Diaspora Wetu Wanafanya Nini cha Kuonekanika Huko Ughaibuni?. Diaspora Mliofanikiwa, Onekanikeni Kupitia TAK na Rudisheni Tanzania Japo Kidogo!

Kwani serikali imeshindwa kuwawekea vitanda na hayo madeski ? Msaada sio deni, si mama amesambaza madeski nchi nzima na kujenga shule na vituo vya afya vya kisasa nchi nzima au yameliwa na mchwa ?
 
Kila mwaka wa fedha serikali ya chama Chako Cha CCM,kinatumia 500+b kununua magari ya kifahari na wakati huo huo watu wanajifungulia chini na wanafunzi Wana kaa chini,mbona hautoi ushauri kwa serikali kuacha matumizi ya anasa na pesa kupelekwa kwenye sekta zinazo wagusa wananchi moja kwa moja ?

Alafu wakati huo huo unataka watu walio jipambania wenyewe bila msaada wa serikali ya CCM,kufanya Kazi ya serikali ya kudumisha miundombinu ya hospitalini na shuleni?
 
huyo mama aliyejenga kituo cha polisi na zahanati namfahamu sana. ni wa nyumban kabisa. alikuwa anafanya kazi hosp. na sasa amestaafu ila ukweli ni kwamba amesaidia sana wengi pale kijijini. hyo zahanat ilikuwa haina choo ndo kusaidia kujenga choo cha kisasa pamoja na maji
 

Na viongozi wa Tanzania wanashindana kutumia fedha za walipa kodi kununuliwa magari ya kifahari ya VX, safari zisizoisha Dodoma, Dar es Salaam, marupurupu fedha hizo zinazidi anazopata diaspora aliyejituma kwa kufanya kazi kwa bidii huku viongozi wa Tanzania wakitumbua mfumo wa hazina ya taifa kwa matumizi ya kufahari.

Kutumia mabilioni ya shilingi za kitanzania kufanikisha uchafuzi wa mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa na Kuhitimisha uchaguzi feki wa 27 November 2024...

Hii ni mifano michache ambayo serikali ingeweza kutumia fedha hizo bila kutapaya ovyo hata huruma kutoa huduma ya afya buree kwa raia imeshindikana wakati nchi kama Cuba wameweza kuzuia maradhi na pia kutoa huduma bure kwa raia kwa kiwango cha huduma zinazilingana na zile za huduma afya katika nchi za dunia ya kwanza
 
Tuanze na wewe ng'wanangwa, mke wako ni Diaspora amewekeza nini huku home?
 
Diaspora wa kitanzania ni njaa kali tu wengi wanasubiri wafariki watusumbue michango! Sitoi mchango wangu kwa Diaspora! Wenzao Wakenya kila mwaka wanatuma mabilioni nyumbani kusaidia uchumi wa nchi wa kwetu kuzurura tu! Marehemu Le Mutuz alirudi nde.ke.ma tu bila chochote!
 
Labda wanaogopa kuombwa ombwa hela,
Ni kweli,hili la watu kuomba hela ni tatizo, hata cha nilipopeleka hili wazo la kipindi TAK, walitangulia kusema hatuna hela!,nikauliza kwenye proposal yangu, kuna popote nimeomba pesa ?。
vile vile kuna misukosuko ya kisiasa akionekana hajakubaliana na baadhi ya masuala ya kiserikali,
hili ndilo linakwamisha uraia pacha, kuna majinga kule serikalini wanaamini diaspora wote ni wapinzani na wata support the opposition, kumbe kuna diaspora wengi kibao, hawana kabisa interest na local politics。
mfano Mange kimambi aliwahi kufungiwa ofisi za ile app yake
Huyu bidada alizidi,najua unajua bidada ni kichaa kabisa, alikuja kuwa too much!,yeye sio mtu wa av production,akaletewa a doctored video ya kiongozi akifanya mambo flani binafsi, yeye akajitapa atarusha!, hata ningekuwa mimi, nafunga!。
Kuna levels fulani mtu hawezi kurekodi video zile kisha zitue kwa huyo kichaa!
P
 
Kwani ni uongo sasa?
Duh。。。!, Mkuu Manjaga, Manjagata hata wewe?!。 Mtu wao anaweza kuandika haya humu,
P
 
Mkuu kwa nini huwa mnachuki kiasi hicho ? Kuchangia uchumi kinamna gani ? Lini serikali ya Tanzania ilisaidia watu kupata fursa nnje ya nchi kama inavyofanya kenya ?
 
Kosa kubwa wanalifanya diaspora na kuwafanya wapate ugumu wa uraia pacha ni Kama anavyofanya huyo mdada kudai hawezi kuwekeza huku Hadi uraia pacha uruhusiwe.
Kama wangewekeza nyumbani kwa maswala ya afya, elimu, viwanda, kilimo wangetengeneza ushawishi mkubwa kuanzia kwa wananchi wa kawaida mpaka wanasiasa kupitishwa Sheria ya uraia pacha. Lakini wamewekeza ugenini huku kwao wameacha kwa kisingizio Cha kusubiri Mambo ya uraia pacha. Matokeo ukimwuliza mwananchi wa kawaida faida ya uraia pacha haioni.
 
Amini usiamini diaspora kama huyu atabarikiwa sana, huu ndio utu na uzalendo wa kweli。
P
 
Mkuu kwa nini huwa mnachuki kiasi hicho ? Kuchangia uchumi kinamna gani ? Lini serikali ya Tanzania ilisaidia watu kupata fursa nnje ya nchi kama inavyofanya kenya ?
Onyesheni mfano ili serikali ijione ilikosea! Hata wenzenu Kenya walianza kwanza kwa kutuma kidogo kidogo mpaka ikaona kumbe kuna fursa! Sasa nyie wa kwetu kulilia michango ya kusafirisha maiti tu! Mzikane huko huko msitusumbue sisi!
 
Wazo la maana sana hili.

Hakuna umuhimu wowote wa kujulikana, kila mtu aishi maisha yake tu.
 

Kwa sheria na uchawi wa mpaka kufikia rais wa nchi anasema anataka aone matajiri wanaishi kama mashetani nani yupo tayari kubeba risk ya namna hiyo? Hao unaowatolea mfano ni kwa sababu nchi yao ya baba na mama inasupport na kuheshimu mchango wao. Kwa nchi ambayo mawaziri wanatoa macho hadi yanataka kuanguka wakisikia diaspora hamna atakayesema issuez zake kiongozi. Its safe to be low profile as a Tanzanian than showing what are your achievements. Najua habari ndio biashara na maisha yako lakini hamna mtanzania atajitangaza ili awe victim wa kufelishwa na ndugu zake! Tubaki JF kuchitchat tu baba, mengine yabaki personal
 
Watu wengi hawana interest kujulikana Bongo.
Ni kweli kuna watu wako very low profile,ila kuna low profile ya being low humble na kuna low profile ya kuwa discreet,ila kuna low profile ku hide, watu wasijujue, zote hizi tunazijua na tunaziheshimu, ila nyingine ni uchoyo tuu, being secretive, siku hizi kuna watu wanapiga picha na mabulungutu ya mahela, ma dola,ukiwauliza what they do,hawasemi!。Lengo la TAK, is to highlight the sucess stories za diaspora wetu, mfano mzuri ni huu,
Nchi imewakataa sasa washoboke nayo kwa nini?
Sio kweli nchi imewakataa, uraia pacha unakuja。
Watu wanajulikana na familia zao na kwenye jamii zao huko.
Yes,its true,mimi wife ni diaspora amevuta ndugu zake wote,hadi mama yake, siku nakwenda kumsalimia,kanipiga na $1000 ya soda!na huko kwao usipime,ila its not enough,kusaidia ndugu ni wajibu hupati baraka kubwa kama charity ya kusaidia the poor Tanzanians。
Leo nilikiwa naongea na mtu kajenga zahanati na kituo cha polisi kwao huko kijijini.
mtu kama huyo atabarikiwa sana, just imagine kama all successiful Tanzania diaspora all over the world wangekuwa visible,what they do and share their success stories na wengine,na ku streach their helping hand to reach the poor of the poor, it would make a big difference!
Hicho ndicho muhimu kwake.
naunga mkono do what you like,what you love,and what will make you happy, kama mtu umebarikiwa,umefanikiwa una uwezo wa kununua magari 5 ya kifahari,and that is what makes you happy,be happy,but take it from me,the true happyness ni yule aliyejenga hospital na police post。
Kwenye kuwekeza nchi haina sheria rafiki watu hata kusaidia wanaombwa rushwa.
Hili ni tatizo
Yani unasaidia halafu unaombwa rushwa ili usaidie.
duh。。。!
Nani anataka ujinga huo?
Usiite ujinga, mimi kama mtu wa media,nina genuine kuona the visibility of successful diaspora to share their success stories
P
 
Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, issues za kikanda na kimataifa, AU, SADC, AfCFTA, Bunge la Afrika, Bunge la EAC, Jumuiya ya Africa Mashariki, EAC na mambo mengine ya kimataifa. Ki

Umefanya vizuri ila kiwe kipindi katika lugha ya kiingereza, TV za lugha ya kigeni hakuna kabisa, waandishi wa habari waliotayarisha vipindi na mahojiano kwa kiingereza hakuna kabisa labda yule wa Mwananchi digital na The Chanzo. Viongozi na watanzania wa kawaida hatuwaoni.

Waandishi wanejazana ktk vipindi vya lugha moja tu rasmi ya KiSwahili wakati kuna ya Lugha rasmi ya pili Tanzania kiEnglish. Kenya wanapiga lugha zote ndiyo maana inasikika kimataifa na kikanda.

Mwandishi nguli anzisha Mapinduzi katika tasni kwa kuitangaza Tanzania na diaspora ktk vipindi utavyotayarisha katika lugha zote mbili rasmi za taifa la Tanzania. Uzuri una uwanja mpana kama mwandishi wakili msomi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…