Mkuu kuna watu ni walalamishi ajabu! wakiona unafanya mipango ya kutoka ndio hao hao wanaanza kukukatisha tamaa.
Ukitoka wanageuka kuanza kukuomba connection. Mfano mzuri ni mimi, ni juzi tu niliandika nyuzi humu kuhusiana na safari yangu ya Marekani.
Lakini ukilinganisha negative comments na positive, negative ni nyingi zaidi. Kama hiyo haitoshi mbali na yote nimepambana kivyangu (kipesa) hadi kufika.
Sikuwahi kumuomba mwanajukwaa yeyote humu hata senti 5, ikiwa naongopa ajitokeze yeyote niliemuomba na sikuwa na kitu kabisa.
Kikubwa sana ambacho nashukuru ni kuwa watu walinisaidia sana hasa ushauri wewe ukiwa mmoja wao.
Lakini baada ya kuwa nimefika huku umegeuka msaada mkubwa kupita maelezo kwangu, umekuwa zaidi ya ndugu, ninapokwama unanisaidia sana hadi nimewahi kuweka thread humu.
Ajabu mbali na yote niliyoandika kuna watu wananifata DM wananiuliza ulifikaje huko,ukiwaambia wasome nilichoandika tangu naanza harakati hadi nafika hawarudi tena.
Ushauri, ndugu zangu kama wewe ni kijana una ndogo za kufika nje, fanya commitment mwenyewe, utasaidiwa ikiwa unaonyesha juhudi na nia ya unachokipigania mbali na hapo ni ngumu sana.
Jikusanye taratibu tu ila kwa akili sana na mipango madhubuti, fanya mambo yako mwenyewe bila msaada wa agents bila hivyo utatapeliwa na kuishia kukata tamaa.
Ukifika nje amin utasaidiwa tu, mimi ni shahidi wa haya,
Bufa amenisaidia sana, Mungu ambariki sana.