaka dakika ya mwisho kabisa bila kujali athari zozote. Ikiwa kundi hili lilimudu kumkabili Mkuu. WA nchi lazima Diamond afikiri mara mbili mbili asifikiri Kama mtoto mdogo.

Simtishi Ila namtahadharisha ili achukue hatua zinazostahili. Nafikiri Diamond Kama atazichukua hoja za hawa wanamtandao akazifanyia kazi atakuwa msanii Bora zaidi kuliko akizipuuza.

Ni kweli kabisa Diamond hakuweza kuzungumzia uonevu na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika miaka ya 2016 - 2019 zaidi ya yote alitoa kibao kisemacho ACHA NIKAE KIMYA.

Diamond asije akadhani hawa wanamtandao ni Wale kina Konde na shilawadu

Diamond lazima aangalie hili kundi linaloongozwa na #Kigigo_kigogo, na wenzake halijawahi kushindwa katika movement wazifanyazo.

Hilo kundi asilipuuze na Kama atalipuuza basi Ajue anafanya makosa makubwa yatakayo mgharimu pakubwa mno.

Diamond asilione kundi hilo Kama watafuta Kick Kama yeye na wenzake kwani kundi hilo halitegemei kick.

Management ya Diamond na washabiki wake ambao kimsingi nafahamu wengi wao wanafikiri kuwa kila anayemkosoa Diamond ni haters wabadilishe huo mtazamo.

Hakuna anayemchukia Diamond labda Wasanii wenzake huko.

Diamond unachopaswa kufanyia KAZI ni madai ya hao Wanaharakati wa mitandaoni.

Wanamtandao hawakatai Diamond kuwa CCM hiyo ni Haki yake Kama apendavyo, lakini tatizo ni diamond kushindwa kutetea maslahi na haki ya jamii yake pale zinaposiginwa.

Diamond Kama anaakili aichukue hii Kama changamoto na ajifunze ili wakati mwingine aweze kutetea maslahi na haki za jamii yake wakiwemo Wasanii.

Lakini Kama atashupaza shingo yake Nina uhakika Diamond huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wake.

Diamond akileta mawazo ya mwendazake akidhani kila anayemshauri na kumkosoa ni hater basi anguko lake halipo mbali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Wivu tu na umaskini unawasumbua
 
Kijana hana washauri wazuri !! mambo ya Usanii na Siasa ni kuwa makini nayo saana, watanzania wanamuhukumu kupitia mitandao.

Ningekuwa mimi, nabadilisha benchi lote la ufundi, naomba radhi naanza ukurasa mpya !!
Vunja bei nae sijui hana washauri naona amejiiingiza kwa fujo siasani.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom