Diaspora wa Uingereza walikuwa wanaringa sana kwa nguvu ya Pauni, sasa hivi tunawacheka

Diaspora wa Uingereza walikuwa wanaringa sana kwa nguvu ya Pauni, sasa hivi tunawacheka

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuka Wanajamvi!

Enzi hizo kwa Bibi wee. Mambo ya Sterling pound pesa iliyokuwa na nguvu. Yani diaspora wa uingereza enzi hizo wacha wee full kujiinua hasa wakituma au kuchenji hela zao. Sie wa akina krone, krona na kroner tulidharaulika sana.

Kujiinua taratibu zinakwisha. Na walivyomuweka mmatumbi ndo waziri wao wa fedha ndo pauni inazidi kwenda chini ikimfuata bibi.

Norway bei ya mafuta ilivyoshukaga walichekaga sana. Eti walizoeaga easy going life now they have to work very hard for the bread.

Elli Richard Sky Eclat Magonjwa Mtambuka
 
😂😂😂 wanaringa alafu hata balozi akiitisha vikao waishia kuja na masambusa , machapati maandazi na pilau kwenye vikao utafikiri balozi wanataka kujua afya Zenu na menu zenu! Hakuna anayeongea points au hata ideas hakuna! Diaspora UK na Ireland you guys must unite and change! muonyeshe upendo ninyi kwa ninyi muache kufitiniana!

Big up kwa Diaspora from the other side!
 
Pound inamfata mama yake kaburini🤣 bado dollars nayo izeeke kama kile kibabu 😁. Tanzania shillings na Kenya shillings nazo zipande bus kama marais wao😂
Dollar ndiyo inazidi kuimarika kwenye kipindi hiki cha global inflation...maana investors wengi wanainunua ili ku preserve mitaji yao. Wao wanaita safe haven currencies....sarafu nyingine imara kwa sasa ni Japanese Yen.

Kaangalie Index ya USD...kwa leo imeweza kufikia 114...figure ambayo Dola haijawahi kufika huko nyuma. It means the $ is getting more stronger than before and this is bad news for global economy.
 
Hapo ndo nashangaa, kwamba dollar ikiwa strong dunia nzima yaumia, ikiwa weak dunia yafurahi...
Waweza elimisha kidogo?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Pound inamfata mama yake kaburini[emoji1787] bado dollars nayo izeeke kama kile kibabu [emoji16]. Tanzania shillings na Kenya shillings nazo zipande bus kama marais wao[emoji23]
Umeua you made my day... Teh teh teh teh teh....
 
Kushuka kwa pound ni suala la muda tu, waziri wa fedha mmatumbi kawaahidi wasipanic wanachokitaka kiuchumi kitakua halafu ndio pound itapanda sana huko juu mawinguni teehteehteh. Ngoja tusubiri tuone kinachoendelea kwa sasa maana leo kwenye soko la Asia pound imestabilise. Ila wabongo wakumbuke kua hata hapo pound ilipo ni parefu sana ingawa imeshuka maana wakati tu wa kipindi cha Mkapa na mkwere mwanzoni, pound ilikua 1500 - 1700 Tshs.
 
😂😂😂 wanaringa alafu hata balozi akiitisha vikao waishia kuja na masambusa , machapati maandazi na pilau kwenye vikao utafikiri balozi wanataka kujua afya Zenu na menu zenu! Hakuna anayeongea points au hata ideas hakuna! Diaspora UK na Ireland you guys must unite and change! muonyeshe upendo ninyi kwa ninyi muache kufitiniana!
Big up kwa Diaspora from the other side!
Sio huko tu tibia za watz hata USA na Canada ni hizo hizo,kama tumelogwa hatupendani,majungu,fitina
 
Mimi niliishi pale mkuu kwa muda kidogo kabla ya kurejea Bongo, (ila bado naweza kuingia pale) nafahamu A-Z za pale ila sikuwa sana na diaspora kwani wao kama alivyoeleza jamaa hapo juu hawako na umoja.

Pauni ni kweli ilikuwa pana sana ukiigeuza kwa madafu hapo juzi kati ila sasa hivi ni shida kidogo dola imekuwa juu, yaani mmarekani apeta tu.

Hali kwa sasa kwa UE ni ngumu sana na huenda baada ya 2 years jamaa wakaondolewana Labour Party.
 
Sio huko tu tibia za watz hata USA na Canada ni hizo hizo,kama tumelogwa hatupendani,majungu,fitina
Tatizo ni backgrounds yachangia ila kama backgorund ipo poa (kwa TZ) unakuwa poa na huitaji diaspora.

Background kama ni ya kimaskini wabongo hawawezi kuwa kitu kimoja kwani kila mtu ajali ya kwake kwanza.

Pili, ni aina ya education mtu alochagua kwani wengi walichagua aina fulani za education ambazo kwa kule huwezi kutoboa ila wabakia na kazi za viwandani au warehouse.
 
Sikumbuki ni lini Uingereza kumewahi kuwa na maisha rahisi kwa mtu anayeishi kwa kutegemea part–time job.

Na hivi pounds inaporomoka mambo yanazidi kuwa magumu kwa ndugu zetu wanaofanya kazi in shifts

Ndo changamoto za mpambanaji
 
Back
Top Bottom