Diaspora Wetu Wanafanya Nini cha Kuonekanika Huko Ughaibuni?. Diaspora Mliofanikiwa, Onekanikeni Kupitia TAK na Rudisheni Tanzania Japo Kidogo!

Okay hao unawaambia waje kwenye hio TAK yako (unatafuta content) je huku kuna watu wa kuwalisha hio content..., na kama wapo je ni wa kutosha ? Hii dunia ya leo ya information overload kupata audience sio lelemama...

Sababu nadhani ungewaambia wanatokea kwenye Forbes au CNN nadhani usingehangaika kuwatafuta wenyewe tu wangekutafuta...
 
Kule kwa RC ku creates TV contents, ni yeye kujiongeza, he has always been doing that, na hata sasa hapo Chuga tayari amejiongeza
Amecreate Soon atarushwa hewani.

Ukisubiri Media ndio wakucretie, utasubiri sana
P
 
Kwa kuongezea kuna mtu alitaka kusaidia zahanati huko kwao Mkoa wa kagera, akaambiwa inabidi apate kibari kutoka kwenye serikali ya eneo husika kuanzia mkoa ahdi wilaya, au aipe serikali huo msaada watafikisha kwenye zahanati husika huo ni utaratibu wa serikali, huwezi kutoa msaada kienyeji, lakini hakusema kama aliombwa rushwa hayo ni maelekezo aliyopewa na wahusika.
 
Mwandishi wa habari na mtangazaji lakini hujui nchi yako inataka kutoa Hadhi maalum kwa diaspora na sio Uraia pacha kama ulivyoandika
Sio kufoka bali kwa mtu kama wewe lazima ungejua tofauti kati ya Uraia Pacha na Hadhi maalum maana limeongelewa miaka hili suala na pia limepelekwa Bungeni na tunasubiri fungu lipatikane tu mchakato uanze

Fuatilia kwanini sio uraia pacha bali Hadhi maalum
Tuje lini mpaka tunastaafu au
 
Kaka mimi naunga mkono hoja yako, siyo hoja mbaya kuwafahamu ndugu zako walioko nje na hata walioko ndani na kufahamu wanafanya nini, wametokea wapi hadi kufika walipo na na ni vipi wanaisaidia jamii waliyotokea.

Ila hili siyo wote wanapenda, hata hapa hapa Tanzania wapo waliofanikiwa lakini hawataki kujulikana au kusema wametokea wapi kufika walipo. Nadhani hili linaweza kuwa linachangiwa na aua utamadini wetu au serikali yetu.

Utamaduni namaanisha siyo kila kabila wanapenda kujionyesha, kuna wapare na wachaga kwa mfano ni wasiri sana, halafu kuna wahaya wao wanapenda watu wawajue na wafahamu yeye ni nani, kasoma kiasi gani, anamaendeleo kiasi gani, au anamiliki nini.

Serikali inachangia kwa sababu, tuna fahamu kuna watu wamefuatiliwa na serikali na kutaka waeleze mali walizo nazo wamezipataje, sasa hili lina watia hofu wengi. Siyo jambo baya, ni sehemy tu ya majukumu ya serikali pia kufuatilia kufahamu, vyanzo vya mapato. Usije ukawa una fadhiliwa na magaidi, au ukawa unauza madawa ya kulevya kitu ambacho siyo kizuri, hivyo usiri siyo jambo la ajabu.

Na pia kuna utashi binafsi, siyo wote upenda kujulikana, na siyo lazima wawe na sababu nzuri au mbaya, ila basi tu.

Mwisho, mimi nataka kusema maendeleo ya mtu siyo lazima yarudi aliko toka, anaweza kuamua kuhama jumla. wapo wanaohama kutoka bara hadi bara, wapo wanahama, nchi hadi nchi, na wapo mkoa hadi mkoa, na wapo wana hama wilaya hadi wilaya , na wapo wana hama mji au mtaa hadi mtaa. Hii ni mapenzi binafsi ya muhusika.

Kwa mfano wewe, sidhani kama unampango wa kwenda kuishi Mwanza au Shinyanga, kwasababu umekulia na kuishi Dar es Salaam na kufanya ndiyo makazi yako ya kudumu, sasa kwanini ukawekeze Mwanza?

Hivyo kuna watu walihamia nje ya nchi na wakaamua kwamba huko waliko ndiyo makazi yao ya kudumu, sasa kwanini wapoteze pesa(Resources) kuwekeza walikoondoka kama hawahitaji kuridi huko?

Kwa taaluma yako ni kawaida kuchokoza hoja, lakini isiwe kama kuna ulazima wa wahusika kushiriki. Ikiwa wapo waliokubali, waheshimu, ikiwa wapo wasiokubali pia wape heshima kwa hilo, ni maamuzi yao. Ukiwananga wataona kama unawalazimisha kuwashindanisha, yani nani zaidi kitu ambacho siyo nia yako na hakina tija kwenye kipindi chako na kwao pia.

Unaponzisha kipindi kifanye kiwe endelevu, kisianze na kufa, au kisiishi muda mrefu.

Nikutakie kila la-kheri huko ugaibuni, wasalimie wote uonanao nao. Tutasubiri kuona kipindi hewani. natumaini tutajifunza na kuelimika kupitia kipindi chako.
 
Kuna mtu alikuwa anataka kutoa msaada kijijini kwao Tanga akaambiwa hospitali ndogo ya kijijini kwao haiwezi kupata msaada wa vifaa vile kabla ya hospitali ya wilaya!
 
Kuna mtu alikuwa anataka kutoa msaada kijijini kwao Tanga akaambiwa hospitali ndogo ya kijijini kwao haiwezi kupata msaada wa vifaa vile kabla ya hospitali ya wilaya!
Inawezekana kwenye hili kwasababu, kuna vifaa vinahitaji taaluma kubwa wa watoa huduma, ambao kwa level ya kituo cha afya hawakuwa na wataalam wenye elimu ya kuvitumia kutoa huduma husika. Kwa mfano, kuna vituo vya afya havina X-Ray machine, siyo kwa kukosa, ila kuna mahitaji yanayosimamiwa na vyombo husika kabla hujasimika mtambo wa x-Ray ili kulinda afya za wananchi wasipatwe na mionzi ikawadhuru, hivyo hilo pia ni sawa siyo kila kitu ni ukiritimba.

Na unaweza kukuta kituo cha afya wahufdumu wake hawana elimu ya kutosha kuvitumia, hivyo ikawa msaada hauna maana eneo husika. Huu ni mfano tu, sitetei wala sijengi hoja kukupinga, au kuhalalisha lililotokea.
 
Walichomaanisha ni kwamba hata ukitoa msaada wa wataalam, kituo cha kijiji hakistahiki kupata vifaa fulani kabla ya kituo cha wilayani.

Ni sheria za ukiritimba wameweka tu.
 
Warudishe kipi ambacho ninyi mliwapa? Passport zenyewe wamezipata kwa mbinde na rushwa juu halafu leo unasema warudishe
 
Huu ndio uhalisia wa ughaibuni

Mafanikio sio bahati bali ni; uelewa, jitihada na kujiamini.

Sasa ukiweza fanikiwa ughabuni, uwezi shindwa kufanikiwa Tanzania.

Mafanikio ni culture (way of thinking), ughaibuni hakuna mtu anaepambana kufanikiwa au aliefanikiwa atataka ku-deal na watu wasio kwenye level yake ya kufikiria.

Waelewa wengi wanajua source of funds, nje ya mifuko yao kama wanashida ya kuwekeza Tanzania; mbinu ni kuandika business plan tu.

Kama unavyoona ‘Chris Lukosi’ analeta mazaga-zaga yake, kuna watu wanaweza kukuletea vifaa vyote vya medical equipments kuanzia kwenye vitanda vya kisasa mpaka all kinds of scans (be, it used).

Achana na hao wanaojenga vyoo vya zahanati kuna watu wanaweza kukuletea vifaa vya hospitali SAFE na Aghakhan hawana, na wana business strategies za kuinua uchumi Bashe hana.

Muhimu ni serikali ya Tanzania kubadili culture, kuomba development proposals za diaspora (na lazima muwape, data sahihi ili waandike vitu vya maana).

Sasa ili uweze kuweka strategy sahihi kwa proposal ya mtu kama unadhani ina faida kwako, łipia consultation fees ili akupe mbinu za kusimamia strategy upate mafanikio (mkono, mtupu aulambwi).

Otherwise kutafuta suluhisho la kudumu, wekeni watu wenye akili waongoze nchi.
 
Miaka kama sita iliyopita hapa nilipo kuna jamaa ni Civil Engineet huku kijijini kwetu mimi na yeye hatujuani wala sijawahi kumsikia katika maisha yangu.

Sema kuna dada mmoja anamgonga (side chick wake) najuana nae ananipigia hoo kuna mtu kanunua ‘Bed and Breakfast’ on the beach front nenda kamsaidie ku-manage atakulipa vizuri nikamuona taahira mwingine tu.

Diaspora wa Tanzania kwa sasa ni wazawa sema wenye mafanikio hawana huo muda wa kujitapa, washakuwa na tabia za kizungu,
 
Walichomaanisha ni kwamba hata ukitoa msaada wa wataalam, kituo cha kijiji hakistahiki kupata vifaa fulani kabla ya kituo cha wilayani.

Ni sheria za ukiritimba wameweka tu.
Huu pia ndio utaratibu wa Waisrael, binti mdogo, hawezi kuolewa kabla ya
binti mkubwa.

Hivyo ikitokea umempenda binti mdogo, ukamchumbia, akamlipia mahari, siku ya harusi kwa kawaida hufanywa usiku huku binti amejitanda ushungi.

Unakabidhiwa binti gizani, unafanya defloration, asubuhi ndipo unagundua kuwa umeletewa dada mtu
na sie yule uliyempenda.

Unakwenda ku complain kwa baba mkwe , ndipo unaelezwa kuwa kwa mila zetu, binti mdogo hawezi kuolewa kwanza kabla ya dada yake, hivyo unatakiwa kutoa mahari nyingine, ndipo ukabidhiwe na binti mdogo.

Kila kitu kina levels kuanzia chini, shule, hospitali, mahakama, hata nyumba unaanzia msingi.

Wakati wa Covid 19, DICOTA walitoa msaada wa madawa na vifaa tiba, ilikuwa shughuli!. Nikakumbuka makontena
ya Makonda.

Hii maana yake, unaweza kuta kuna wana diaspora wengi tuu, wana moyo na nia ya kusaidia nchi yao lakini vikwazo wanavyokutana navyo, vinawavunja moyo.
P
 
Ukiritimba wa kijinga tu na logical fallacies za argument from tradition.
 
Ukiritimba wa kijinga tu na logical fallacies za argument from tradition.
Ukiritimba ni kweli upo, fallacies pia zipo, ila pia kuna some logical as well. Kama mtakumbuka enzi za misaada yenye masherti, anayesaidia ndie anaamua asaidie nini, watu hawana maji, barabara wala kituo cha afya, wanaletewa mradi wa bembea za watoto.

Wafadhili ndio walikuwa wanaamua watafadhili nini, Nyerere alikataa, Mwinyi akakubali.

Mkapa akawaelimisha watuulize tuna shida gani na tunahitaji nini ndipo watusaidie, ndipo basket funding ikawa introduced, fedha zote za wafadhili zinaingizwa kwenye kapu moja, na sisi ndio tunaamua tufanyie miradi gani, including general budget support.

Japo beggers can not be chooses, mtu mwenye njaa ya kitoweo, badala ya kumpa msaada wa samaki, ale, akimaliza aombe tena, na tena na tena, hivyo kuwa ni omba omba, mfudishe kuvua samaki, mpatie nyenzo za uvuvi, ajitegemee.

Ndio maana tulishauri Hata Nyerere alikataa, Rais Magufuli usikubali, shikilia msimamo. Tanzania tusikubali misaada na mikopo yenye masharti kuingilia sovereignty yetu
 P
 
Hili ni jambo la maana umeleta na ninajua diaspora wengi wanaipenda sana nchi yao Tanzania nawasaidia sana familia zao.
Kitu kinacho wasitisha ni Sheria zetu za uwekezaji hasa kwa diasporas aidha hazijulikani au zinatumika kibabe kuwaweka kwenye wasiwasi au suspence.
Pia ni taabu wao
Kuwekeza kwa jina la ndugu sababu uaminifu kwenye mambo ya mali ni kitu adimu sana hapa kwetu
Sheria itoke tu kua Wana haki kama watanzania kwenye biashara na umilikaji uone kazi ya wanadiaspora kwa mitaji na uzoefu utakao kuja kwa maanufaa ya TZ yetu.
 
Wewe na viongozi ni sehemu ya tatizo na hamna diaspora waonajielewa watafanya kazi na nyie. I guarantee you hii agenda yako itafeli.
 
Wewe na viongozi ni sehemu ya tatizo na hamna diaspora waonajielewa watafanya kazi na nyie. I guarantee you hii agenda yako itafeli.
Kauli huumba, kwasababu Mungu na shetani, wote wawili hukaa ndani yetu, ukiwaza mema, ukisema mema na kutenda mema, yote hayo ni ya Mungu aliye ndani yako, hivyo mtu ukimsemea mema, kauli yako inamuumbia mema na yanatokea.

Ukiwaza mabaya, kusema mabaya na kutenda maovu ni shetani aliye ndani yako, hivyo hii kauli yako inaweza kweli kuniumbia kufeli.

Kwa vile mimi ni mtu very honest (ukiondoa mambo
Yetu yale) na kipindi cha TAK, ni kipindi very genuine kusaidia, hakina any ill motives wala agenda zozote, then wish yako ni wish ya kishetani, kikifeli ni shetani
ameshinda, nitakuwa sina jinsi kwasababu kuna wakati Mungu humruhusu shetani kushinda.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…