Diaspora Wetu Wanafanya Nini cha Kuonekanika Huko Ughaibuni?. Diaspora Mliofanikiwa, Onekanikeni Kupitia TAK na Rudisheni Tanzania Japo Kidogo!

Mange ana matatizo yake tatizo kwenye kushughulikia haya mambo kunakuaga na double standard kiasi kwamba watu wanaanza kufikiri ni kama kukomoana tu.

Kuna watu wengi sana wanavunja sheria, wanadhiaki wengine na mbaya zaidi wapo mpaka wanatashia maisha ya watu lakini kwa sababu ni watu wa system au machawa wa chama tawala huwa hawaguswi.

Kosa alilolifanya Mange ni dogo sana ukilinganisha na kitemdo alichofanya Bashite cha kuvamia studio za clouds na silaha za kivita lakini hakuchukuliwa hatua zozote. Nakubaliana na wewe Mange ni kichaa lakini izo sheria za kushughulikiana ziwe msumeno kwa wote angalao italeta picha kwamba hakuna conflict of interest za kisiasa
 
Wazo la maana sana hili.

Hakuna umuhimu wowote wa kujulikana, kila mtu aishi maisha yake tu.
Wabongo wengi na serikali yao wana tabia ya kuwapuuza watu, halafu watu wana fight kivyao mpaka wanaitoa huko nje, halafu wakishaitoa ndiyo utawasikia "huyu Mtanzania".

Abdulrazak Gurnah kaondoka Zanzibar zamani sana in the 1960s huko. Kaenda Uingereza, kasoma kivyake, kafundisha vyuoni. Serikali ya Uingereza imekuwa na mchango mkubwa kwake kuliko Zanzibar/Tanzania.

Alivyoshinda nishani ya Nobel tu, watu wakaanza kum claim "huyu Mtanzania".

Hawajamsoma, hawamjui, hawajamsaidia, wamemzingua mpaka kaamua kuishi nje kama mkimbizi asiye na kwao.

Halafu aliposhinda nishani ya Nobel mpaka rais wa Zanzibar kajiweka karibu naye akisema huyu Mzanzibari.

Leo kuna mshikaji alikuwa anakaa Canada karudi Zanzibar miaka kadhaa, mpaka sasa kitambulisho cha ukazi Zanzibar wanamzingua, anasema hata uchaguzi ujao wa 2025 inaonekana hataweza kupiga kura, kwa sababu ya huu ujinga. Wakati wenzetu wa nchi nyingine wanapiga kura hata wakiwa nje ya nchi.

Sasa kwa figisu hizi unategemea vipi watu wenye uelewa wa mambo washobokee habari za Utanzania?
 
Mimi nilikuwa na idea kama yako.

Ila ilikuwa kwenye engagement ya social media. Niliona Watanzania wajinga wanaongea sana, halafu wenye akili wako kimya.

Nikaanza kuwatafuta hao waliofanikiwa, wanaofanya mambo ya maana.

Nikamtafuta mmoja anaongoza foundation yenye budget ya $5 billion dollars hapa New York City at that point. Jamaa yuko vizuri kapita Harvard, Tanzania nako yuko well connected kuanzia Ikulu (alikuwa mshauri wa rais) mpaka mtaani.

Nikamwambia nakuomba uje tuongee na Watanzania, mambo ya career, uzoefu wako, matatizo ya Tanzania, fursa za kuyatatua, na chochote utakachopenda. Vijana watapata mengi ya kujifunza kwako.

Jamaa aliniambia yuko tayari kuongea on a small scale setting na watu wachache anaowajua lakini social media ya Bongo ni toxic space. Watu wanapenda fitna na kubishana kuliko kuelimika. Na yeye hapendi ubishi wa kijinga. Na zaidi ana high visibility akianza kubishana bishana na watu mitandaoni inaweza hata kumuharibia kazi yake.

Kuna wakati nilimuona kama selfish lakini kadiri muda unavyoenda na ninavyoangalia mazungumzo ya Wabongo nimemuelewa sana.
 
Jaribu kumcheki Ernest Makuliro wa EBM scholars . Au Kibonde. Au Kada mwenzio loveness mamuya wa.kijani wataku.connect na diaspora.

Wengi wanachoka na sheria. Yanayosemwa sio yanayotendwa kikwete aliwaahidi mengi ila yote yalikuwa siasa. Hata hili la dual citizenship.

Halafu.watu.wanaogopa majungu majungu wakishajulikana basi majungu kwao yanahamia.

Mbona Tundu lissu akienda marekani ana watu.kibao wana msupport kama Ohio wanajitahidi sana kina.Rwabutaza
 
Mange ana matatizo yake tatizo kwenye kushughulikia haya mambo kunakuaga na double standard kiasi kwamba watu wanaanza kufikiri ni kama kukomoana tu.
true,kuna vitu akifanya mburu matata,is not a big deal,lakini akifanya mtu mwenye jina ni issue!
Kuna watu wengi sana wanavunja sheria, wanadhiaki wengine na mbaya zaidi wapo mpaka wanatashia maisha ya watu lakini kwa sababu ni watu wa system au machawa wa chama tawala huwa hawaguswi.
true!
Kosa alilolifanya Mange ni dogo sana ukilinganisha na kitendo alichofanya Bashite cha kuvamia studio za clouds na silaha za kivita lakini hakuchukuliwa hatua zozote.
Kuvamia mahali ni mtu asiye na access ya mahali hapo, media zote ni public access places,RC ni president of regional,has all the rights to Access to all public places including Clouds media, hivyo hakuvamia。
Nakubaliana na wewe Mange ni kichaa lakini izo sheria za kushughulikiana ziwe msumeno kwa wote angalao italeta picha kwamba hakuna conflict of interest za kisiasa
naunga mkono hoja。
Kwa sheria na uchawi wa mpaka kufikia rais wa nchi anasema anataka aone matajiri wanaishi kama mashetani nani yupo tayari kubeba risk ya namna hiyo?
naunga mkono hoja
Hao unaowatolea mfano ni kwa sababu nchi yao ya baba na mama inasupport na kuheshimu mchango wao.
Tanzania tunathamini sana diaspora,hadi wana kitengo pale MFS, na soon tunakwenda kupitisha uraia pacha
Kwa nchi ambayo mawaziri wanatoa macho hadi yanataka kuanguka wakisikia diaspora
is this true?
hamna atakayesema issuez zake kiongozi.
tunaheshimu sana the right to privacy
Its safe to be low profile as a Tanzanian than showing what are your achievements.
tunaheshimu hili pia, lakini kwasababu diasporas wa jirani zetu wako open and transparent,watu wanaona the visibility yao and what they do, kwasababu Watanzania,lie low, ni low profile,watu hatuoni diaspora wetu wanafanya nini, seeing is believing, then tuna conclude kuwa diaspora wa Tanzania, they do nothing!。
Najua habari ndio biashara na maisha yako
its true huu ni mwaka wa 34 kwenye habari,na tangu 2007, niliikwaa LL。B from UDSM, na sasa ni pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea,lakini bado niko kwenye habari。
lakini hamna mtanzania atajitangaza ili awe victim wa kufelishwa na ndugu zake!
naunga mkono hoja
Tubaki JF kuchitchat tu baba, mengine yabaki personal
Japo jf ni ukumbi wa chat tuu, lakini I'll keep fighting for TAK, ili wazo hili lisije likafa kama wazo hili Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!
P
 
My target viewers na audience ni the locals,hivyo ni vipindi vya lugha ya Kiswahili,kwenye mainsteam media。
Waandishi wanejazana ktk vipindi vya lugha moja tu rasmi ya KiSwahili wakati kuna ya Lugha rasmi ya pili Tanzania kiEnglish.
Mimi ni mzalendo, na vipindi vyangu ni vya kizalendo kwa kutumia lugha ya kizalendo ya Kiswahili ambayo ndio lugha yetu adhimu, ila PPR, tunafanya documentaries za English za wateja kama hizi

Kenya wanapiga lugha zote ndiyo maana inasikika kimataifa na kikanda.
ni kweli
Mwandishi nguli anzisha Mapinduzi katika tasni kwa kuitangaza Tanzania na diaspora ktk vipindi utavyotayarisha katika lugha zote mbili rasmi za taifa la Tanzania. Uzuri una uwanja mpana kama mwandishi wakili msomi.
Asante naipokea changamoto hii
P
 
My target viewers na audience ni the locals

Local imekuwa saturated sasa inatakiwa uende kimataifa, habari za Tanzania kimataifa ni chache tena zinatolewa na waandishi wakiwa Nairobi au Johannesburg.

Kazi hii ya kuhabarisha kimataifa kwa kiEnglish tunakupatia wewe maana ni kama hakuna waandishi wote kwa kiswahili wameshamaliza mchezo yamebaki manyoya, ila ukijikita kwa KiEnglish utakuwa Millard Ayo, SnS, Michuzi n.k kwa ujio wa kiingereza kwa soko la nyumbani na kimataifa pia.
 
Diasporas wetu ni ma atheists tu na kazi ya kutumia maneno magumu ya kiingereza hapa JF na X tofauti na hapo kujisifia tu wapo mtoni. Hongera kwa huyo Dada!
 
Asante kwa ushauri,habari inafanywa na waandishi wanaoitwa reporters,mimi stage hiyo nimeipita kitambo,sasa nafanya tuu programs, TAK sio program ya news ,ni program ya analysis,hili eneo bado halina watu wa kutosha。Vyombo Vya Habari Vya Tanzania, Havina Uwezo wa Uchambuzi wa Habari, News Analysis-Jicho Letu
P
 
Kaka Mimi naomba tu kupata fursa huko nje ya kazi hata za kufanya usafi, nk cz nataka kuachana na kazi yangu ya Media Producer & Graphics designer. Asante
Nafungua Bureau huku,nitaajiri Watanzania,hivyo muda muafaka ukifika,huna haja ya kubeba box, utaendelea na media production yako, the only problem ni it takes time。
P
 
Shida kubwa ni siasa za chama chako pendwa, acha kutupia lawama na maswali yasiyojibika kwa hao diaspora waliokimbia nchi kwasababu za kisiasa na hali ngumu ya uwekezaji.
sio diaspora wote wameikimbia nchi kwasababu za kisiasa,au hali ngumu ya uchumi,wako diaspora kibao walikwenda kimasomo,wakawa porched for brain drains na kupewa decent jobs。
p
 
Kuvamia mahali ni mtu asiye na access ya mahali hapo, media zote ni public access places,RC ni president of regional,has all the rights to Access to all public places including Clouds media, hivyo hakuvamia。
Kwa maelezo ya wale vijana wa clouds walishurutishwa kurusha hewani maudhui ambayo RC alikuja nayo pale studio, huo ni uvamizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…