Dickson Job na Ladack Chasambi wametemwa kwenye kikosi Cha timu ya Taifa

Dickson Job na Ladack Chasambi wametemwa kwenye kikosi Cha timu ya Taifa

DAR ES SALAAM: KAIMU Kocha Mkuu wa @taifastars_ Hemed Suleiman Morocco ameita kikosi cha wachezaji 34 kujiandaa na mchezo wa Juni mwaka huu dhidi ya Zambia, kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 nchini Marekani, Mexico na Canada.

MAONI YANGU : Dicksoni Job na ladack Chasambi wamekua na wamekua na kiwango kizuri huu ndiyo ulikua wakati mzuri kwa vijana kutumika Taifa stars Lakini kuna ujanja ujanja mwingi na kujuana kwa wanaopanga kikosi.
View attachment 3000152
Hivi huyu kocha Mzanzibari amewahi kufundisha timu gani kwa mafanikio au kwakuwa ni Mzanzibari na bibi yule yuko madarakani?
 
Job anacheza team inayo dominate Bongo unaenda mwaka wa tatu sasa, ni starter na vice captain pia hiyo nidhamu ni kwenye team ya taifa tu mkuu?
Unaelewa nini kuhusu neno NIDHAMU?
Mwenendo wa Simba SC ulikuwaje kipindi Maximo anamkataa KASEJA kutokana na utovu wa nidhamu?
 
DAR ES SALAAM: KAIMU Kocha Mkuu wa @taifastars_ Hemed Suleiman Morocco ameita kikosi cha wachezaji 34 kujiandaa na mchezo wa Juni mwaka huu dhidi ya Zambia, kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 nchini Marekani, Mexico na Canada.

MAONI YANGU : Dicksoni Job na ladack Chasambi wamekua na wamekua na kiwango kizuri huu ndiyo ulikua wakati mzuri kwa vijana kutumika Taifa stars Lakini kuna ujanja ujanja mwingi na kujuana kwa wanaopanga kikosi.
View attachment 3000152
tunamuamimi zaidi kocha mwenye utaalam na sisi wengine makocha wa vidole na mahaba ya vilabu tukae tu kimya
 
Dickson Job na Chasambi ni vijana na ni wachezaji wazur sana ni kocha kichaa tu ndio anaweza kuwaacha kujumuika kwenye kikosi chake.
 
Ifike kipindi tuache makocha wafanye kazi wewe shangilia timu ikishinda ikifungwa kalale mapema!
 
Ni kweli iko chini sana tena sana.
Wewe ambaye upeo wako wa kufikiria uko juu nifumbue macho na hasa kwa kuweka wazi chanzo halisi na kisababishi kikuu cha unachokiita bifu kati ya Dickson na Mwl wa timu yetu ya taifa halafu sasa kupata upembuzi wa nini akifanye Dickson Job ili kulimaliza hilo.

Mimi ninachokifahamu ni kwamba ktk mchezo baina ya timu yetu na DRC Job hakuwepo kwenye kikosi cha kwanza kwa awali kabisa lkn baada ya Mwl kuona kikosi cha mpinzani akaamua kubadili maamzi kabla ya kuingia uwanjani Dickson aanze badala ya Mwaikenda.
Dickson akagomea maamzi ya Mwl kwa kusisitiza kuwa kwakuwa alikuwa ameshaandiliwa kucheza basi acheze huyohuyo.

Sasa kama hizo ni taarifa za kweli unataka Mwl amuite Dickson ili akafafanye naye nini?
Wewe huoni kwamba kutokuwepo kwa Job kunatoa nafasi kwa vijana wengine kuonesha vipaji vyao?

Lkn bado ninakuomba uweke wazi ili nami niondoe dhana niliyonayo dhidi ya Dickson Job.
Mfano, labda Mwl alimuomba atoe sehemu ya posho yake ya siku ampe Mwl ili awe anamuanzisha kikosi cha kwanza.
Naziweka shukurani zangu hapa chini mkuu.
Reasoning yako iko low sana, umeshinda mkuu
 
Dickson job hana heshima na hii ni kawaida kwa makocha wazawa kudharauliwa kwa akubali kucheza right back kwenye club yake lakini national team anakataa kucheza.
 
Back
Top Bottom