Diaspora Hawatoi connection?

Mpango wa kusoma masters ukimaliza ndo unatafuta kazi kupitia kile cheti cha masters cha kule na sio hiki cha tanzania ni moja ya njia rahisi sana
 
wabongo kwenye kusaidiana bado sana mfano mtu ana kila kitu passport,nauli na hela ya kujikimu akiwa mfano marekani kupata mchongo wa kwenda mbele inakua mziki wakati kuna mwaliko tena mtu anaweza kukulipa kidogo kufidia muda wako,kuna internship tunaweza kuonganishiana ata kwa malipo siyo mbaya au kusaidiana link ya vyuo vya bei nafuu kabisa ila kwa mbongo hapo kipengele kukupa mwongozo tuna ogopana sana.
 
Bro europe life ni tamu kaz zipo sijaadithiwa na mtu uwe mchapa kaz tu mi nmerud bongo lakini najuta why nilirud sema tu ni my parents wish lakini Europe asikuambie mtu kugumu sema tu gumu kama we mvivu
Maisha ni kupambana tu
 
Vipi kuhusu nchi za 'Nordic' mkuu hasa Sweden au Denmark...?... unaweza toa msaada tafadhali njia rahisi za kufika huko
Are you fixed kwa AUS tu au hata nchi zingine?
 
Well spoken
 
Aah mwalimu mpwayungu village naona leo umetema point. Vipi na wewe ulijaribu kupaa mbele ukaletewa figisu sio.
Mimi nlidhani ungeishia pale Lyandembela au Kivalali, au ukienda mbali saana basi Ulete (kidding)
 
Vipi kuhusu nchi za 'Nordic' mkuu hasa Sweden au Denmark...?... unaweza toa msaada tafadhali njia rahisi za kufika huko

Sina uzoefu nazo mkuu. Labda wadau wengine watachangia. Check channel ya EBM as well kupata muongozo.
 
Wabongo hawezi kukusaidia ukimtoa. Mshana Jr watz waliobaki Mimi naona bado hawana utu.
Endelea kumuabudu tu huyo uliyemtag,inaonekana na wewe ni miongoni mwa aliowachota akili kwa story zake zakufikirika za kishirikina,

Msaada haulazimishwi,wala hukuzaliwa ili iwe jukumu la mtu mwingine kukusaidia wewe,vipi kuhusu wewe umesha saidia wangapi mpaka leo?
 

Mkuu kwa mfano mimi nakualika wewe kama nani yangu au kwenye function gani?

Nadhani wengi mnadhani mualiko wowote tu unatosha kupewa visa ila hamjui ni lazima muwe na ukaribu na huyo mtu na wewe as a visitor uonyeshe upo well established nyumbani na utarudi ili upewe visa kigezo ambacho vijana wengi hawana maana ndo wanatafuta maisha. Kama haupo vizuri bongo kwa maana ya a stable job, assets, ndoa, watoto, na hela visa ya kutembea kwa mualiko ni mtihani.

Niseme tu diapora wanatumia internet hii hii kutafuta hizo internships na kazi mnazotaka wawajulishe sio kwamba wanaenda kwenye hizo organizations in person. Wewe muhitaji ni bora kuwekeza nguvu nyingi kuzitafuta hizo nafasi, ukikpata ndo mshauriane na mtu wako wa karibu aliyeko huko. Hao diaspora wana majukumu mengine hawawezi kuacha majukumu yao na kushinda online siku nzima kukutafutia internships na kazi. Tujiongeze hapa tuache uzembe na lawama za reja reja.

Hakuna mtu anaogopa kuwapa muongozo ila you're asking way too much hata kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wenu. Mimi sina muda wa kumtafutia mtu chuo, passport au internship huo muda sina kabisa Ila akipata nitamsaidia all the way through ndo maana nilisema lazima ucheze part yako as well hakuna mtu ataacha majukumu yake kukusaidia wewe kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…