Diamond usiwapuuze wanaokuandama sasa, hao sio shilawadu au Konde Gang. Chukua hoja zao

Diamond usiwapuuze wanaokuandama sasa, hao sio shilawadu au Konde Gang. Chukua hoja zao

Diamond ana mashabiki MAZEZETA sana

Ndio maana petition yake imeishia kupata kura 49 kwa saa 13

Ndio maana hawezi tumia Twitter anajua kule wenye akili ni wengi

Hili daraja hapiti
Hoja ya kuwa Twitter ina watu wengi wenye akili ni hoja ya kizamani mzee, imeshapitwa na wakati. Siku hizi Twitter kuna wajinga na vilaza wa kumimina.
 
Mjifunze kuwa na vipaumbele.
Pambaneni kuhusu katiba mpya, pambaneni kuhusu tume huru ya uchaguzi, mkishayapata haya amieni kwa wasanii. Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye anaweza kupigana vita ambayo anajua kabisa anaenda kupoteza.
 
Yani unamuinea huruma Mondi aliekuzidi kila kila kitu?

Kwa nini usiuonee huruma ukoo wako unaotafunwa na umasikini?
Punguza hasira chief, hawa watu ni wa kwenda nao taratibu kwanza!
😂😂😂
 
Hawa wanaharakati unaowaita ni wasomi na wana exposure ya hali ya juu sana wananifikirisha sana.Exposure yao na usomi wao unawafanya wanashindwa kutambua sio kila mtu lazima awe mwanaharakati kama wao,watu wengine wameamua kuwa wafanyabiashara na mfanyabiashara yeyote anaside na upande utakaomletea faida hyo ndo principle dunia nzima.Hata hao wazungu mnaowaona ni watu wanaosimamia haki pale linapokuja swala la biashara watasimama na ilipo faida.Ndo maana mpaka leo wanaendelea kuinvest Uganda na Rwanda.Diamond ni mwanamziki na mfanyabiashara cku Chadema wakiwa madarakani ataside nao na ccm ikirudi tena atakuwa nao vilevile.Na labda wanashindwa kuelewa au wanajitoa ufaham serikali zetu za Africa ni ngum sana kukuacha ukaishi kwa amani ukianza kuwakosoa refer akina Lissu,Mbowe,Sugu na wengine ndo maana hao akina Kigogo wamejificha kuhofia usalama wao ila wanataka wenzao waende front wakale shaba,au wamesahau kilichomkuta Marehem Remmy Ongala na wimbo wake wa Mrema?
Wanang'ang'ana tu Diamond amechagua upande ambao sio "sahihi". Hakuna mtu timamu anapigana vita anayojua kabisa kuwa matokeo yake ni kupigwa. Watengeneze kwanza mazingira ya akina Diamond "wajao" kuweza kuwa huru kuchagua upande "sahihi". Wakifanikisha hilo watakuwa na haki ya kuwahukumu wale ambao wanashindwa kuchagua upande "sahihi".
Wanalazimisha kumfanya Diamond mwanaharakati, mambo ya ajabu kabisa yaani!
 
DIAMOND USIWAPUUZE KINA KIGOGO NA WANAMTANDAO, HAO SIO KINA KONDE NA SHILAWADU

Na, Robert Heriel

Diamond hapaswi kupuuza hii movement ya Wanaharakati wa kimtandao na wanasiasa, asije akafikiri kundi hili nila Wale Wasanii wenzake ambao hata shule hawajaenda.

Diamond anapaswa Ajue kuwa Wanaharakati wa mtandaoni ni wasomi tena sio wakubahatisha, wana-exposure ya hali ya juu kumshinda hata yeye mwenyewe,

Kama ningeambuwa nimshauri Diamond kuhusiana na kile kinachoendelea mtandaoni ningemwambia aombe radhi hata ya kinafiki kwani yote anayotuhumiwa ni kweli.

Diamond anapaswa Ajue kuwa kundi hili ndilo lile lile lililokuwa linamshambulia Mwendazake bila kukoma mpaka dakika ya mwisho kabisa bila kujali athari zozote. Ikiwa kundi hili lilimudu kumkabili Mkuu. WA nchi lazima Diamond afikiri mara mbili mbili asifikiri Kama mtoto mdogo.

Simtishi Ila namtahadharisha ili achukue hatua zinazostahili. Nafikiri Diamond Kama atazichukua hoja za hawa wanamtandao akazifanyia kazi atakuwa msanii Bora zaidi kuliko akizipuuza.

Ni kweli kabisa Diamond hakuweza kuzungumzia uonevu na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika miaka ya 2016 - 2019 zaidi ya yote alitoa kibao kisemacho ACHA NIKAE KIMYA.

Diamond asije akadhani hawa wanamtandao ni Wale kina Konde na shilawadu

Diamond lazima aangalie hili kundi linaloongozwa na #Kigigo_kigogo, na wenzake halijawahi kushindwa katika movement wazifanyazo.

Hilo kundi asilipuuze na Kama atalipuuza basi Ajue anafanya makosa makubwa yatakayo mgharimu pakubwa mno.

Diamond asilione kundi hilo Kama watafuta Kick Kama yeye na wenzake kwani kundi hilo halitegemei kick.

Management ya Diamond na washabiki wake ambao kimsingi nafahamu wengi wao wanafikiri kuwa kila anayemkosoa Diamond ni haters wabadilishe huo mtazamo.

Hakuna anayemchukia Diamond labda Wasanii wenzake huko.

Diamond unachopaswa kufanyia KAZI ni madai ya hao Wanaharakati wa mitandaoni.

Wanamtandao hawakatai Diamond kuwa CCM hiyo ni Haki yake Kama apendavyo, lakini tatizo ni diamond kushindwa kutetea maslahi na haki ya jamii yake pale zinaposiginwa.

Diamond Kama anaakili aichukue hii Kama changamoto na ajifunze ili wakati mwingine aweze kutetea maslahi na haki za jamii yake wakiwemo Wasanii.

Lakini Kama atashupaza shingo yake Nina uhakika Diamond huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wake.

Diamond akileta mawazo ya mwendazake akidhani kila anayemshauri na kumkosoa ni hater basi anguko lake halipo mbali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Atuondokee tu bwana, huyu dogo kwa sasa hana issue tena tushajuwa biashara zake.....kaishiwa kimuziki, anaganga tu kwa biashara haramu za kina Salim SK na kundi lake nani asiyejuwa hili?
 
Mtu anashauriwa namna ya kuwa Bora wewe unaleta akili za mende hapa.
Diamond hawezi kuomba radhi wala kuikosoa CCM kwani anajuwa fika akifanya hivyo tu yuko chini ya mamlaka kutokana na biashara zake haramu anazofanya na kina Salim SK na kundi zima limzungukalo. In short, the guy is finished and fucked.
 
Kuna tofauti kubwa kati na Msanii mpigania HAKI za binadamu na Msanii anayesifu dhuruma na uovu wa watawala!! nafikiri hapo ndipo mnapompoteza Nasibu. Sasa kwa sababu nyie ni wabishi haya mwambieni aendelee then atauona mwisho wake.

Mitandao ya kijamii ndiyo silaha tosha iliyobakia ya watanzania.

View attachment 1811098
Halafu nyie watu aisee! Eti atauona mwisho wake!!!
Kwahiyo unataka kusema Diamond angesimama dhidi ya serikali mnayoituhumu kuwa ni serikali dharimu angekubalika zaidi na "karia" yake ingekuwa na mwisho mzuri?
 
Chadema bwana, wao demokrasia ni kila mtu kuwa chadema na kuisapoti chadema kwenye kila jambo lao hata kama jambo hilo hukubaliani nalo[emoji2297][emoji2297]
 
Tatizo mondi mwenyewe Sasa hivi skendo ndo zina beba kuliko mziki wake. Yaani nyimbo wiki watu washaisahau.
So hata akiomba msamaha... Yule ni mtu wakujali tumbo lake kama most of wanasiasa. So usitegemee akiona ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu au hata za mziki bado atauchuna akisubiria wengine waongee....ni opportunist akusbiri wengine waumie Yeye aneemeke.
Halafu wakati wa anawachamba wapinzani alisahau alizani kuwa mashabiki zake ni wa CCm tu??
Tatizo ni Sasa anapotaka hili jambo liwe la KITAIFA wakati hao mashabiki zake waliomo upinzani wakati wanatekwa wanapigwa mapanga wanafungwa kwa kesi uchwara hakuona sababu ya kuwaongelea. Why now anataka wawe upande wake.
Yeye angekuja a sema jamani "wale mashabiki zangu" naomba mnisapoti but sio kulifanya jambo la KITAIFA.na Uzalendo
Halafu jamani hata tukisema tusapoti hivi kweli hizi nyimbo zake Za weka nipake mate mara nipitie kwenye tope mara nipake mafuta niteleze ndo Nyimbo za kusimama kama TAIFA na kusema zinatuwakilisha???
 
Unahangdaika bure tu!

Diamond hata akikosa hyo tuzo ataendelea kuwa icon wa muziki hapa tz na EAC kwa ujumla huku chadema ikiendelea kuwa chama cha upinzani.

[emoji23][emoji23][emoji23]Yani ukitafakari sana kwamba kwenye hii kampeni mna gain kitu gani unabaki kuwahurumia tu
😂😂😂😂
Umeupiga mwingi sana humu ndani mkongwe!
Inabidi ufanyiwe "sub"!
 
Atuondokee tu bwana, huyu dogo kwa sasa hana issue tena tushajuwa biashara zake.....kaishiwa kimuziki, anaganga tu kwa biashara haramu za kina Salim SK na kundi lake nani asiyejuwa hili?
Sasa kwanini usimkamate umpeleke rumande kuliko hii kuzunguka zunguka kama kuku anataka kutaga?
 
Diamond Kama haelewi wanachozungumzia wanamtandao nitaamini elimu kweli no muhimu
Samahani lakini mkongwe, "no offense intended".
Kama hauelewi kwanini Diamond ameamua "kuside" na hao unaowaona hawafai wewe ni zaidi ya ndezi.
Kama hauelewi kwanini Diamond ameamua kujiweka kando na uwanaharakati, basi anza kutia mashaka kuhusu elimu yako!
 
Unadhani kila mtu ni shabiki wa mambo ya siasa? kuna sehemu yeyote nimeandika kuhusu chama chochote cha siasa?

Hii thd inamuhusu Diamond na sio chama cha siasa,

Jibu swali nililouliza na kama huna jibu basi ficha ujinga wako kwa kupiga kimya.
Tatizo hao "mbugira" wanadhani kila anayemsapoti Diamond ni MWANACCM!
😂😂😂
 
Back
Top Bottom