Diaspora tukutane hapa: Tupeane ushauri wa kuanza maisha mapya Tanzania

Hiyo IST haioni ndani kwa Johns Creek High School, kwa mfano tu. Na hiyo ni public high school.

Nikikutajia private schools ndo kabisaaaaaa hiyo IST yenu hata vumbi haitotimuliwa.

Kwanza international school ni shule ya kiraka. Baba akimaliza mwaka wake wa kukaa Bongo anahama na mwanawe. Si shule yenye ubora wa shule za kawaida.
 
Ukiwa vizuri vumbi unalisikia tu.

Utalisikiaje tu wakati liko kila sehemu?

Hadi kwenye barabara za lami [ambazo nyingi, kama siyo zote, zipo chini ya kiwango] vumbi lipo. Uongo?

Hata hao unaodai wapo vizuri nao wanaishi mavumbini tu!

Ona hapo hiyo mimaji ilivyotuama hadi rangi imebadilika na kuwa ya kijani. Na hapo supposedly ni kwa hao walio vizuri! Nani aliye vizuri Marekani aishiye kwenye maji machafu yaliyotuama namna hiyo?



Hapa napo haishi mtu aliye hohehahe. Hilo hapo siyo vumbi? Halafu ona hicho kimtaro....



Hapo napo je? Hiyo siyo barabara ya vumbi na tope? Na kibongo bongo hiyo ni nyumba ya mtu aliye vizuri....

 
Wewe kule huwa hawaendi kujufunza skills ili wazilete huku. Kule huwa wanakwenda kuishi. Wansokwenda kusoma huko hawana tofauti na wahitimu wa hapa hapa nchini. Kutafuta maisha na kutafuta skill ili uje uitumie ni vitu viwili tofauti kwa mtazamo wangu. Wanaweza kukusoa mifumo ya ndani kwasababu wameona mifumo mizuri huko nje ni tofauti na huku kwetu lakini hakuna anayeweze kuja na ku implement mfumo mzuri aliouona huko. Humu serikalini mbona wapo wengi walio soma na kuishi huko nje?! Nenda kaangalie ni mabadiriko gani wameleta huku kwetu waliyoyatoa huko nje?! Hao wazungu walio nunua hekari huko iringa wanaweza kufanya hivyo hata ukiwapeleka mars, hiyo ni asili yao sio sisi tunaopenda kuajiriwa na kulipwa mishahara. Sisi tunaweza kuuza ardhi kwa mzungu kisha tukamfanyie kazi ya kumlimia mzungu huyo shamba. Huwa tunatoa visingizio sana lakini hata hiyo dual citizenship ikikubaliwa wataleta nini?! Wanaweza wakajijengea nyumba nzuri lakini sio investment ya maana. Kama wanaweza auwa na, skills hizo kwanini wasiwekeze hata huko waliko?! Mbona hapa nchini tunatumia computer zinatoka marekani, mbona kuna simu zinatoka kila kona ya dunia na bidhaa kibao. Kama huku kikwazo ni hiyo dual citizenship wawekeze huko ambako ni maraia kwani uwekezaji unamipaka?! Mbona Dangote kawekeza Tanzania au nayeye ana uraia wa Tanzania?! Hizo skills hata wakizitumia huko waliko ni sawa pia. Wakiona Tanzania kunafursa waje tu, weengi waliisharudi wanauliza eti tunaishije baada ya muda wanaelewa tu na hawana cha skill wala nini, lakini ungewakuta huko nje ungesikia story za uwekezaji kibao. Wako wengi na wengine wameajiriwa tu hakuna cha skills walanini.
 
Mimi ni mzawa hao wazungu wamenunua kama wawekezaji au ndio unawachoma hivyo kwa Lukuvi. Mimi benki za Dar ziliniambia siwezi kufungua akaunti kwa sababu sio raia.
Siwachomi, wamenunua kihalali. Sasa ambao si wazawa wanaoperate account iweje wewe mzawa ukataliwe?
Au ulivyoombwa barua ya mtendaji ukaenda jumla?
Mimi nawashauri, mkiwepo huko Diasporani[emoji28] jitahidini kutafuta fursa mrudi kwenu kuendeleza kwenu, msikae mnasifia vya wamarekani wakati ndugu zenu wanalima kwa jembe. Mfano Marekani mnakula ndizi za southern america, ambazo bukoba tunatengenezea pombe (rubisi), kule mbeya zinaozea masokoni, moshi zinakatiwa mbuzi. mnaweza kuziexport na kutengeneza pesa ya maana na kunufaisha familia na nchi, kwa kuanzia na mtaji ambao mnaudharau huko. Kumbukeni, Kwa namna moja ama nyingine unyanyapaa wa Nazism ndio umeleta kuwepo kwa taifa bora la Waisrael, msisubiri trump awarudishe, jirudisheni wenyewe.
 
Nyani Ngabu upo sahihi, lakini sasa unafanya nini kuleta mabadiliko? Au utabaki kusifia jiko safi la mjomba huku kwenu mkipikia mafiga kwenu?
Mbaya zaidi hata wazaliwa wa huko ambako mnakusifia wamekubali kuishi hukuhuku kwenye vumbi na mitaro michafu, tena wakiwa na vyeo vya juu, tunapishana nao kila mara mitaani, sembuse nyie.
Ni sawa Watanzania tulio wengi tunaishi kwenye uchafu, leteni usafi wenu nasi tunabadilika. We are not Rwandese!
 

Nafanya nini kuleta mabadiliko? Nalipa kodi.

Wewe unafanya nini?
 
Nafanya nini kuleta mabadiliko? Nalipa kodi.

Wewe unafanya nini?
Mimi nafanya ninavyoweza kwa uelewa wangu nilionao, pamoja na kulipa kodi kila mtu analipa, nawe ongeza na exposure uliyoipata huko ughaibuni
 
Either direct or indirect, wote tunalipa kodi mkuu. Hata nnayekula vegetables ambazo nimelima in my backyard nimezilipia kodi kwenye mbolea

Basi wote tunachangia maendeleo ya taifa, iwe moja kwa moja au vinginevyo.
 
Kwa nini unarudi mkuu?
Mi nnataka kuimbia nchi, nishauri nianzie wapi mkuu huko chi za watu.
 
Ndio.
 
Mimi ni mzawa hao wazungu wamenunua kama wawekezaji au ndio unawachoma hivyo kwa Lukuvi. Mimi benki za Dar ziliniambia siwezi kufungua akaunti kwa sababu sio raia.
Tatizo na nyinyi mnaongea sana. Mbona wengi tu wana US/British passport na wapo Bongo wanafanya mambo yao bila bughudha.
 
Kumbe VUMBI mlimaanisha dust mimi nilijua UKATA...BTW mimi ulaya nilikuwa nasumbuliwa sana na HAY FEVER....Ile vumbi fulani hivi
 

Hamna kisingizio bali ni uhalisia, nchi yetu imejaa fitna na mambo ya kukomoana
 
Kumbe VUMBI mlimaanisha dust mimi nilijua UKATA...BTW mimi ulaya nilikuwa nasumbuliwa sana na HAY FEVER....Ile vumbi fulani hivi

Hilo siyo vumbi la chavua kweli? Unajua chavua ni nini?

Hata hili vumbi hapa kwenye picha ni la ukata. Kwa walio na hela hukuti vumbi la hivi mitaani.

Unabisha?



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…