Diaspora tukutane hapa: Tupeane ushauri wa kuanza maisha mapya Tanzania

Diaspora tukutane hapa: Tupeane ushauri wa kuanza maisha mapya Tanzania

Hahaha hapa ndio unapowaua

wakupe uwenyekiti tu bado upo Dernmack?
 
Aisee mie naogopa kuumwa,ningekua mzima na sina hayo maradhi niliyonayo ningerudi.Tanzania kuna fursa nyingi za mtu kujiendeleza kwa sababu nchi yetu bado inakua,a lot of opportunities ,Tanzania ukiwa broke utalima nje viazi,utakula,ulaya ukiwa broke ni hadithi nyingine,lol
nchi gani huko dada yangu
 
Inategemea pia unataka kurudi bongo ukafanye nini? Kula pensheni yako ? au uendelee kuchacharika kulisaka tonge? Je una investments (assets) ambazo zinatengeneza hela bongo, au una liabilities (dhima) ambazo zitakugharimu hela?

Umekaa ughaibuni aka ng`ambo, mamtoni, majuu miaka mingapi? Na katika muda huo wote ulishaweza kurudi Bongo kusalimu ndugu jamaa na marafiki pamoja na kuyajaribu maji (To test the waters). Ukirudi kichwa kichwa unaweza kuumbuka.

All in all, home sweet home, hata kama utarudi uwe choka mbaya, nyumbani ni nyumbani
 
Ukitaka kurudi Tanzania hakikisha ushajenga nyumba yako, na una gari yako ya matembezi. Na utakapo jenga hakikisha ni nyumba ya geti sio uswahilini. Angalia jinsi ya kuwekeza kama utafungua biashara ya vyakula itakuwa nzuri sana manake haina mikopo. Na restaurant yako iwe ya kisasa ilio safi, kama utaangalia kwenye kilimo huko napo kuzuri sana Watanzania wengi hawajaamka kwenye kilimo cha kisasa. Tanzania kuna hela kama utajua jinsi ya kuitafuta, Mfano Ulaya na America ukienda shule income yako ya mwaka ipo juu kuliko anaefanya kazi za kawaida(factories, Nursing home, general labor). Ikiwa umeweza kujituma ulaya sidhani kama utashindwa kujituma nyumbani. Ulaya unatajirisha tajiri wa company lakini ukija Tz wewe ndio unakuwa tajiri na kuajiri watu.
 
rudi tu bongo kwa income ya 1.5m per month unaish vizuri sana

ukiweza kuwa na mbinu za kuipata hiyo kwa mwezi utaishi vizuri tu

Aisee!

Kuna watu wanaridhika jamani.

Tshs. 1.5M ni wastani wa $750.

Watu wanatengeneza zaidi ya $1000
Ndani ya wiki na ni kazi ya kawaida.
Huyu atahitaji Kurogwa kurudi.
 
kwa bibi,siwezi kusave sijui kwa nini,nipe mbinu basi,lol

Dada Rebeca hii ni changamoto kwa kila mtu ila inabidi ujue saving inatakiwa kua sehemu ya matumizi yako ya kila week au mwezi...

kama unavyoweka kodi, chakula, usafiri mawasiliano usiache kabisa kuweka na akiba na dharura na pambana ukikwama tumia dharura sio akiba... mwanzo ni mgumu sana mimi nilikua natumia mpaka kodi
 
Ulaya ni ngumu SANA. kama umeenda kimagumashi utatamani urudi home maana utaonekana kama kinyangalika fulani. kwa mTanzania kwenda ughaibuni ni kupoteza muda tu. hapa pana fursa nyingi SANA. Ulaya ni mwendo wa kubeba box na kuwapokea mizigo wageni wanapoingia na kutoka hotelini. waache Wasomali na Wakongo wapigike huko. sisi hapa shwaari.
for Tanzanians to go outside the country is by choice not by chance.
 
Copenhagen DN

Mkuu London ni expensive kuliko miji mingine,rent iko juu,ila kazi zipo kibao

nje ya mji,kuko poa rent ni cheap sema kazi hamna,

namanisha hizi unskilled jobs

unafanyaje wa anglikana wakulipie rent?lol

Mkuu wewe kweli mjeda
 
Dada Rebeca hii ni changamoto kwa kila mtu ila inabidi ujue saving inatakiwa kua sehemu ya matumizi yako ya kila week au mwezi...

kama unavyoweka kodi, chakula, usafiri mawasiliano usiache kabisa kuweka na akiba na dharura na pambana ukikwama tumia dharura sio akiba... mwanzo ni mgumu sana mimi nilikua natumia mpaka kodi

Asante mkuu,nimejifunza kitu
 
ulaya ni ngumu SANA. kama umeenda kimagumashi utatamani urudi home maana utaonekana kama kinyangalika fulani. kwa mTanzania kwenda ughaibuni ni kupoteza muda tu. hapa pana fursa nyingi SANA. Ulaya ni mwendo wa kubeba box na kuwapokea mizigo wageni wanapoingia na kutoka hotelini. waache Wasomali na Wakongo wapigike huko. sisi hapa shwaari.
for Tanzanians to go outside the country is by choice not by chance.
Sasa maisha msomali angekuwa anaishi Somalia ukilinganisha anayoishi Denmark ama Norway dah
 
Da'Vinci
Mkuu kukata tamaa sio njia njema kwenye maisha ya binaadamu. Kuna njia nyingi tu za kujaribu mfano hutoka mialiko ya dini na shuhuli tofauti. Pia unaweza kujifanya mfanyabiashara una duka lako unataka kuweka bidhaa kutoka USA au Europe. Uswahilini kuna njia kibao za kujifanya mmiliki wa company isiojulikana(nadhani umenifahamu) ukienda ubalozini jiweke katika hali nadhifu (kiofisini) ongea English ya kiofisini sio ya ki mtaani.
 
labda zamani,siku hizi ukiwa na biashara unataka kuinvest unatakiwa uwe na kiasi kikubwa tu kabla ya kufanya biashara yenyewe,
 
ulaya ni ngumu SANA. kama umeenda kimagumashi utatamani urudi home maana utaonekana kama kinyangalika fulani. kwa mTanzania kwenda ughaibuni ni kupoteza muda tu. hapa pana fursa nyingi SANA. Ulaya ni mwendo wa kubeba box na kuwapokea mizigo wageni wanapoingia na kutoka hotelini. waache Wasomali na Wakongo wapigike huko. sisi hapa shwaari.
for Tanzanians to go outside the country is by choice not by chance.
Wabongo bana! Leo Tz kuna fursa? Hapa hapa mnapolia kila siku Magu kawabana hela hamna mtaani....hamna demokrasia?
 
Back
Top Bottom