Still sio kitu cha kuja mtandaoni ku-brag huku ukiponda watu.
Ona sasa unakimbilia kusema naringa. Sio kuringa ni kuachana na blah blah. Ningesema tu natengeneza pesa nyingi ingekuwa ni mizinguo ya kiswahili tu. Kimsingi ni zaidi ya dola laki na nusu. Ni kitu kama 170 na chenji. Vichenji vingine vina udhia kupata namba yake kamili. Kuna pesa niliyorudishiwa na watu wa kodi na kuna malipo ya bima.
Na kumbuka nilisema si ujanja. Bwege yeyote akiingia Marekani akiwa mtu wa kujituma katika chano za pesa anaweza kutengeneza hiyo pesa. Kama una mshahara wa elfu tisini ukiendesha teksi, Uber, ukiwa mlinzi, ukipeleka piza, ukiosha vizee, ukiwa na kiduka sehemu, ukitengeneza magari kwenye gereji ya mtu utashindwa kupata zaidi ya dola laki kwa mwaka?
Ofisa wa BOT akitoka kazini mshahara haumtoshi atakubali kuwa mlinzi mahali au afungue kibanda cha chipsi. Hatakubali ataona bora achonge mchongo wa wizi kazini.
Utamkuta mbongo yuko Tanzania hana kazi, hana pesa tapeli tapeli tu anawacheka walio nje eti wanalea vizee. Hizi mnazoziita kazi chafu ndio zinazofanya Ulaya na Marekani watu wasikose kazi.
Wabongo kazi kama za ulinzi mnaona utumwa mnawapa wamasai walinde nyumba kwa sababu hamuwalipi. Wewe na mahela yako uwani usiku kumejaa wamasai utafikiri wameuwa simba.
Mwanadiaspora akipata elfu sitini kwa mwaka anaridhika. Hamna sherehe au shughuli ya wabongo atakayokosa.
Kama una nyumba kubwa ukipangisha basemant yako unaweza kupata hata elfu kila mwezi juu ya mshahara wako wa mwezi. Lakini watu wanakaa kwenye apartment masharti ya kipumbavu kama Mwananyamala tu. Na nyumba yangu sipangishi mtu. Hakuna raha kama kutembea ndani ya nyumba uchi (butt naked) kutoka chini levo ya kwanza mpaka juu gorofa ya tatu.
ONYO KALI KWA WOTE WANAOKEBEHI DIASPORA NA MUAMSHO KWA DIASPORA WAVIVU NA BONGO LALA WALIOKO NJE HOHE HAHE AFADHALI WANGEBAKI BONGO.
Na nyie watu wa uhamiaji hamtukomoi mnakomoa nchi. Wenzenu walioamka kama Kenya na Nigeria wanapata pesa kibao kwa raia wao wenye uraia wa nchi mbili. Benki za Tanzania zilinikatalia nisihamishie dola zangu kutoka Marekani kuja Tanzania. Hasara ya nani hapo? Yaani wamenitibua wacha ninunue tiketi ya kwenda Jamaica nikale kuku kwa mrija wajamaica wachukue dola hizo.