Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Pastor Anafunguka...
Sijawahi kuona kampuni ya vilevi kama vile pombe ambayo inamtumia mteja wake mmoja aliyelewa huku anapigana na watu baada ya kulewa kwenye tangazo lake! Au amelala mtaroni kwa kuzidiwa na pombe, au amejisaidia (amejinyea na kujikojolea) huku anaongea mwenyewe maneno yasiyoeleweka! Haya yote pombe inayafanya lakini hata wao kampuni ya vilevi wanaona aibu kwa wateja wao kuwa wawakilishi na mabalozi wao kwa jamii.
Uwe na Uhakika
Mungu hawezi kuwakilishwa na waimba ngono, bangi, sigara, ushoga, shisha, clubbing na taka taka nyingine kama watumishi wake endapo bado wako huko wakifanya hayo.
Kama hawaiamini Injili kwanza na kutubu dhambi zao na kugeuka, kufunguliwa toka kazi zao mbaya zinazoiharibu jamii, hawawezi kuitwa watumishi wa Mungu kama sisi ambao tumeishaamua kumuishi Kristo na kumzalia Mungu matunda yapasayo toba!
It is Higher Time to Speak the Truth
Neema ni ya wote lakini ambaye hajaikubali si wa Bwana bado,
Kila amwaminiye asipotee,
Lakini kama hajaamua kuamini bado na kugeuka, si mwana wa Mungu wala mtumishi wa Mungu.
Tuilinde imani hii tuliyopewa mara moja kwa wivu mkubwa,
Wanetu watakuta kitu cha ajabu tusipoisimamia kweli yote.
Askofu Dickson Cornel KabigumilaABC Global Duniani