Diaspora Hawatoi connection?

Diaspora Hawatoi connection?

Kwanza inabidi uchague nchi unayotaka kwenda.

Pili, chagua njia unayotaka kutumia kufika huko ambayo itakua rahisi kwako. Kwa vijana njia rahisi zaidi ni shule.

Kama una degree omba kufanya masters. Ni rahisi kupata scholarships kwa masters programs kuliko undergrad.

Kama mpango wako ni kuzamia then huhitaji hata hiyo scholarship, apply chuo, visa na nauli zote ni GHARAMA ZAKO. Ukifika unaingia mtaani. Kazi na malazi utapata tu.
Mpango wa kusoma masters ukimaliza ndo unatafuta kazi kupitia kile cheti cha masters cha kule na sio hiki cha tanzania ni moja ya njia rahisi sana
 
wabongo kwenye kusaidiana bado sana mfano mtu ana kila kitu passport,nauli na hela ya kujikimu akiwa mfano marekani kupata mchongo wa kwenda mbele inakua mziki wakati kuna mwaliko tena mtu anaweza kukulipa kidogo kufidia muda wako,kuna internship tunaweza kuonganishiana ata kwa malipo siyo mbaya au kusaidiana link ya vyuo vya bei nafuu kabisa ila kwa mbongo hapo kipengele kukupa mwongozo tuna ogopana sana.
 
Bro europe life ni tamu kaz zipo sijaadithiwa na mtu uwe mchapa kaz tu mi nmerud bongo lakini najuta why nilirud sema tu ni my parents wish lakini Europe asikuambie mtu kugumu sema tu gumu kama we mvivu
Maisha ni kupambana tu
 
Vipi kuhusu nchi za 'Nordic' mkuu hasa Sweden au Denmark...?... unaweza toa msaada tafadhali njia rahisi za kufika huko
Are you fixed kwa AUS tu au hata nchi zingine?
 
Naandika huu uzi baada ya kusoma na kusikia mara kadhaa kwamba diaspora wabongo hawatoi connection za kwenda nje compared to diaspora wa nchi kama Kenya, Nigeria nk. Mimi kama diaspora napinga hii notion vikali.

Hapa JF Kuna nyuzi zaidi ya 100 zinazojadili jinsi ya kwenda nje, a quick search mtu unapata majibu yote na bado watu tunachangia nyuzi kila leo. Mnataka connection gani zaidi?

EBM anatoa free knowledge on YouTube na bloggers wengine jinsi ya kwenda nje, hiyo sio connection? Tuwape bundle za kuingia youtube au?

Mimi binafsi nimeshirikiana na watu kadhaa toka kwenye forum hii hii toka walipoanza harakati zao za kwenda nje na sasa wapo mbele needless to say walifanya sehemu zao na mambo yao yakafanikiwa. Sasa urafiki umekua undugu. Tatizo ndugu zangu wamatumbi mnapotaka connection mnataka hao diaspora wawape hadi hela na passport wawatafutie. You have to play your part as well.

Kimsingi kwenda nje is as easy as ABC. Kupata connection ni vizuri but isn't everything. Mimi nilienda bila connection yeyote ile, maelezo yote yapo kwenye websites za nchi husika ila ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako pia, kuna watu wanadhani diaspora wana a magic code ya kwenda nje this couldn't be further from the truth. Ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako.

Wabongo wenzangu punguzeni kulalamika kiboya, JF Kuna more than 100 threads, YouTube ipo, website za nchi husika zipo, tunajitoa as much as we can but we can only do so much. Maisha yako ni jukumu lako, kusaidiana kupo ila sio wajibu.

Nipo around mazee.
Well spoken
 
Connection inayotakiwa ni wewe akija umpe hifadhi naumsaidie kutafuta kazi na apate viza ya mda mrefu aachane na mambo ya kurenuew viza kila wakati

Sasa nyie mnamwambia tu nauli mpaka Marekani ni million Tatu basi, sasa kujua bei ya nauli ni connection? Acheni uhuni bhana mna Roho mbaya tu
Aah mwalimu mpwayungu village naona leo umetema point. Vipi na wewe ulijaribu kupaa mbele ukaletewa figisu sio.
Mimi nlidhani ungeishia pale Lyandembela au Kivalali, au ukienda mbali saana basi Ulete (kidding)
 
Vipi kuhusu nchi za 'Nordic' mkuu hasa Sweden au Denmark...?... unaweza toa msaada tafadhali njia rahisi za kufika huko

Sina uzoefu nazo mkuu. Labda wadau wengine watachangia. Check channel ya EBM as well kupata muongozo.
 
Wabongo hawezi kukusaidia ukimtoa. Mshana Jr watz waliobaki Mimi naona bado hawana utu.
Endelea kumuabudu tu huyo uliyemtag,inaonekana na wewe ni miongoni mwa aliowachota akili kwa story zake zakufikirika za kishirikina,

Msaada haulazimishwi,wala hukuzaliwa ili iwe jukumu la mtu mwingine kukusaidia wewe,vipi kuhusu wewe umesha saidia wangapi mpaka leo?
 
wabongo kwenye kusaidiana bado sana mfano mtu ana kila kitu passport,nauli na hela ya kujikimu akiwa mfano marekani kupata mchongo wa kwenda mbele inakua mziki wakati kuna mwaliko tena mtu anaweza kukulipa kidogo kufidia muda wako,kuna internship tunaweza kuonganishiana ata kwa malipo siyo mbaya au kusaidiana link ya vyuo vya bei nafuu kabisa ila kwa mbongo hapo kipengele kukupa mwongozo tuna ogopana sana.

Mkuu kwa mfano mimi nakualika wewe kama nani yangu au kwenye function gani?

Nadhani wengi mnadhani mualiko wowote tu unatosha kupewa visa ila hamjui ni lazima muwe na ukaribu na huyo mtu na wewe as a visitor uonyeshe upo well established nyumbani na utarudi ili upewe visa kigezo ambacho vijana wengi hawana maana ndo wanatafuta maisha. Kama haupo vizuri bongo kwa maana ya a stable job, assets, ndoa, watoto, na hela visa ya kutembea kwa mualiko ni mtihani.

Niseme tu diapora wanatumia internet hii hii kutafuta hizo internships na kazi mnazotaka wawajulishe sio kwamba wanaenda kwenye hizo organizations in person. Wewe muhitaji ni bora kuwekeza nguvu nyingi kuzitafuta hizo nafasi, ukikpata ndo mshauriane na mtu wako wa karibu aliyeko huko. Hao diaspora wana majukumu mengine hawawezi kuacha majukumu yao na kushinda online siku nzima kukutafutia internships na kazi. Tujiongeze hapa tuache uzembe na lawama za reja reja.

Hakuna mtu anaogopa kuwapa muongozo ila you're asking way too much hata kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wenu. Mimi sina muda wa kumtafutia mtu chuo, passport au internship huo muda sina kabisa Ila akipata nitamsaidia all the way through ndo maana nilisema lazima ucheze part yako as well hakuna mtu ataacha majukumu yake kukusaidia wewe kila kitu.
 
Back
Top Bottom