Uteuzi pia lazima uzingatie mchango wa muhusika katika nchi anakotoka.Uwe wa kodi nk
Ukiangalia ma diaspora wengi wangependa waje kuongoza mashirika mfano yanayolipa vizuri yaliyoanzishwa na watu wa ndani kwa kodi zao.Diaspora wanataka kuvuna wasipopanda.Utakuta wengine walikimbia nchi wakasema ina hali ngumu.Kuna watu wakabaki wakapigana wakiwa ndani hali ikawa nzuri sasa inapofikia uteuzi hivi Raisi aache kumpa mpiganaji aliyebaki ndani mwenye uzalendo na nchi yake jua liwake mvua inyeshe aende akatafute mkimbizi wa kiuchumi anayeitwa diaspora ampe?
Anyway ili Diaspora wa Tanzania muonekane wa maana igeni wenzenu ma dispora Wahindi,wachina na wazungu na waarabu
Diaspora wa kizungu,kihindi,kiarabu na kichina kazi yao huwa ni
1.Kueneza utamaduni wao kwenye nchi husika.Mfano mzungu ataleta mambo ya kizungu,hoteli za kizungu.Tabia za kizungu,mila za kizungu,Mavazi ya kizungu nk
Mhindi vivyo hivyo na mwarabu vivyo hivyo na mchina vivyo hivyo Kama mzungu.Mchina ataleta hadi CHINESE restaurant
Taabu inakuja kwa Diaspora la kitanzania likienda kwa watu ni taabu litaanza kila kitu kuiga cha kule lilikoenda.Unakuta hata uvaaji jitu nzima zee lakini limetinga kikaptula na kikofia cha machizi.Kula utakuta linajisifia kula MCdonalds nk Kuliko kula KANDE ZA KITANZANIA.
Hata kunyoa tu litanyoa kaa bweeege fulani hivi la marekani au ulaya hata huwezi lijua kama ni litanzania.
2.Madiaspora wa nchi za kizungu ,kichina,kiarabu na kihindi wao huwa kazi yao kuleta na kuuza bidhaa za kutoka kule kwenye nchi zao.Ukiwaona wazungu unajua atauza vitu vya kizungu,ukiona muhindi unajua yeye ni muuzaji wa bidhaa za india,Ukimwona mwarabu unajua kabisa biashara ya mafuta na gesi toka uarabuni yeye ndio mwenyewe ,Ukiona mchina unajua yeye ndio agenti mkuu wa biashara za china huko aliko.
Kwa kuwa mawakala wa biashara na bidhaa za nchi wanakotoka wanaziingizia nchi zao mapato kibao.
Ukija madiaspora wa kitanzania ukiuliza nani agent wa biashara za Tanzania kule unakuta hakuna! Wako tu kule kama vibarua wa wazungu halafu kesho utasikia mtukumbuke kututeua.
Sipingi Raisi kuteua lakini wameisaidia nini Tanzania sio familia zao.Mfano akiwepo Diaspora analeta watalii labda elfu moja kwa mwaka mimi nitakuwa wa kwanza kuomba huyo diaspora ateuliwe kuwa balozi mdogo kwenye ubalozi wa Tanzania kwenye hiyo nchi alipo.Lakini hivi hivi tu hakuna.MKONO MTUPU HAULAMBWI .kILA DISPORA ajiulize kwa nini anafikiri ateuliwe ametoa mchango gani kwa nchi?
Madiaspora wa Tanzania jifunzeni kwao muwe na faida kubwa kwa nchi yenu Tanzania kama wenzenu